Huyo kigogo aliwahi kugombea urais akafika hatua ya mtu Tano! Aliwahi kuwa waziri ofisi ya boss wake wa Sasa. Akishirikiana na walowahi kugombea nafasi Ile na Bado wanaitamani Wana mpango wa muda mrefu na mfupi wa kunyong'onyeza aliyepo Kwa kufungulia matukio ya hapa na pale ili Madame skate tamaa na kuiona nafasi Ile ni ngumu!Kigogo kasema Pambalu na timu yake hao chadema ndo wanachoma. Nenda Twitter.
Walianza na ugaidi uchwara, ikafuata filamu ya kuchoma masokona mashule, na machinga kuvurushwa, ikaja ya mauaji ya jumla na rejareja na Sasa wamerudi kwenye moto kwenye masoko!
Lengo la mapichapicha haya ni kumvuruga Madame na kuhamisha kifikra hasa pale anapotaka kuwafukuza kazi! Wanajulikana wenye kazi hii na wamekalia ofisi nyeti za umma!
Nimpe ushauri wa Bure bi mkubwa kuwa, kikulacho ki maungoni mwako! Kaa mbali ni mkulugwa anayewalazimisha watu wahamie Burundi na huyo mtoto wa mzee wa ubatizo wa moto! Wanakuchezesha kistela wowowo bila wewe kung'amua! Ccm acheni kuwatia wananchi umaskini Kwa kuwachomea bidhaa zao, msiwasingizie cdm!