Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

Aibuuuyamwakaaaa loooh
 
..wazazi wenye watoto wa kiume wanaokaribiana kiumri nadhani watanielewa.

..wakati mwingine dawa ya kukomesha mizozo na magomvi kati ya watoto wa kiume ni kuwaacha wapigane mpaka wachoke na kuishiwa nguvu.

..baada ya hapo utaona hawazozani na kugombana kwani wanajua hakuna wa kuwaamua kama ilivyokuwa zamani. Kila mmoja atakuwa anakumbuka kichapo alichopokea toka kwa nduguye.

..sasa nirudi kwa waheshimiwa sana MADIWANI WA JIJI.LA DSM. Nadhani Polisi wameingilia kuamua ugomvi wa madiwani zaidi ya mara mbili.

..Mimi nashauri siku nyingine Polisi wasitokee kabisa kama watapata taarifa za vurugu ktk mkutano wa madiwani.

..Madiwani waachwe watwangane, watoane meno, wavunjane miguu, wavuane nguo...Shauri yao! Hawa ni watu wazima lakini wana-behave kama wahuni au vibaka.

..Hebu fikiria baada ya UPUMBAVU ule huenda MADIWANI walilipana POSHO ya kikao.

NB.

..Suala la kumuwajibisha Meya wa jiji la Dsm halikupaswa kupelekwa kwa misingi ya vyama.

..Ilipaswa madiwani wa chama tawala na wapinzani wachukue uamuzi wa pamoja, kumuadhibu, au kutomuadhibu, mstahiki meya.
 
Umeongea vema. Kuna kundi moja linajiona Lina haki ya kufanya uhuni wowote kwani wanajua kuna watu wako nyuma yao kutoa msaada

Utasikia wanakimbilia kusema "askari mko wapi? Toa nje huyo, kamata peleka sijui wapi huko

Siku moja askari waseme tu , malizaneni wenyewe bana nyie si watu wazima?

Nyie si waheshimiwa kabisa? Nyote si mmechaguliwa na wananchi? Nyote si mnaakili timamu? Si hakuna aliyeingia na kilevi humo?

Basi malizaneni ki utu uzima!

Halafu wakae pembeni watizame movi. Atakayezidiwa apewe msaada wa kupelekwa hospital tu au huduma ya kwanza

Halafu waandishi wa habari wanakaa angle nzuri kuchukua matukio ki uhakika na weledi kutuhabarisha na kutunza kumbukumbu

Na mwisho kabisa najiuliza, hivi hakuna vitu vingine vya kujadiliwa na madiwani zaidi ya kumg'oa meya!?

Dar es Salaam wanafunzi wote wanakaa kwenye madarasa na madawati bora?

Kuna baadhi ya watanzania wanaaibisha ubinadamu wa mwadamu mwenye akili timamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ya msingi ya Polisi ni"KULINDA MAISHA YA WATU NA MALI ZAO"
Hivyo uwepo wa Polisi mahali pale ndio kazini kwao,wala sio kuingilia Kikao cha Madiwani.
Vivyo hivyo,Uwepo wa Polisi kwenye mikusanyiko mbali mbali utaendelea kuwapo na kuhitajika kwa manufaa ya Wananchi na wote.
Kamanda SIRO na Askari wako ninawapongeza sana kwa kudumisha AMANI nchini.Ongezeni ushirikiano na Wananchi,MNAKUBALIKA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni pamoja na kushiriki kumuua Akwilina au?
 
Mkuu mkurugenzi na wajumbe wa ccm walijua wanataka kufanya nini,ile forgery ya Jina haikuwa bahari mbaya but something planned so police waliwekwa standby incase
 
Watu wanahangaika kumng'oa meya badala kushughulika na tatizo la ajira.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupigana tu ni kosa kisheria, hivyo polisi hawezi kuacha mpigane!
Kama ngumi mnaziweza watafuteni huko mtaani ambapo polisi ni ngumu kufika
#keyboard warriors#

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha ile imetupa picha moja kubwa muhimu.BARAZA LA MADIWANI inapofika hatua ya kupigania maslahi ya vikundi au vyama (sio wananchi), hugeuka na kuwa GENGE LA WAHUNI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona watu wazima wanatwangana waacheni wameshiba ugali wataacha wenyewe,polisi walifanya makosa Sana kuwaamulia
 
Watu wanahangaika kumng'oa meya badala kushughulika na tatizo la ajira.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia wameshau madarasa na walimu wao wana kazana kumngoa Meya ili wapige 5b ambayo Meya amezuia isitumike kwa njia za wizi.. Yaani ukiona Maccm qamekomaa mahali jua kuna ulaji wanao shindwa kuiba kwa kuzuiliwa na wapenda nchi yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 



Ila huyo mkurugenzi anawadhalilisha ccm.
 
Huo mda Wa kujadili kumng'oa meya wangeutumia kutatua kero za uchafu katika jiji ingesaidia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…