DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Boonge la ushahidi... Mange akipatwa na baya
Sasa hapo ushahidi ukwapi sentence Ina loop za kutosha hapo ..unajua Sheria?? Technicalities ñyingi hapo za kuondoa hiyo sentence huko ukofikiria itaweza kufaaa. kila MTU abaki sehemu yake.. Naheshimu sana tunguli zako.. Tawire.
 
Hv ikisomwa inavuka bahari????
Itapanda bombardier mpaka Nairobi, then mpaka Dubai, pale itasubiri kidogo kubadilisha ndege kama masaa manne then mpaka Los Angeles, sema sasa hapo itavuka bahari nyingi. Kuna India, Red Sea, Antlantic na Pacific kama sikosei, na maziwa hahahaha Huyu mbakwata Ana masikhara Sana, G.W. Bush alivyokuwa anachukiwa si kitambo wangemuondoa dunian kwa njia Yao ya jadi.


Pathetic!!!;;
 
Hatari Tupu mimi sihukumu kwa kweli dunia hii
Mungu tunusuru
 
Hicho anachokieleza kwamba Mange "ataondoka" ni kuwazia mambo yasiyowezekana! Katika nyakati zetu ni lazima kuacha kutumia matisho kama zamani kwamba ukimfanya hivi dhidi ya dini utadhurika. Kama anamaanisha kuwa Yeye Sheikh na viongozi wenzie watamuomba Mungu ili "amupumzishe" Kimange hilo ni jambo ambalo Mungu hawezi kufanya kabisa! Labda kama kuna Mungu tofauti na tunayemjua wengine. Ningeelewa zaidi ikiwa angemuombea Mange maisha marefu na kujaliwa moyo Wa kutambua makosa yake na kutubu.
Na statement za namna hii ya shekhe ndo zinafanya dini flani inadhihakiwa ovyo au wengine wanaiita dini ya kichawi (rejea aliyopata kunena Mtemi Deo Kisandu). Kwa mintaragu hii Waislam wanatakiwa kulikataa hafharani jambo alilosema shekhe na wabainishe kwamba dini ya kiislam haina maslahi na tishio la shekhe na kwamba hayo ni manung'uniko yake binafsi.

Kama kweli Mange alitakiwa kujibiwa kwa kutukana "uislam" basi majibu hayakutakiwa kutolewa na mtuhumiwa, angetafutwa kiongozi mwingine ndo alaani matusi ya Mange kwa niaba ya dini. Anapojitokeza yeye umma unaona kama kajitokeza kujitetea kwa uovu wake.

"Ewe Mwenyezi Mungu (Subhana Wataala) jalia aliyonenewa Mangekimambj yasimtokee, la sivyo umma utaibebesha taswira ya kimaangamizi dini yako ya hakhi na wote waiaminio"
 
Ndugu yangu Mshahana Jr, hao wanatoa hukumu kwa watuhumiwa wenyewe ni watuhumiwa, hivyo hawana hiyo credibility ya kuwahukumu hao watahumiwa na ndio maana wale mafarisayo sijui walipompeleka yule mwanamke aliyetuhumiwa kwa uzinzi walipoambiwa na Yesu yeye aliyemsafi awe wa kwanza kutupa jiwe kila mtu aliingia mtini.

Kwa zana ya sahihi hivyi twende kwa ushahidi, kama jaji mkuu alikuwa hajalizika na hukumu, alikuwa na uwezo wa kukata rufaa, sasa kwa kuwafukuza kazi maana tayari wameshahukuniwa hapo mahakama imewakuta hawana hatia, hao watu wanatakiwa wanakate, rufaa.
Hahaha mbona tusio na ajira tupo wengi na tunazo qualifications za kujaza nafasi zao. Waje huku wote tukae benchi. Mtoa haki ukituhumiwa hata sio vizuri, acha nasisi tukajaze hizo nafasi wajifunze kwetu, next time wasirudie michezo michafu.
 
Na yeye angevunga tu , hapo sasa ndio ataharibu, bora atumie muda huo kupiga dua ya kuliombea taifa. Dhidi ya watu wasio litakia mema taifa hili


Huwa namwona huyu Sheikh ni mtulivu na hana makuu na watu wa imani zote na itikadi zote, rika zote na jinsia zote, si jambo zuri kabisa kumchafua kiongozi huyu. Mungu akuondolee maumivu uliyopata, tunakufahamu wewe si mtu wa namna uliyosemewa.
 
Huwa namwona huyu Sheikh ni mtulivu na hana makuu na watu wa imani zote na itikadi zote, rika zote na jinsia zote, si jambo zuri kabisa kumchafua kiongozi huyu. Mungu akuondolee maumivu uliyopata, tunakufahamu wewe si mtu wa namna uliyosemewa.
WACHA BWANAAAA,EHEEEEE ENDELEA NA HADITHI YAKO
 
Zingekuwa na nguvu wangedhurika wanajeshi wa marekani au waisrael kwa dhuluma wanazotenda middle east na Afghanistan,
Mbona hutaji Boko haram, Al kaida na al shabab hao wanayofanya ni halali? Je Yemen wanauawa na nani kama siyo waislam wenzao wa Saudia? Je, Taliban wanaowaua ndugu zao ni wamarekani? Albadili ya shekh amesema itatupata hata sisi member wa JF. Yeye ameingiaje kama siyo member basi na yeye tutakufa naye.
 
