DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

naona anatafuta huruma ya waislamu...
ati mange katukana waislamu wote
 
Mange Kimambi,naam.
Mwanamke aliyemtukuna Lowasa matusi yote ya nguoni na Chama tawala wakawa wanafurahia.
Mange Kimambi,mwanamke asiyeishiwa na vituko na hoja,matalakiwa na mama wa watoto watatu.
Sheikh,badala ya kuombea kichaa apone,umeshindana nae na sasa kichaa anamwaga yote, ya kweli na ya uongo.
Umeudhalilisha Uislamu,pima na chukua hatua!!!
Waliokuwa wakishangilia EL akitukanwa ndio haohao wanamhimiza sheikh na kumpamba ajibizane na "kichaa!!" Sheikh anaadhirika wao wako pembeni wanatazama sinema ya kutisha!!!
Sheikh amevukwa nguo ila utamu wa madaraka nao...
 
naona anatafuta huruma ya waislamu...
ati mange katukana waislamu wote
Da Mange anavyomfukunyua sasa...kila baada ya nusu saa anarusha bomu. Sheikh kaingia cha kike kumjibu chizi, bora angepiga kimya ona anavyodhalilika sasa!
 
Hapana hapa busara ni Shekh ni kuomba sluu haya mambo yaishe salama, yule dada katishiwa maisha yake ujue sasa anafanya lolote analojua ili q kweli maneno ya sheikh yakitimia na yeye kajilipizia kisasi. She has nothing to loose,
Sentence ya mwisho katika msg yako ..."she has nothing to lose" ... Hivi kweli MAISHA YAMEKOSA THAMANI KIASI HICHO? ... Are we not VALUABLE BEINGS/CREATURES before God the Almighty? ... Kwa nini maisha yetu yakose THAMANI kiasi hicho ... ?

By the way, a little correction to that grammatical error in your sentence above ... "Loose > Lose ...
 


Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.

=====

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).

Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.


Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.

Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.

Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.

Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi

Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, walijiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.

Kwa kadri ya kumbukumbu zangu , HAKUNA MTU YETOTE ALIYEJARIBU KUPAMBANA NA JF NA AKASHINDA , labda huyu Musa Salum atakuwa wa kwanza .
 
huyu shekhe wa dar anapenda kula huyu si mchezo.sijui kwake hamna chakula
 
Aliyemshauri kumjibu Mange ndio kakosea.. Pole sana kwa sheikh, ila Mange kamwambia ukweli mtupu... Mange ni mwana TANU yule, hivi mnazikumbuka ahadi kumi za mwana TANU? Basi Mange anaziishi zile ahadi zote hasa ile ahadi inayosema "8.Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko". Na kama kuna ahadi Mange imemshida kidogo ni moja tu ile ya mwisho... "10. Nitakuwa mtii kwa Raisi na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania". hiyo tu...
Mkuu,nimecheka mpaka mbavu zimeniuma!
 
Nadhani hakutakiwa kutoa tamko kama alilotoa hadharani..Tatizo alikuja kwa pupa mno..Alitakiwa kuwauliza hao wapambe wa chama kabla ya kutoa tamko la ku mu attack mrembo wa kule Amerika

Alitakiwa kumuuliza RC nini kilimkuta alipo jaribu kupambana na yule dada

Halafu angekuja kwa super brand a.k.a the nation pia angemuuliza pia..

Sasa kwa kashfa hizi zote sidhani kama waumuni watamuelewa..Ni vema akajivua gamba tuu..

Tatizo hachelewi kutuwekea video za dhambi alizokuwa anafanya…

Yule mrembo wa kule Amerika anaita kitu cha “HIROSHIMA”
 
Back
Top Bottom