Dar: Waliomuua Wayne Derek Lotter wahukumiwa kunyongwa

Dar: Waliomuua Wayne Derek Lotter wahukumiwa kunyongwa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1669987194383.png

Hukumu imetolewa na Jaji Laila Mgonya wa Mahakama Kuu baada ya kuridhika na ushahidi kupitia mashahidi wake 32 ambao umethibitisha washtakiwa walitenda kosa hilo.

Mwanaharakati wa ujangili na raia wa Afrika Kusini, Wayne Derek Lotter aliuawa Agosti 16, 2017 kwa kupigwa risasi akiwa kwenye Taxi katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selaissie, Masaki, Kinondoni.

Awali washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa 22, lakini 11 waliachiwa huru na DDP. Waliotiwa hatiani na kuhukumiwa kifo ni Watanzania 9 na raia wawili wa Burundi.

==================

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa 11 katika kesi ya mauaji ya mwanaharakati wa ujangili, raia wa Afrika Kusini, Wayne Derek Lotter.

Katika hukumu yake iliyosomwa leo Ijumaa, Desemba 2, 2022 na Jaji Laila Mgonya imewatia hatiani washtakiwa hao baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake 32 kuwa umethibitisha mashtaka dhidi yao bila kuacha mashaka yoyote.

Waliotiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu hiyo ni pamoja na Rahma Almas, mkazi wa Mbagala B, Nduimana Ogiste, maarufu kama mchungaji na raia wa Burundi, Godfrey Salamba mkazi wa Kinondoni Msisiri A na Chambie Juma Ally, mkazi wa Kia/Boma.

Wengine ni Allan Elikana Mafue; Ismail Issah Mohammed (Machipsi); Leornad Phillipo Makoi; Ayoub Selemani Kiholi; Abuu Omary Mkingie na Habonimanda Augustine Nyandwi (pia raia wa Burundi) na Michael Dauv Kwavava;

Lotter ambaye alikuwa Mkurugenzi na Mwanzilishi-mwenza wa Shirika silo la kiserikali la PALMS Foundation, lililokuwa linahusisha na mapambano ya ujangili.

Mwanaharakati huyo aliuawa Agosti 16, 2017 kwa kupigwa risasi na watu waliomvamia akiwa kwenye teksii yeye na mwenzake, katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selaissie, Masaki wilayani Kinondoni.

Awali washtakiwa katika kesi hiyo ni 22, wakiwemo raia wa Burundi wawili.

Hata hiyo baada ya kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa usikilizwaji kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dar es Salaam, Kisutu iliyofunguliwa katika hatua ya uchunguzi wa awali kwa ajili ya kukamilisha taratibu za washtakiwa wanne walifutuwa kesi na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakabakia 11 ambao wote wametiwa hatiani.

Baada ya mahakama kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka iliwaachia huru washtakiwa wengine Saba baada ya kuridhika kuwa hawakuwa na kesi ya kujibu.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 13 ya mwaka 2021 washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili, kula njama kumuu Lotter na kumuua kwa maksudi Lotter.

Wametiwa hatiani Kwa makosa hayo yote kutokana na ushahidi wa mashahidi hao na vilelezo mbalimbali yakiwemo maelezo yao ya onyo waliyoyatoa wakihojiwa Polisi ambayo pia yameungwa mkono na ushahidi mwingine kama sheria inavyoelekeza.

MWANANCHI
 
Hata Mimi nimeshangaa Kwa Hilo,
Bongo bado upelelezi ni O,

Hapo walibanwa watu mbupu na koleo kupata ushahidi ambao hata uhakika nao hawana..

Kosa la kwanza ni kula njama. Watu wengi walihusika kwenye kuchora ramania la tukio la kufadhili mauaji hayo. Kumbuka alivamiwa na watu wanne, hivyo hao watatu walifanya mipango ya kumfatili na wengine kutoa fedha.
 
Kosa la kwanza ni kula njama. Watu wengi walihusika kwenye kuchora ramania la tukio la kufadhili mauaji hayo. Kumbuka alivamiwa na watu wanne, hivyo hao watatu walifanya mipango ya kumfatili na wengine kutoa fedha.
Hao waliokamatwa wana connection yeyote ya muingiliano wa kikazi na marehemu?

Isije ikawa walengwa wapo kidimbwi wanakula Bata,

Jumba bovu wameangushiwa wengine ambao hawana hatia.

Bongo hii hakuna linaloshindikana ikiwa zipo kesi kibao zinasuburi kupewa watu ambao hawana hatia.

Mimi Bado nina mashaka sn kutokana na udhaifu wa upelelezi wetu inchini.
 
High Court of Tanzania
Dar es Salaam, Tanzania

11 people sentenced to death for 2017 murder of anti-poaching activist Wayne Lotter​



Source: Video courtesy of Millard Ayo

A high court in Tanzania on Friday sentenced 11 people to death for the murder of a well-known conservationist in the East African country more than five years ago.

Anti-poaching activist Wayne Lotter, described as a "hero to many" for his anti-poaching efforts, was shot dead in August 2017 while riding in a taxi in Tanzania's commercial capital of Dar es Salaam.

TANZANIA-SAFRICA-CRIME-CONSERVATION
A picture taken on January 14, 2017, shows South African conservationist Wayne Lotter taking part in the Walk for Elephants event endorsed by the Chinese embassy, in Dar es Salaam. DANIEL HAYDUK/AFP VIA GETTY IMAGES

Those sentenced to death include nine Tanzanians and two citizens of neighboring Burundi. Tanzania hasn't carried out an execution in decades.


