DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria



Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.

=====

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).

Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.

Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi


Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.

Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.

Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.

Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, wajiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.

Waislam huyu sheikh wa BAKWATA rafiki yake askofu mokiwa aliyepigwa chini kanisa anglikana kwa sababu hizo za kujitanabahisha na CCM. Mpigeni chini huyu ni hasara kufanya taasisi ya kiislam kuwa tawi la CCM
 
Mtazamo wako tu.Unashauriwa kwenda mbele zaidi ukijua kuwa hawa ni binadamu sio malaika
Nafahamu ndugu Yangu
Ustaarabu huwa unatafutwa kwa udi na uvumba
Mtu huvuna apandacho
Sasa wewe uanze kunyosheana vidole na mitusi kwa wakuu wa dini kisa kufurahisha kadamnasi!
Eeh Mola wangu nipitishe katika njia ya kukupendeza kwa ajili ya kizazi changu na taifa langu!
 
Ninacho jaribu kukuelewesha ni kuwa!
HUKUMU YAO MWACHIENI ALIYO MWEKA HAPO!
Sijasema kwamba wao ni watakatifu!
Ungeijua hiyo story ya MFALME SAULI NA DAUDI ndiyo ungejua nia Yangu ni nini!
Tujaribu kusoma hivi vitabu vya dini, yeyote tu, huwa vinasaidia sana kutupa mwongozo wa maisha haswa kwa vizazi vyetu na hata taifa kwa ujumla!
Mimi navijua vitabu vya dini na hata ishu ya Saul ni hekima tu ya Daudi iliyomwongoza kutomwua sawa na mtu mwingine yeyote anavyoweza kufanya lakini ni Daudi huyo huyo aliyeamuru kuuawa kwa URIA kisa kanogewa na penzi la mke wa Uria na Mungu alimwadhibu katika hilo so usimtumie kama mfano katika hili.
Mbali na hayo kama tunaamini hukumu aachiwe Mungu iweje huyu sheikh aamue kumtisha dada yule si amwachie Mungu kama kawaida basi?

Huyu sheikh ni mjinga kabisa ona sasa stori zake zote zimemwagwa hadharani ataweka wapi uso wake?
 
Hao ulio wataja wamevurugana na serikali sio mtu binafsi!
Sijui kama unaipata point Yangu!
Hawa watu sio wa kugombana nao maana NI SAWA NA KUJIPALIA MKAA KICWANI AU KUFUNGIWA JIWE KIFUANI NA KUTUPWA BAHARINI!
BELIEVE ME!
Siku hizi hata mawakala wa shetani wamejichomeka kuwa viongozi wa dini,sasa wewe endelea kumuamini kila anaejiita kiongozi wa dini ni mtumishi wa Mungu utakuja shangaa
 
Kwa sisi tuliosoma lugha,Ukipewa speech na kueleza nini hasa lengo/dhumuni la fanani kwa hii conference ya Sheikh ni Kumjibu Mange tu,nimeona amesema swala la kwanza ni kuhusu Mufti zuberi lakini amelipa dakika moja au mbili na dakika zaidi ya 10 akimuelezea mange.

Siungi mkono kitendo cha mange kumtukana Sheikh wa DAR kwamba ni Mngese na pia siungi mkono kitendo cha sheikh kumwambia mange mwisho wa kusema ni mwaka huu basi.

Kauli aliyoitoa Sheikh sio nzuri kabisa,what if Mange ndani ya mwaka huu akapata ukichaa? Unadhani watu watamuhisi vipi Sheikh? Kila binadau ana kichaa chake,nani alikuja kujua Kisando atakuja kuwa chizi? Tuondoe hilo,hatuombei mabaya mungu haepushie mbali,no one knows 2mrw,waht if Dada wa taifa kadondoka ndani ya mwaka huu,unadhani jamii itamchukuliaje Sheikh wa DAR?

Ukiangalia vizuri hiyo interview,Sheikh amejaa upepo sana,anaonyesha amekasirika sana,wakati vitabu vya dini vinasisitiza kusamehe hata 7 mara 70 lakini yeye kaonjeshwa kidogo tu na mange akawaka,viongozi wa dini huwa wanatufundisha tusamehe waliotukosea lkn kwa yeye naona hajataka kumsamehe bali ameenda mbali na kuwa na uhakika kabisa kwamba Mange Mwaka huu ndio wa Mwisho Kuongea how? Kwa wanaomjua mange hajaanza kutukana online leo,binasfi nimeanza kumfahamu miaka ya 2008 alivyoanza kuchambana na TK.

Namuomba Sheikh afute kauli yake aliyoitoa haiakisi hekima ya "Mtumishi wa Mungu" anavyotakiwa a-act pindi akiingizwa kwenye majaribu,aite tena waandishi afute kauli,ile kauli ni nzito sana,maana kitu chochote kitakachomtokea Mange watu wengi wataahisi Sheikh kafanya mambo,Je ikitokea hilo(Hatuombei litokee) unafikiri watu wake nao watatulia? Wakisema yeye amtumia mahakama ya Mungu na sisi tunatumia Sheria Mahakama ya mkononi hapo kutakuwa na Amani?

Theory of a karma,ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga,what goes around comes around....To Every Action there is an equal and opposite reaction.
 
Nasikitika sheikh kutopewa maelekezo ya awali..kuhusu impact ya kuvuliwa kanzu na huyu dada wa mbele
 
Mimi navijua vitabu vya dini na hata ishu ya Saul ni hekima tu ya Daudi iliyomwongoza kutomwua sawa na mtu mwingine yeyote anavyoweza kufanya lakini ni Daudi huyo huyo aliyeamuru kuuawa kwa URIA kisa kanogewa na penzi la mke wa Uria na Mungu alimwadhibu katika hilo so usimtumie kama mfano katika hili.
Mbali na hayo kama tunaamini hukumu aachiwe Mungu iweje huyu sheikh aamue kumtisha dada yule si amwachie Mungu kama kawaida basi?

Huyu sheikh ni mjinga kabisa ona sasa stori zake zote zimemwagwa hadharani w wapi uso wake?
Uria alikuwa ni askari
Sauli alikuwa ni mfalme na mpakwa mafuta wa Mwenye Enzi Mungu
Hapo ni tofauti kubwa sana kama unanielewa ninavyotofautisha kati ya wakuu wa dini na mtu wa kawaida!
Kwa Sheikh kuwa na nafasi hiyo sio kitu cha mchezo mchezo!
Ukiisoma Zaburi ya kwanza utanielewa zaidi!
Uwe na usiku mwema
 
Siku hizi hata mawakala wa shetani wamejichomeka kuwa viongozi wa dini,sasa wewe endelea kumuamini kila anaejiita kiongozi wa dini ni mtumishi wa Mungu utakuja shangaa
Sina muda wa kuwatukana au kujibizana nao
SI HERI MTU WA DINI KULIKO MUUZA BAR
HERI MISIKITI NA MAKANISA NA MA TEMPLE KULIKO MADISCO!
Ukiwa na watoto utanielewa!
Gd9t
 
Alipewa na hakuyasadiki akidhan vitisho vitamtisha dada angu mpenz
Amuulize mzee wa upako..alitishia mwandishi kuwa atakufa mwezi may..kwa kuanika habari zake za kunywa faru John aka Bapa kubwa..mwandishi hadi leo yupo hai..ni mwaka unaishi

Myths of the story..Mwanadamu huwezi mpangia mwenzio muda wa kuoshi
 
Mbona namna alivyokuwa akiongea inafanana na zile video za akina nanii kule wapi sijui tofauti tu hakuna ile kaniki.
 
Back
Top Bottom