Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

Mkuu Heri ya mwaka mpya ikufikie huko uliko
Asante ndugu yangu, na wewe Heri ya mwaka mpya huko uliko. Niliamini kimakosa kwamba tungeuanza mwaka mpya kwa Uongozi wa Tanzania kuacha ushamba na ulimbukeni...nilikuwa naota tu, kaniki asili yake!
 
Hii ni hatari kwa viongozi wote wa kuteuliwa mkoani Dar kuwa mabingwa wa kufoji...mara huyu kafoji vyeti, mwingine kafoji majina lakini cha ajabu wanadunda tu. Viongozi wanaochaguliwa na wananchi msikubali katu kila siku kudhalilishwa na na hawa washamba na limbukeni. Amkeni wakazi wa Dar, hali kama hii hamwezi kuiruhusu iendelee. Kuna siku mtaamka mtakuta wamefoji hadi haki zenu na usalama wenu…ebo!
Mbona wewe hujaamuka?
 
Jina sahihi la kuwaita CCM ni WAHUNI.
Hiki chama kinafanya mambo ya kihuni bila hata aibu hasa siku hizi. Wakati wa JK vitendo vya ulaghai vilikuwepo lakini ilikuwa kwa staha na akili kubwa sio KISHAMBA namna hii.
Nadhani mzee Kinana na vijana wake walikuwa sahihi kwenye Yale mazungumzo yaliyo dukuliwa.
 
Kikongwe tu haitoshi umesahau UTAJILI ,lakini pia ukumbuke ukiwa kikongwe basi unakua huna NGUVU .
Lakini ni mambo ya aibu sana. Inatutia doa sana kimataifa.. Huwezi kuamini mambo kama haya yana fanywa na Chama. Kikongwe Afrika.. Yaani nimeangalia ile video nilitamani kulia.. Ccm wana fanya mambo ya aibu.. Hawajui uongozi ni dhamana.. Halafu watatuambia tulinde amani.. Ipi???? Wakati wao ndio wavunjifu wa amani?? Halafu huu upuuzi unafanywa na watendaji wale wale wa TAMISEMI ambao wako ofisi ya rais.. Jamaniii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefurahishwa sana na njia aliyo onyesha Meya Jacob katika kikao cha Halmashauri ya Jiji la Dar kilicho kuwa kimepangwa ili "kumkomesha" Meya wa Jiji Isaya Mwita baada ya kukataa kuwa na bei ya kuunga mkono juhudi.

Akidi haikutimia kwa wajumbe wa CCM hivyo wakaamuwa kufoji jina la Diwani ambaye hayupo na kusaini.

Jacob akashtukia mchezo na kuchukua attendance register ili kuonyesha ulimwengu hila za CCM katika vikao halali unaofanywa na Mkurugenzi kushirikiana na madiwani na Wabunge wa CCM akiwemo na Mheshimiwa Zungu ambaye ni mwenyekiti wa Bunge asiyepaswa kabisa kushiriki tabia kama hizo.

Walipotaka kumdhibiti kwa kutumia polisi Boniphace alijipanga tayari kutembeza MKONO NA KUNG FU kiasi waka gwaya kumkabili.

Kinachoundwa ni kuhakikisha Meya anakuwa wa CCM kwa gharama yeyote na bila aibu.

Mtindo aliotumia Boniphace ni wakuiga maana CCM hawana aibu hivyo kuna wakati ikibidi kuwapa kichapo ni sawa tu.

Ama kweli 2020 ni #NoHateNoFear
Ndungulile na Musa Zungu mmejidhalilisha kuliko maelezo
 
Kusema ukweli CCM kama chama kikongwe na tawala chenye kushika dola kinatia aibu sana na kuleta fedheha ktk masuala ya uchaguzi. Tuhuma zenyewe ni ubabaishaji mtupu, tume ilikuwa inaendesha huo uchunguzi ni "zero brains" tupu na hata huo mchakato wa uchaguzi wenye kuhusisha watu 16 tu, bado wanataka kuchakachua matokeo!? Ama kwa hakika CCM hii upuuzi wowote ule ktk masuala ya uchaguzi unaweza kutokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aibu ona wewe, wazee wa PhD macho makavuuu.
 
Nimefurahishwa sana na njia aliyo onyesha Meya Jacob katika kikao cha Halmashauri ya Jiji la Dar kilicho kuwa kimepangwa ili "kumkomesha" Meya wa Jiji Isaya Mwita baada ya kukataa kuwa na bei ya kuunga mkono juhudi.

Akidi haikutimia kwa wajumbe wa CCM hivyo wakaamuwa kufoji jina la Diwani ambaye hayupo na kusaini.

Jacob akashtukia mchezo na kuchukua attendance register ili kuonyesha ulimwengu hila za CCM katika vikao halali unaofanywa na Mkurugenzi kushirikiana na madiwani na Wabunge wa CCM akiwemo na Mheshimiwa Zungu ambaye ni mwenyekiti wa Bunge asiyepaswa kabisa kushiriki tabia kama hizo.

Walipotaka kumdhibiti kwa kutumia polisi Boniphace alijipanga tayari kutembeza MKONO NA KUNG FU kiasi waka gwaya kumkabili.

Kinachoundwa ni kuhakikisha Meya anakuwa wa CCM kwa gharama yeyote na bila aibu.

Mtindo aliotumia Boniphace ni wakuiga maana CCM hawana aibu hivyo kuna wakati ikibidi kuwapa kichapo ni sawa tu.

Ama kweli 2020 ni #NoHateNoFear
Mbona kwenye clip inayotembea sijawaona Polisi pale bali walinzi wa Kampuni ya Ulinzi?
 
Back
Top Bottom