Poachers in Tanzania target various wildlife, including elephants that are often killed for their tusks.

Lotter was the director and co-founder of the PAMS Foundation, a nongovernmental organization which said he had helped to train thousands of game scouts throughout Tanzania and developed an "intelligence-based approach" to anti-poaching that had success in countering wildlife trafficking.

Krissie Clark, who co-founded the foundation with Lotter, told CBS News in 2019 that her colleague had received multiple death threats over his work with PAMS before being killed.

"If we really want to defeat this illegal wildlife trafficking, we have to go for the blood supply; we have to stop the money at the heart of this crime," Clark told CBS News.

After the announcement of the sentences, Clark released a statement saying she and her colleagues were relieved the trial was over.

"Wayne's murder and the sentencing of the eleven accused should serve as a reminder to everyone that poaching and wildlife crime is devastating to all of us," she said. "It destroys Tanzania's extraordinary natural heritage and damages families and communities. Wildlife crime doesn't pay

Source : CBS News
 
Soma jumla ya kurasa 33 za hukumu : Source : hapa chini :

Judgement

Republic vs. Khalid Almas Mwinyi @ Banyata & 17 Others (Criminal Session Case 13 of 2021) [2022] TZHC 13051 (20 September 2022);

… to commit Murder Their intention was to eliminate WAYNE DEREK LOTTER a South African National who had NGO in Tanzania known …
Court name
High Court of Tanzania
Case number
Criminal Session Case 13 of 2021
Media neutral citation
[2022] TZHC 13051
Judgment date
2022-09-20


IN THE HIGH COURT OF TANZANIADAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY AT DAR ES SALAAM CRIMINAL SESSIONS CASE NO. 13 OF 2021

REPUBLIC

Versus

1. KHALID ALMAS MWINYI @ BANYATA

2. RAHMA ALMAS MWINYI @ BABY @ RAHMA ALMAS IDDI

3. NDUIMANA OGISTE @ JONAS ZEBEDAYO@ MCHUNGAJI@ NDAYISHEMEZE ZEBEDE@ NDAISHIME ZEBEDAYO@ OMARI HASSAN

4. GODFREY PETER SALAMBA

5. CHAMBIE JUMA ALLY

6. ALLAN ELIKANA MAFUE

7. ISMAIL ISSAH MOHAMED @ MACHIPS

8. LEONARD PHILIPO MAKOI

9. AYOUB SELEMAN KIHOLI

10. JOSEPH ALEXANDER LUKOA

11. GAUDENCE JAMES MATEMU

12. ABUU OMARY MKINGIE

13. HABONIMANA AUGUSTIN NYANDWI @ OGISTEE

14. MICHAEL DAUD KWAVAVA

15. EMMANUEL THOMAS SONDE

16. KELVIN ATHANAS SOKO

17. SAMIA SALEH HUJAT

18. ALMAS SWEDI @ MALCOM

RULING ON A PRIMA FACIE CASE

Tuliondoka nyumbani kwa Fahami Karama huko Temeke majira ya kama saa mbili kasorobo usiku. Tulikuwa watu watatu katika gari Toyota IST mali ya Fahami ... Karama.”Further, the fact that the ....


12 Further, at the Police station, according to PW32-BF the cautioned statement of the 1st accused was procured while the 1st accused remained in custody from that day, todate, facing the charges as mentioned earlier.

Further the said car was kept under Police custody and the same was admitted forevidence in respect of this case as Exh. P28 respectively. However, up to the closure of the prosecution case, the 1st accused’s cautioned statement was not tendered before the court. The fact which prevented the court to get the benefit of knowing the contents of the same to further link the accused with the offences charged.

The 1st accused’s admission and confession of the fact that he is the owner of the car in issue (Toyota IST) Exh. P28 and also that the same is regularly used by Fahami Karamais well corroborated with the contents of 2nd accused’s cautioned statement, when interrogated about the ownership and the use of the said car. The 2nd accused said, and I quote:

“Hiyo gari ni mali ya mdogo wangu Khalid Almas anayefanya kazi benki ambaye tunaishi naye hapa nyumbani na pia amepanga nyumba nyingine huko Mikocheni B. Gari hiyo ameitoa kwa ajili ya matumizi ya familia kumsaidia Mama yetu na yeye Fahami Karama kwani ni mlemavu wa mguu, ana mguu wa bandia.

.... The concept of “no case to answer”of which is also knownas a “Prima facie case” is well entrenched practice in Common ...

READ MORE : SOURCE :
 
Kama wanajua kuwa kuna injinia wa hiyo kitu kwann hawakueataja mahakamani, hivi wewe unaweza kukubali kunyongwa na ukamuacha aliyesababisha wewe uingie hatiani anadunda uaraiani
Hao waliokamatwa wana connection yeyote ya muingiliano wa kikazi na marehemu?

Isije ikawa walengwa wapo kidimbwi wanakula Bata,

Jumba bovu wameangushiwa wengine ambao hawana hatia.

Bongo hii hakuna linaloshindikana ikiwa zipo kesi kibao zinasuburi kupewa watu ambao hawana hatia.

Mimi Bado nina mashaka sn kutokana na udhaifu wa upelelezi wetu inchini.
 
Back
Top Bottom