DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

HV KUMTISHIA MTU MAISHA SI KOSA LA JINAI? DAH! SHEIKH, BAHAT MBAYA AMESAHAU KUWA AMEBEBA DHAMANA YA WAUMIN NA KUJENGA PICHA KUWA DIN YAKE NI YA VISAS NA VITISHO.

MANGE KAKOSEA ILA SHEH KACHOCHORA ZAIDI.. ANGEMPUUZA, ANGEPATA MAKSI.
 
kumbe na wewe unaenda kwenye page ya mange?....ndio maana una akili ndogo kama piriton
Kuna shida gani kwenda huko na kusoma hizo Habari?
Nilichogundua ni kuwa watu wengi walio na mahusiano ya karibu na Bashite huwa maisha yao binafsi ni ya ajabu ajabu sana. Na kuwa karibu na Bashite ni balaa kwani lazima utakuja kuumbuka mbele ya jamii, wapi lemutuz siku hizi? Muro jee? Sasa shehe wetu.
Hakika muhimu ni kujitenga na Bashite huenda ana laana
 
Huu mzozo katika ya Bakwata na Mange Kimambi ni hatari.
 
Tuhuma hubaki kuwa tuhuma mpaka pale itakapothibitika... Kinyume chake hugeuka kuwa uzushi..

Wachina wana taratibu zilizonyooka sana... Kitendo tu cha kutumiwa kinakulazimisha kuondoka kwenye wadhifa ama nafasi uliyonayo mpaka itakapothibitika vinginevyo... Kama tuhuma husika zilikuwa uzushi umewini na aliyekutuhumu inakula kwake.... Lakini kuna swali hubaki hewani... Kwanini utuhumiwe wewe?

Tuhuma humuondolea mtu heshima... Humuondolea mtu uaminifu na kuaminika... Hufedhehesha na kuleta aibu kwako na kwa jamii yako... Tuhuma za wizi rushwa na uasherati huwa na uzito wake tofauti kabisa na tuhuma nyinginezo kama uchawi nk...
Anapotuhumiwa mtu wa kawaida... Haiwi jambo kubwa sana kama anapotuhumiwa kiongozi wa kiserikali ama wa kisiasa au kijamii... Lakini pia tuhuma za kiongozi wa kijamii pia zinaweza zisibebe uzito sana kama tuhuma za kiongozi wa dini.. Na pengine kiongozi mkubwa wa dini...

Kiuhalisia na kijamii pia bila kusahau kiimani... Tuhuma si jambo jema, si jambo la kheri kabisa.. Hufedhehesha na kutia aibu... Muungwana ni kitendo... Mtu anapaswa kuonyesha uwajibikaji na kujali kwa kujiuzulu mpaka tuhuma zitakapothibitisha vinginevyo... Na hii ni kutaka kulinda heshima yako, ya familia yako na jamii nzima unayoiongoza... Kujiuzulu hakumaanishi kuwa ni kweli umetenda bali ni kutoa nafasi ili kupisha uchunguzi na kuepusha sononi kwa jamii yako... Yaani matendo ya tuhuma zako visihusishwe na cheo wala imani yako

Kuna kiongozi mkubwa wa dini (Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam) kashauriwa vibaya na pengine kwa kughafilika akasahau weledi.. Akasahau dhima na wajibu wake katika jamii... Akaitisha press conference kutoa vitisho ama unabii kuwa kuna binti mwanaharakati Mitandaoni maarufu kama Mange Kimambi huu ni mwaka wake wa mwisho kuishi kutokana na kuwatukana viongozi na watu mbalimbali... Nadhani akiwepo yeye

Hili halikukaa vizuri sana kwakuwa kisheria nj kwamba kiongozi wa dini ametoa kitisho cha dhahiri cha kuangamiza.. Yaani ametishia kuua... Hapa ndio Mange kapashikia bango.... Matamshi ni kama risasi ikitoka imeroka haina rivasi... Kiongozi hakupaswa kuyasema yale... Naamini kuna mfumo wa uongozi ndani ya taasisi anayoiongoza.. Walau angemwachia msemaji wa taasisi amjibu Mange kama kungekuwa na ulazima wa kufanya hivyo... Mgawanyo wa madaraka una maana kubwa sana.... Sasa hivi Mange akipatwa na baya kiongozi atashangilia unabii ila kutakuwa na ukakasi mwingi kwenye jamii.....

Press conference ya kupitisha hukumu ya kifo cha Mange imezua balaa kubwa... Mange hana dogo na hana cha kupoteza ila ana wafuasi wengi na wanaojua mengi pengine kuliko hata kiongozi husika.. Mange akalianzisha kwenye mtandao wake wa Instagram... Halafu wafuasi wake wakaanza kufunguka siri za kiongozi wa dini, kuanzia ulawiti, uasherati mpaka mambo ya aibu kabisa kama ya kufanya ngono kwenye gari na ofisini, kuhonga na kutembea na wake za watu... Watu wanatiririka hasa.. Huku ni zaidi ya kuvuliwa nguo...
Pengine kati ya hizo inawezekana nyingine ni tuhuma tu zisizo na chembe ya ukweli.. Lakini tayari kiongozi keshachafuliwa vibaya... Anadhalilika yeye familia na taasisi anayoiongoza... Tuhuma ni nyingi mno... Kila jambo hutokea kwa sababu... Je hili limetokea ili kiongozi wa dini mabaya yake yadhihirike?
Vyovyote iwavyo kuilinda taasisi, kuilinda familia na wanajamii wake.. Na kulinda heshima kidogo aliyobakiwa nayo.... ASHAURIWE KUPUMZIKA.....
 
Kuna mtu kampenyezea Mange upupu mwingine wa Shekhe afu anamwambia Mange arelax mtu mchafu yule dua yake haivuki ata nguzo ya umeme kwenda mbinguni [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ndugu yangu Mshahana Jr, hao wanatoa hukumu kwa watuhumiwa wenyewe ni watuhumiwa, hivyo hawana hiyo credibility ya kuwahukumu hao watahumiwa na ndio maana wale mafarisayo sijui walipompeleka yule mwanamke aliyetuhumiwa kwa uzinzi walipoambiwa na Yesu yeye aliyemsafi awe wa kwanza kutupa jiwe kila mtu aliingia mtini.

Kwa zana ya sahihi hivyi twende kwa ushahidi, kama jaji mkuu alikuwa hajalizika na hukumu, alikuwa na uwezo wa kukata rufaa, sasa kwa kuwafukuza kazi maana tayari wameshahukuniwa hapo mahakama imewakuta hawana hatia, hao watu wanatakiwa wanakate, rufaa.
 
Hahaha ingekuwa rahisi hiv
Nimesoma post nyingi inasikitisha sana, inaonesha hakuna muislama aliechangia au waislam hawajitambui, sidhani matusi haya yangeenda kwa Pengo, Gwajima nk kama watu wangemuunga mkono Mange kiasi hiki. Kiongozi wa waislam kutukanwa na muislam akaunga mkono hoja labda awe amebatizwa
read btn the lines mjomba, usipende kulinganisha mambo. Kwanza angalia chanzo then zama deep ujue nani mkosaji nani yupp sahii, kwa maoni yangu Sheikh alitakiwa akae kimya. Sasa ameuwasha Moto WA mafuta ya taa
 
Back
Top Bottom