Chama chochote cha siasa kikishindwa mara nyingi hugeuka kutoka chama cha siasa na kua kikundi cha uasi.
Dalili kubwa za kundi na uasi ni kuanza kudai uhuru ambao tayari inchi inao.
Wakati mwingine kundi la waasi huona serikali iliyopo si halali kuongoza nchi.
Serikali iliyopo inatakiwa kufuatilia kwa ukaribu kabisa nyendo za watu hao kwa sababu nia na malengo yao ni kuhatarisha usalama wa nchi.
Asili ya Chadema ingekuwa Mara labda wangejaribu, ila wengine ni pesa tu...piga sana ruzuku...matozo ya kijinga kwa wabunge wa chama hicho...ila kusema hata waanzishe kitengo cha inteljensia ya chama wameshindwa hadi wanadakwa na Muroto kama panzi!
Wewe ni kiazi. Nini cha maana tu aweza kujifunza kwenye nchi zenye tabia hizo za kishenzi hadi tuzifanye rejea? Rais ni binadamu na raia sawa na wengine.
Nchi si mali ya Chama, familia au ukoo. Nchi inaongozwa kwa Sheria, yeyote anayekosea apelekwe mahakamaani na kushitakiwa kwa haki, siyo ashughulikiwe kwa hisia tuu. Hatuwezi kuendesha nchi km familia, baba anataka, baba anasema, nchi haiendi hivo!!
Sent from my SM-J530F using
JamiiForums mobile app
Maandamano & Sheria Husika
Sheria ya Jeshi la Polisi ya mwaka 1961 na marekebisho yake ya mwaka 1995, ambayo ndiyo huelekeza na kuongoza kuhusu njia na namna ya kuendesha maandamano nchini, inasema:
(1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara, kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:
(a) Sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) Dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) Maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye Gazeti la Serikali.
(2) Pale ambapo mtu amewasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda, au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa pale atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo husika ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa.
(3) Afisa polisi ambaye taarifa imewasilishwa kwake kulingana na kifungu kidogo cha (1), hatatoa amri ya kusitisha chini ya kifungu kidogo cha (2) kulingana na taarifa husika, isipokuwa ameridhika kwamba kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kuna uwezekano wa kusababisha kuvunjika kwa amani au kuathiri usalama wa taifa au kudumisha amri kwa umma au kutumika kwa dhumuni lolote lisilokuwa halali.
Hii ndiyo sheria inayoongoza Jeshi la Polisi kwa maana rahisi maandamano ni mpaka pale jeshi la polisi limekubali na kutoa kibali baada ya waandamanaji kuomba kibali hicho.
Vyovyote vile, kuhusu maandamano hayo, jeshi la polisi linapaswa lijiridhishe pasipo shaka kuwa hayahatarishi maisha au kuleta madhara yoyote na hayataingilia haki za watu wengine ambao hawataki kuandamana.
NINI KINACHOWEZA KUTOKEA?
Kinachoweza kutokea baada ya katazo la jeshi la polisi, ni kujitokeza kwa watu wenye nia ya kutaka kuandamana kwa nguvu. Ukifanya hivyo moja kwa moja utakuwa unatenda kosa la UHAINI ambalo ndilo kosa kubwa kuliko yote nchini kwa mujibu wa ibara ya 28 ya Katiba yetu.
Sheria inasema kwamba kama ukifanya yafuatayo utakuwa umefanya uhaini katika Jamhuri ya Muungano:
(a) Kifungu cha 39 (1) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote akajaribu kumuua Rais, atakuwa ametenda uhaini.
(b) Mtu yeyote aliye ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote akaanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano atakuwa naye ametenda kosa la uhaini.
(c) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri, kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, au kufungwa kwa Rais atakuwa ametenda uhaini.
(d) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondoa Rais madarakani visivyo halali atakuwa ametenda kosa la uhaini.
(e) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi mkuu wa serikali atakuwa ametenda kosa la uhaini.
(f) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kupindua serikali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama atakuwa ametenda kosa la uhaini.
ADHABU
Kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini, adhabu yake ni kifo; na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.
Hivyo, Watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuzijua sheria za nchi yetu ili kuweza kujiepusha kutenda makosa ya jinai dhidi ya nchi yetu.