Nadhani huyu mange atafwariki ulimwengu very very soon, na akifyarikyi basi itakuwa mbegu ya shetani imekufa kabisa kabisa, maana kuna watu walijidai wao ni CCM na wao ni nchi ila leo hii tunashuhudia hawapo kabisa na kila mtanzania anajivunia kuwa mwana CCM.
Imposibo, pamoja na kwamba inawezekana leoleo karogwa sana
 
Na yeye angevunga tu , hapo sasa ndio ataharibu, bora atumie muda huo kupiga dua ya kuliombea taifa. Dhidi ya watu wasio litakia mema taifa hili
You are right. Ila nchi hii imeombewa sana lakini tunaendelea kurudi nyuma hatua mia moja........Tuangalie hao waombeaji wanaweza kuwa ndio tatizo. Huyu sheikh naona ana mambo yake mengi sana hayaeleweki....uchafu uchafu tu.
 
Inasikitisha sana, huyu dada ni kazi ndogo sana kumrekebisha, hao anaowaumiza kwa matusi ambao wana uwezo, si wanfanye mpango wawalipe wamexican ama gege la BROTHERS nao watamshughulikia vizuri sana.

America kila kitu kinawezekana.
Anatakiwa aendelee kuwepo
 
Labda huyu (sheikh) hatamwona bidada (mange) akitukuna. Waliomsema na kumbeza ENL kwa ugonjwa wake wako wapi. Tusimpangie Mungu,ana mipango yake kwa kila mmoja wetu.
 
labda kama tuna imani tofauti... mungu anakupa kwa hitaji lako... hata ukitaka kuua...! au mpaka tukupe aya mkuu...! mungu sio wako pekee... ni wawote... wabaya, watakatifu... nk wanyama...
Atakaye ua kwa upanga atakufa kwa upanga
 
68917b6657e0c383f12acda7c6b2da64.jpg


Na hapa Shekh alikuwa kwenye kongamano la nin labda?...

Kwanin hamtaki kuukubali ukweli,Shekh ameambiwa ukweli yy aliwasema viongozi wenzake wa dini kuwa wasichanganye siasa na dini,ila yy anapoonekana kwenye majukwaa ya siasa anatangaza injili sio?!,
Tatizo hamuelewi nini maana ya kuchanganya dini na siasa! Hakuna sheria inayokataza viongozi wa dini kushiriki siasa! Tumeshaona hata CHADEMA kwenye mikutano yao kukiwa na viongozi wa dini!

Mbona hatuoni mkiwamwagia matusi kisa tu wapo kwenye mikutano ya CHADEMA?

Wakazi wa Temeke wanakumbuka Sheikh Omar Mtopea alikuwa ni mmoja wa wapiga kampeni wakuu wa kumnadi Mrema kwenye uchaguzi wa ubunge! Lakini kwa kuwa Sheikh Mtopea hakupeleka u-NCCR wake misikitini; aliachwa!

Zakaria Kakobe alishawahi kuzunguka huku na kule kumnadi Mrema wakati wa kampeni! Lakini kwa kuwa kampeni za Kakobe hazikuwa makanisani, hauwezi kusema alikuwa anachanganya dini na siasa!

Unless mtu alete ushahidi kwamba huyo sheikh alikuwa analeta u-CCM wake misikitini; vinginevyo kuwepo kwenye mikutano ya CCM huwezi kuita ni kuchanganya dini na siasa!

Au hata kwenye hiyo mikutano ya siasa unless awe anatumia nafasi yake kama sheikh kuwashawishi kuichagua CCM, hapo ndipo unaweza kuita kuchanganya dini na siasa!!

Rudini darasani mkajifunze tofauti kati ya kuchanganya dini na siasa na haki ya kiongozi wa dini kushiriki shughuli za kisiasa!!!
 
mjomba ukibishana na mpumbavu na wewe utakuwa hivyo hivyo sheikh angetumia busara zake kama kiongozi wa dini kuonyesha mfano kama kiongozi wa dini kwa wafuasi wake
lakini sio kwa kupovuka na vitisho
umetokea sura gani maalim?
 
huyu shehe ni kama alicheza kamari kwa kumtisha Mange kuwa atakufa asipofunga mdomo wake ili atishike asiwatukane tena viongozi na anajua Mange ni muislam angeogopa....lakini kwa bahati mbaya ni kama amechochea moto kwenye kuni Mange ndio kazidi kumporomoshea matusi....inabidi awe mpole tu kama ni vita ameshashindwa
Mi nadhani tunamlisha maneno Sheikh Alhad!

HAKUNA POPOTE ALIPOSEMA MANGE ATAKUFA! Alichosema yeye ni kwamba huu ni mwaka wa mwisho Mange Kimambi kutukana watu mitandaoni!!

Ina maana mtu hawezi kuacha kutukana watu hadi afe?!

Sisi Waafrika ni watu wa kuamini sana ushirikina na moja ya mambo ambayo tunaamini ni kitu kinaitwa kipai pai (sina hakika kama kweli ipo). Now let's assume kweli kuna watalaamu wa kupiga kipai pai! Na watu wakampiga Mange kipa pai na bila kutarajia anajishtukia anabeba mabegi hadi Dar es salaam!

Hapo hajadumbukia mdomoni mwa Kamanda Sirro?! Hiyo jeuri yake ya kutukana watu itaendelea?!

Huo ni mfano tu kwahiyo tusikimbilie kusema Sheikh Alhad kamtisha kumuua Mange wakati alichosema ni kitu tofauti kabisa!
 
Hahaha mbona tusio na ajira tupo wengi na tunazo qualifications za kujaza nafasi zao. Waje huku wote tukae benchi. Mtoa haki ukituhumiwa hata sio vizuri, acha nasisi tukajaze hizo nafasi wajifunze kwetu, next time wasirudie michezo michafu.
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Back
Top Bottom