Nimeguswa na ukatili dhidi ya Binadamu wengine kwa mgongo wa Dini.
Talebani wamechukua nchi ya Afghanistan Juzi, raia wengi wanataka kuikimbia nchi kwa kuhofia ukatili wa Dini.
Hakuna Aya lakini
Wezi wanakatwa mikono.
Wazinzi wanapigwa mawe hadi kufa au kuuliwa kwa kuchinjwa.
Wanawake wanazuiliwa kufanya baadhi ya kazi.
Mnafanya hivyo bila ruhusa ya kitabu chenu Qurani.
Mi ninavyo fahamu Dhambi ni kumkosea Mungu na yeye ndiye atakemwashibu mdhambi.
Makosa ya kijamii yanahukumiwana sheria za kijamii.
Halafu mnaiita Dini ya Amani.
Kumbe bado hata hunielewi !!!---- nikuulize swali je hao Talibans ni Qur'an ??, vipi wale crusaders walioua watu kinyama kwa mgongo wa ukristo katika karne ya 12, 13 walikuwa wa wanawakilisha Ukristo ??.--- au yule mchungaji aliyekuwa akiwanyoa akina mama mavu★★ madhahabuni je huyo anawakilisha Ukristo???--- hebu utuambie kama anawakilisha na utoe andiko, au wale mashoga wanaotetea ushoga wao kwa kumnukuu Yesu, je ni sahihi kusema kwamba wao wanamfuata yesu haswaaa!!??
Narudia kusema tofautisha kati ya Mafundisho ya dini na Wafuasi wa dini, mafundisho ya dini yatabaki kuwa yalivyo yasipotiwa mkono lakini wafuasi wapo wa aina tofauti na kila mmoja anaweza kudai kwamba yeye ndiye anaelewa mafundisho vizuri na akatenda anachoamini.
Lete andiko la Qur'an ili tulijadili na sio matendo ya Talibans, Isis, Alshabab nk.
Umezungumzia juu ya adhabu zilizoainishwa ndani ya Qur'an, katika Qur'an kuna makosa yenye adhabu hapa duniani na huko akhera mtu ataadhibiwa kama hatotubia kwa Mungu hapa duniani, Mfano mtu akizini na ikathibitika na mashahidi 4 wakatoa ushahidi kwamba wamemuona/wamewaona Wakizini basi kwa mujibu wa Qur'an watu hao ni lazima wachapwe mijeledi mia kila mmoja, ipo hivi; kama watu wanne wameshuhudia kwamba wamewaona hao wazinzi wakizini maana yake bila shaka hao watakuwa WALIZINI HADHARANI, kitendo ambacho hata sheria za kidunia zinatambua ni kosa kuzini hadharani au hata mke na mume kufanya ngono hadharani ni kosa kwa sheria za duniani sembuse sheria za dini !!!? --- ili kulinda heshima ya jamii ni lazima watu hao wapigwe viboko 100 hadharani ili jamii pia ijifunze kwamba kuzini ni kosa mbele ya Mungu bali kuzini hadharani ni kosa kwa jamii pia. Hapo sasa utaona makosa yanayoathiri/gusa jamii ndiyo yaliyopewa adhabu za hapa duniani mfano mwingine ni Kosa la wizi ambalo adhabu yake ni kukatwa mkono, (hapa kukatwa mkono inayo maana pana mbali na maana ya moja kwa moja ya kukata mkono), kosa jingine lenye adhabu ni kuua kwani nalo linahusu jamii, kosa kubwa kabisa mbele ya Mungu ni Shirk, lakini huwezi ona kosa hilo limepewa adhabu kwani ni kosa moja kwa moja kati ya mtu na Mungu na jamii haihusiki.
Mtukufu mtume (saw) katuasa; Kutafuta elimu ni faradhi kwa Muisilamu mwanamume na muisilamu mwanamke, kama Talibans wanawazuia Wanawake kusoma watakuwa wanaenda kinyume na Mafundisho ya mtume (saw), yawezekana wao wanao Uisilamu wao.
Kifupi ni kwamba lete aya ya Qur'an tujadili na usilete Watu tuwajadili.