DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Alaf sio kila mbwa akubwekeae umrushie jiwe angetulia huyu Shekhe angechukua credit nyingi lakin kwa alichokifanya mmmmmmh
 
Da mange anawapa za kiukweli balaa.
Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana. Taifa limegawanyika kabisa
 
Sijawahi kuona shehe anaombea watu vifo...kiukweli huyu shehe kaharibu taswira ya uislamu
 
Aliyemshauri sheikh amjibu Mange amekosea sana! Huyo sheikh anajutia bila shaka!
 
Huo ni Mkutano wa CCM Temeke mwaka 2014 na yeye alienda pale kama Mgeni Mwalikwa! Na ulikuwa ni mkutano wa ndani wa kuchagua viongozi wa Jambo!!

Don't forget, huyu Sheikh carrer yake kaanzia Temeke.
68917b6657e0c383f12acda7c6b2da64.jpg


Na hapa Shekh alikuwa kwenye kongamano la nin labda?...

Kwanin hamtaki kuukubali ukweli,Shekh ameambiwa ukweli yy aliwasema viongozi wenzake wa dini kuwa wasichanganye siasa na dini,ila yy anapoonekana kwenye majukwaa ya siasa anatangaza injili sio?!,
 
Aliyemshauri sheikh amjibu Mange amekosea sana! Huyo sheikh anajutia bila shaka!
Hata hivyo kuna ambao walimpa rai aache kumjibu huyo dada lakini hakutaka ushauri wao. Kuna tatizo mahala
 
Hilo la kujipa nafasi ya kuhukumu, anyway... kwangu naona ni very completed kuliko tunavyochukulia!!

Tusisahau, huyu sio mwanasiasa kwamba keshazoea kuoga matusi! Watu kama akina JPM wanafahamu kabisa kwamba kuoga matusi itakuwa ni sehemu ya maisha yao!!

Kinyume chake, huyu ni kiongozi wa dini... wala hana uzoefu wa kutukanwa hovyo hovyo tena bila sababu! Mbaya zaidi, ni mtu mzima! Halafu anaibuka mtu from nowhere na stori za uongo na kuanza kumwamgia matusi mazito mazito!!

Man, simuungi mkono suala la kuapiza lakini jaribu kuchukua nafasi yake! Nae ni binadamu... usitarajie eti kwavile ni kiongozi wa dini ndo basi wala haitamuuma kuambiwa mse'nge... tusi baya kuliko yote kwa mwanaume!

Suala la kumjibu Mange... naona ukisoma maoni ya watu wote yanaashiria kitu kile kile ambacho Sheikh amekisema! Kwamba, Mange anatumia matusi kama njia ya kuwatisha watu na kweli 99% ya watu wanamuogopa sana Mange kwa sababu tu ya kuogopa atawamwagia matusi!

Hatujui tu lakini ukweli ni kwamba Watanzania wapo vifungoni na aliyeshika funguo za Mahabusu ni Mange!! Na Mange hilo analifahamu ndo maana amejawa na kiburi kwa sababu tu anafahamu watu wanamuogopa kwa ajili ya matusi yake! Ni kwamba ameshapewa free pass ya "usimguse huyo... hivi unamjua vizuri wewe!!!"

Sheikh amegoma kuwa mfungwa!! Na amesema wazi kwamba watu walimuonya asimjibu kwa sababu atazidi kumwagiwa matusi! Sheikh Mkuu akagoma kuwa terrolized hata kama alifahamu haya yangetokea! Na kwenye Uislamu, kujitia unyonge wala sio sifa ya uchamungu!

Na hapa ndipo Waislamu wanapoonekana wakorofi manake kujitia unyonge kwao wala sio sifa!!

Mkuu Chinge nimekusoma kwa uzuri kabisa..

Mimi simuungi mkono huyo mwanadada hata,kwani anachokifanya sio kitu kizuri na hakikubaliki kwa jamii zetu za watz .

Na pia siungi mkono kiongozi mkubwa na mwenye dhamana kuanza kumjibu huyo Dada kwasababu anajulikana tabia zake najua hata Shehk anamjua vizuri...,kinachotokea sasa ni muendelezo wa matusi kutoka kwa Mange,kwa jinsi ninavyomfahamu Mange hajawahi kuonesha unyonge pale anapokuwa Attacked na mtu yoyote yule na hili Shehk analijua..,sasa kitendo cha yeye kutokuonesha uvumilivu kitamgharimu sana tena saaanaa.

Kengine ambacho sijakipenda ni ile hali ya kujipa nafasi ya Mungu ya Kuhukumu na hapa naongelea kiimani zaidi na kwa mujibu wa sheria ni makosa..,hili ni kosa la Jinai maana ametishia.

Mkuu Chige huo ushauri wa yeye kushauriwa kukaa kimya alafu akakataa utamgharimu sana.
 
Kuwa katika position kama yake sio kitu cha mchezo mchezo tu

Maana ingekuwa ni rahisi hata wewe ungekuwa hapo
Lakini ana kipawa ambacho Mwenye Enzi Mungu anemtunuku!

Ndiyo maana kwenye Biblia Takatifu Mfalme Daudi hakuthubutu kumwuua Mfalme Sauli, tena alimwita mpakwa mafuta wa Mola, akamwambia Mwenye Enzi Mungu pekee ndiyo atakaye kuhukumu!

Hivi viti wanavyo kalia wakuu wa dini sio vya mchezo, ni watu wanao shika roho za watu yaani ni IMANI!

