DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria



Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.

=====

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).

Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.


Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.

Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.

Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.

Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi

Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, walijiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.

Mkwara mbuzi huuuu! Huyu sheikhe ni punguani.chizi huyu. Kwani wewe ni mungu mkuu
 
Hicho anachokieleza kwamba Mange "ataondoka" ni kuwazia mambo yasiyowezekana! Katika nyakati zetu ni lazima kuacha kutumia matisho kama zamani kwamba ukimfanya hivi dhidi ya dini utadhurika. Kama anamaanisha kuwa Yeye Sheikh na viongozi wenzie watamuomba Mungu ili "amupumzishe" Kimange hilo ni jambo ambalo Mungu hawezi kufanya kabisa! Labda kama kuna Mungu tofauti na tunayemjua wengine. Ningeelewa zaidi ikiwa angemuombea Mange maisha marefu na kujaliwa moyo Wa kutambua makosa yake na kutubu.
Ni kweli mkuu najiulizaga sana hawa watu wanamtumia Mungu yupi hasa ambae wanakua na majibu tayari kwa kile ambacho Mungu huyo anaenda kufanya kiasi cha kukaa na kutangaza
 
shekhe kadondoshwa chini kwenye kila round za pambano mbaya zaidi final round ya 12 kapigwa technical knockout kalala mazima bila kuamka....hakika chizi fresh amebaki kuwa unbeaten mpaka sasa
 
Ushabiki wa kisiasa bado haujafikia na haupaswi kufikia hatua hiyo ya kuwatusi wanadamu wenzio ...
Ushabiki wa kisiasa kwa awamu hii ya 5 ni vita ya kweli. Silaha zote zinatumika kuumaliza upinzani. Hao wanaotumia matusi ni kwavile hawana uwezo wa kupata hizo silaha nyengine tu.
 
Nimecheka sana! Unajua bhana kipindi kile tukuwa bado wadogo na atukutembea kwenda nje ya nchi tuliamini sana na tulimezeshwa ujinga sana na watu wa madrassa kuhusu albadili sasa tumetoka na tumejua kwamba ni ujinga wa ovyo kabisa
 
Nimecheka sana! Unajua bhana kipindi kile tukuwa bado wadogo na atukutembea kwenda nje ya nchi tuliamini sana na tulimezeshwa ujinga sana na watu wa madrassa kuhusu albadili sasa tumetoka na tumejua kwamba ni ujinga wa ovyo kabisa
hujakutana na chuma wewe..ingia 18 za watu upigwe..ndo utaijua dunia
 
hujakutana na chuma wewe..ingia 18 za watu upigwe..ndo utaijua dunia
Huo ni uchawi wa kwababu na sio albadili ile wanao soma mashekhe ubwabwa wale wa madrassa siamini na sitoamini kwamba albadili inaweza ikamdhuru mtu maana mungu wakweli apendi mtu alibikiwe mpaka akapoteza akili yake kama akipoteza akili nani atamsujudia .ukitembea ukitoka hapo kwenu bongo ndio utaamini aya maneno yangu
 
Ukitaka kujua ugumu wa dini ni hapo, namna ya kumtreat mbaya wako. Hii ya kumwombea mbaya wako mabaya haina cha padre wala sheikh. Binadamu yeyote timamu anamwombea mbaya wake mabaya. Mnaoenda kanisani msidanganyike na mahubiri ya wachungaji wenu madhabahuni au mashehe kwamba eti mbaya wako mwonbee mazuri hiyo haipo. Hao viongozi wa dini wanakesha kuwaombea wabaya wao mabaya. Bahati nzuri tu Mungu hana akili za kibinadamu.
Mkuu unachoongea umegeneralize sana,sijui kama unajua communication skills,sisi wengine tumeokoka tunaomba ushahidi wa wachungaji wetu inaonekana unawajua sana.Hapo nilipo highlight red,kwa jinsi unavyo andika unapotosha watu,kama kuna mchungaji amekosea au padre au sheikh deal naye personally usijumuishe na wengine.Tia ushaidi kwamba wachungaji wetu wanakesha wanawaombea watu mabaya.Biblia imetuagiza kuwapenda adui zetu sasa kama wewe umeshindwa kumpenda adui yako hiyo haibadilishi ambacho Mungu anataka tufanye.Nasubilia ushahidi wako au hao unaowajua wataje majina yako kuliko kujumuisha wote,that is very bad and shows lack of skills in public speaking.
 
Lusekelo alitoa matamko kwa waandishi wa habari kuwa watakufa ila hadi leo hakuna aliyekufa mbaya sana naye mwenyewe hajaenda kuuza gongo kama alivyoahidi.

Shekhe naye kaingia mkenge ule ule wa Mzee shekhe Yahya,.

Yaani, daima siasa uchwara mbuzi zitakutokea puani tu ukijiingiza bila kufata principles.

Tunasubiria mwisho wa Mange kimambi ndani ya hii 2018.
Ila akivuka hadi 2019 sijui majibu yake kwa shekhe yatakuwa ni nini hasa!? Shekhe ajiandae kupata aibu za daima pale Miss. Kimambi atakapo toboa hadi 2019

Any way, Shekhe na hadhi yake kwa dini na hapo nchini siyo mtu wa kujibizana na Mangi Kimambi.
Nisingeona comment yako ningejitoa jf ni mchangiaji mzuri sana Mkuu mchana mwema
 
Ushawahi muuliza kakobe kwanini anaona mapungufu ya SERIKALI tu na sio upinzani?

Kwa sababu Tamko la Rais linatuathiri wote watanzania, kinyume na tamko la Mbowe au Maalim wa CUF. Sina haja ya kukujibu mengi utafunuka tu.

Na huyu sheikh wako, mwambie afunge mdomo kabisa, kwa maana tumemuhifadhi tu vinginevyo kwa madhambi anayofanya ni sawa na kusema yupo uchi. Hatutaki kumvua nguo hapa hadharani, lakini akipanua mdomo tutaanika uchafu wake woteeeeeeee. Maana kama asipoenda motoni huyu sheikh basi hakuna wa kwenda motoni.

Nasikitika hakusikiliza ushauri nasaha wa watu wenye busara waliomshauri " ASIMJIBU MANGE" na yeye hakusikia. Kifupi hakumjibu MANGE ila aliwajibu waislamu wote waungwana walioamua kukaa kimya na kumdharau kwa maovu yote anayoyafanya. Sasa kachokoza waislam wote, eti Mange katukana waislamu wote- Hapana, waliotukanwa ni wale wanaoutusi na kuudhihaki uislam huku wenyewe wakijiita waislam kwa kutumia kivuli cha BAKWATA. Mwaga ugali nasi tumwage mboga!!!!!!!! Mange tulia huyu tuachie sisi.
 
Hata BAKWATA wenzake hawampendi ndio maana wakamshauri amjibu mange ili mambo yote yawe hadharani.
 
Back
Top Bottom