Mkuu tumia akili yako ya kuzaliwa japo hata kidogo......hivi umewahi kufika Lagos mkuu? Pale katikati ya jiji kuna nyumba za hajabu yaani Tandale kwa kina Diamond afadhali, halafu sasa huo uchafu ndio usiseme. Yaani fananisha mjini hapa Bongo (stesheni) kuwe na jalala la hajabu na harufu isiyo na mfano na nyumba kibao za udongo na zenye mabati ya kutu zimezagaa kila kona katikati ya jiji, umeipata hiyo picha? Je, Bongo iko hivi? Kwa hapa Afrika mashariki slums kama hizi zipo pale Nairobi (Kibera) tu.
Mkuu wakati nakujibu reply yako nimekupa mfano mdogo tu wa kueleweka kulingana na muktadha wa comparison yako kati ya moshi Detroit, lakini naona kabisa wewe ndio umetumia akili za usingizini na hata kushindwa kung'amua nilichokimaanisha.
Na hiii comment yako bado ni mwendelezo wa kile kile nilichokujibu awali, naona hata haujui ubora/advancement ya majiji unalinganshwa kwa kuzingatia vigezo gani, umekomaaa tu "slums" "slums".... Kama ndio hicho ndio kigezo chako basi Detroit ni mji mchafu sana unazindiwa mbali sana mkoa wa Moshi uliopo Tanzania kwa usafi. Kwa mantiki hiyo basi kwa mujibu wa vigezo vyako Moshi ni zaidi ya Detroit, yaani Moshi pameendelea sana kuliko Detroit huko nchini Marekani. Kitu ambacho kwa ni illogical fallacy kwa mtu yeyote aliye timamu.
Unapolinganisha ubora wa majiji angalia anza na vitu kama uzalishaji,miundo mbinu,huduma za kijamii,idadi ya watu na uchumi kwa ujumla.
Sasa labda nikuulize tofauti na usafi.
Je, Dar inaifikia hata nusu GDP ya Lagos?
Je,Dar ina viwanda sawa na Lagos?
Je,Miundo mbinu iliyopo Lagos unaweza ukalinganisha na Dar?
Je,unajua population ya Lagos ni na sawa na ya mikoa mingapi ya Tanzania kwa ujumla?
Je, kwenye entertainment,elimu,vituo vya kazi utailinganisha Dar na Lagos?
Hivi kwanza unajua " slums" zinasababishwa na nini?