Tuwe wasngalifu sana kwenye maswala haya!

Tusiwafanye wakakunja roho zao!

Kweli nawaambia mwisho wake huwa sio mzuri hata!
Mtazamo wako tu.Unashauriwa kwenda mbele zaidi ukijua kuwa hawa ni binadamu sio malaika
 
Nimeshaona mkuu.

Shehk kafanya kosa kumjibu huyu dada,angekaa kimya tuu ili kulinda heshima yake.
Halafu huyu sheikh sijaelewa povu limemtoka kwa sababu gani. Ndio maana msikitini kwake huwa siendi kusali. Amekaa kimjinimjini sana huyu sheikh.
 
Hii nayo ni double standard Mahakama ya kumshitaki Mange eti ipo mbiguni ambapo hakuna rushwa lakini ya JF ipo hapa hapa DSM maana yake mahakama za rushwa! au mimi ndo nimemuelewa vibaya huyu Kada wa sisiemu.
 
Sawa nafasi aliyonayo ni kubwa sana lakini kaamua kuidhalikisha kwa sababu ya njaa na tamaa ya mali ndo maana kaamua kuitumbukiza siasa katika kipawa chake ili tu afurahie maisha ya duniani huku akihubiri wenzie wasiangaikie msisha ya duniani(UNAFIKI)
Utajiju kwa kweli
Mimi huwa nawa heshimu sana wakuu wa dini zote!
 
Ni wapi alipochanganya dini na siasa?! Umeshaambiwa, ile picha ambayo watu walikuwa wanatandika ubwabwa ilikuwa ni msibani... kuna Sheikh kafariki K,nyama na Sheikh Mkuu alikuwa pale. Jama wa CCM walipomuona, wakaenda kumjulia khali.

Ile picha nyingine ilikuwa ni ya mwaka 2014... sasa ni wapi huko ambako kachanganya dini na siasa?

Inaonekana watu hamfahamu tafisiri ya kuchanganya dini na siasa!

Kiongozi wa dini kuwa kwenye shughuli za siasa huwezi kuita ni kuchanganya dini na siasa! Hakuna sheria inayokataza viongozi wa dini kushiriki shughuli za kisiasa... kinachokatazwa; wewe upo msikitini au kanisani unaanza kuhubiri siasa... huko ndo kuchanganya dini na siasa!!

Au hata kama sio msikitini/kanisani, unafika kwenye halaiki, hususani kipindi cha kampeni kama hiki halafu unatumia nafasi yako kama sheikh au askofu, kumpigia mtu wako kampeni!
Heri yao wale wasioona lakini wanaamini!
 
Kma ni mtanzania ana haki ya kuwa mwanachama wa chama chochote anacho kiona kina faa na kma ni kada wa ccm ,sio kosa kisheria kumpigia kampeni mgombea wa ccm ,
 
Kma ni mtanzania ana haki ya kuwa mwanachama wa chama chochote anacho kiona kina faa na kma ni kada wa ccm ,sio kosa kisheria kumpigia kampeni mgombea wa ccm ,
Binafsi sioni mantiki ya Sheikh kulalamika labda kama ametukanwa!
 
Unamaanisha viongozi wa dini kama Baba Askofu Niwemugizi aliyeundiwa zengwe la uraia wake au unamaanisha kiongozi wa dini kama sheikh Ponda ambaye kila siku anapelekwa polisi na kulazwa ndani bila sababu...hebu tuwe serious kidogo aisee...kwahiyo viongozi wa dini type ya kina Nabii Tito na huyu sheikh wa dsm ndio wateule wa Mungu waachwe wataadhibiwa na mungu tuu...ahahahhaa. MANGEEEEEE...NYOOSHA HAWA WENGINE MUNGU ANA MAMBO MWNGI YA KUFANYA HAWA MALOZANA NAO HUKUHUKU AHERA HESABU TUU.
Hao ulio wataja wamevurugana na serikali sio mtu binafsi!
Sijui kama unaipata point Yangu!
Hawa watu sio wa kugombana nao maana NI SAWA NA KUJIPALIA MKAA KICWANI AU KUFUNGIWA JIWE KIFUANI NA KUTUPWA BAHARINI!
BELIEVE ME!
 
...sheikh ubwabwa huyu anatumika Na watawala wa ccm...amejiharibia sana kuanza kulumbana Na mange..!yeye kama hapendi anachosema mange ana angalia kwanini page za insta za mange???kama anachosema mange si kweli kwanini ahangaike nae????

...ona sasa tumejua anapenda mku.ndu...haya amejitakia mwenyewe... Alafu anatishia mtu maisha....yeye amekuwa Mungu????..wachawi ndio wanaotishia vifo watu...
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] unahis mange kule hana security ya kutosha basi jidanganye

Hana chochote usidanganyike, umarekani ukitaka kula lazime ufanye kazi hakuna cha bure wala cha mjomba. Mlinzi bei yake waijua?

Kama ana uwezo asingenyanganywa watoto NA mtalaka wake. Umarekani mama kunyanganywa watoto ni mama mwenye malezi mabaya au mchafu kitabia NA blogs zake zinadhihirisha.

Hao wanao tukanwa wafanye maamuzi magumu.
 
Hivi huyu shekh si aliambiwa amuache asimjibu sasa ameona ubishe wake?
Duh insta mambo ni fire aieseee
 
Back
Top Bottom