Dar: Wafanyakazi wawili wa Kampuni ya Mwananchi Communication wakamatwa kwa kusambaza taarifa za uongo za Corona

Mnaingia huko kuvizia nani atasema nini,shame!
 
Naomba kuuliza inakuwaje hadi watu wanakamatwa kutokana na meseji za whatsapp? Je, mkiwa na kundi lenu la watu watano ambao mna same interest na miashare habari za zinanzosemekana kuwa ni tofauti mnaweza kukamtwa pia? Kivipi mtakamatwa au hizi whatsapp zipo monitored?
 
Niko Mbeya na hizi taarifa nilizisikia kabla sijaenda Madaba last week, niko mbey angoja nitafuatilia lakini huku mbona si taarifa ya ajabu? Hata last two weeks kulikua na taarifa ya Bas la Luwinzo kukamatwa baada ya kugundulika kuw akuna mgonjwa wa Corona alitoroka karantini akapanda hilo basi akakamatiwa makamabko? Mbona ni habari za kawaida sana? Waje Mbeya au hapa Makambako watasikia mengi sijaona tatizo.

Kama si kweli si ni suala la kutoa taarifa sahihi tu? kwanini wanajichosha wakatyi kuna watu wana kazi zao? Hizo resources za kuwakamata si tungezitumia kwa kufanya mambo mengine?
 
Hao tayari ni wahalifu, kama wameweza kuzusha hilo jambo basi wanaweza kuzusha lingine kubwa hivyo ni lazima wadhibitiwe ipasavyo.

Wenye mamlaka kama hawajasema chochote wewe hizo taarifa unathibitisha vipi?

Nakumbuka kipindi cha JK kuna dogo alisemaga mkuu wa majeshi kalishwa sumu, kapewa taarifa fake naye akakimbilia kuzisambaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Badala wapambane na korona, wanahangaika na watu!
Korona itachukua uhai wako na wapendwa wako na siyo serikali. Ukifanya uzembe, mzaha
na ujeuri, inakula kwako.

JIKINGE UMKINGE WAPENDWA WAKO.

JILINDE UMLINDE JIRANI
 
Ma group ya WhatsApp sio sehemu salama

Tuendelee kuchapa kazi tujenge Nchi yetu huku tukichukua tahadhari za kiafya

Sent using Jamii Forums mobile app
Tyliwaambia watu hapa kwamba End-To-End Encryption ya whatsapp sio guarantee ya kutoonwa jumbe za whatsapp.

Tukasema kama mwanakikundi mmoja wa whatsapp akidukuliwa na software kama PEGASUS SPYWARE basi group lote mmeisha.
 
Sawa nimekuelewa, uiku mwema
 
Wataalamu husema kati ya kundi la watatu mmoja ni nyoka ama ana mawasiliano ya moja kwa moja na nyoka, makundi ya whatsapp ni kichaka chenye nyoka wengi
 
Watsapp kuna masnich kibaoo.. watu hawaelewi tu..
 
Wats app watu wanachomwa na wenzao humo humo kwny ma grupu sishani ka TCRA wana mda wa kudukua kila mtu kila dakika....

Kuna masnitch tu ukiongea wana screen shot wanatuma kunapohusika
Y

Tyliwaambia watu hapa kwamba End-To-End Encryption ya whatsapp sio guarantee ya kutoonwa jumbe za whatsapp.
Tukasema kama mwanakikundi mmoja wa whatsapp akidukuliwa na software kama PEGASUS SPYWARE basi group lote mmeisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Influenza,
Sasa kumbe issue haihusiani na kampuni ya mwananchi maana mi nilijua wameandika kwenye gazeti !
sasa kuna haja gani ya kuhusisha ujinga wao na kampuni?
 
mara polisi anayekushtaki naye corona inamnyoosha !
hapo ndipo atajua kwa nini kunguru ni ndege ila habebi abiria ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…