Dar: Wakamatwa wakifungua vyuma vya nguzo Daraja la TANZANITE

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wawili (2) waliokuwa wanajaribu kuharibu kwa kukata baadhi ya vyuma vya ngazi moja ya nguzo namba P9 ya Daraja la Tanzanite lililopo maeneo ya Salender, Ilala.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Muliro J. Muliro amesema watuhumiwa hao ambao majina yao (yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) walikamatwa tarehe 02/04/2022 saa 10 alfajiri wakiwa wanajaribu kufungua vyuma vilivyopo kwenye nguzo ijulikanayo kama P9 ambayo ipo kwenye daraja hilo. Wanahojiwa kwa kina na watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa hatua zaidi.

Pia Jeshi la Polisi limewakamata watu wengine kumi (10) waliokutwa chini ya Daraja huku wakidai wanaokota vyuma chakavu kwa ajili ya biashara ya vyuma. Watuhumiwa hao pia wanahojiwa kwa kina ili kubaini malengo yao kwa ujumla chini ya Daraja hilo yalikuwa ni nini na kuona kama wanamahusiano na wale waliokuwa wanajaibu kuiharibu baadhi ya miundombinu ya nguzo ya daraja hilo.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kuwa halitamvumia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma, Ulinzi katika eneo hilo na maeneo mengine umeeendelea kuimarishwa na atakayejaribu kuiharibu atakamatwa na mifumo ya kisheria ya kishughulika nae itazingatiwa.

DARAJA LA TANZANITE (1).jpg
 
Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kuwa halitamvumia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma
Jeshi la Polishi halitamvumilia yeyote atakaeharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma.

Na kwa minaajili hiyo Jeshi la Polisi Kanda Maalum liko tayari kuvumilia wale wote watakaoharibu miundombinu iliyojengwa kwa manufaa binafsi.
 
Kwakua hpo ni kwenye daraja ambalo lipo dar na watu upita kwa wingi hpo ndyo maana wamejulikana, hali ni mbaya uku kwenye ujenzi wa Reli ya SGR nati zilizofungiwa taluma zinafunguliwa sana yani kuna maeneo hali ni mbaya biashara ya chuma chakavu cjui kama itaiacha hii reli salama waafrika hatupendi maendeleo na hta yakiletwa kwetu bdo 2tabomoa wenyewe kwa mikono yetu
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wawili (2) waliokuwa wanajaribu kuharibu kwa kukata baadhi ya vyuma vya ngazi moja ya nguzo namba P9 ya Daraja la Tanzanite lililopo maeneo ya Salender, Ilala.
Uzalendo ni mgumu sana kwa baadhi yetu!!
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wawili (2) waliokuwa wanajaribu kuharibu kwa kukata baadhi ya vyuma vya ngazi moja ya nguzo namba P9 ya Daraja la Tanzanite lililopo maeneo ya Salender, Ilala.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Muliro J. Muliro amesema watuhumiwa hao ambao majina yao (yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) walikamatwa tarehe 02/04/2022 saa 10 alfajiri wakiwa wanajaribu kufungua vyuma vilivyopo kwenye nguzo ijulikanayo kama P9 ambayo ipo kwenye daraja hilo. Wanahojiwa kwa kina na watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa hatua zaidi.

Pia Jeshi la Polisi limewakamata watu wengine kumi (10) waliokutwa chini ya Daraja huku wakidai wanaokota vyuma chakavu kwa ajili ya biashara ya vyuma. Watuhumiwa hao pia wanahojiwa kwa kina ili kubaini malengo yao kwa ujumla chini ya Daraja hilo yalikuwa ni nini na kuona kama wanamahusiano na wale waliokuwa wanajaibu kuiharibu baadhi ya miundombinu ya nguzo ya daraja hilo.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kuwa halitamvumia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma, Ulinzi katika eneo hilo na maeneo mengine umeeendelea kuimarishwa na atakayejaribu kuiharibu atakamatwa na mifumo ya kisheria ya kishughulika nae itazingatiwa.
View attachment 2175387
Yani watu ni wapuuuzi wa kutupwa, mtu anaharibu miundombinu ya mabilioni anaenda uza chumanbei chee
 
Back
Top Bottom