Dar: Waliomuua Wayne Derek Lotter wahukumiwa kunyongwa

Dar: Waliomuua Wayne Derek Lotter wahukumiwa kunyongwa

Hamna watu washenzi ,wezi na waharibifu kama wachina , na huu uvunaji haramu na ujangili wa rasilimali wanafanya all over Africa .
 
Halafu kati ya ile mikataba iliyosainiwa hivi karibuni inasema wao Wachina wasipewe adhabu au vipi?
 
Mkuu ongeza nyama kwa faida ya wengi.

Hao wauaji walikaa kikao wanunue silaha nje ya tanzania. Huyo Faume Karama alichukua Tzs3 million akampatia Makoi ambaye alimtumia Nduimana kwa njia ya western union ili anunue bunduki Burundi. Nduimana anadaiwa alinunua bunduki UZI na risasi 200, akaisafirisha isivyo kihalali hadi Tz, akampatia Faume.
 
Mzee hujui maana ya "kula njama" aliefyatua risasi ni mmoja lakini njama ya kunuia na mpango mzima ulipangwa na watu 11. Kwa iyo wote lazima wapigwe kitanzi wafe kwenye kamba na wanye mavi. Ukinyongwa kwa kamba mpaka "unye" na unazikwa na kimba.
Kuna kesi ya yule RPC Zombe na askari wenzake walikula njama wakauwa watu wanne akina Chigumbi na kuwapora fedha, waliachiwa na mahakama kisa muuaji "alitoroka" na hakuwepo mahakamani.
Muuaji ni yule aliyefyatua risasi.
Sasa hapa naona baada ya rufaa Kuna wengine watabadirishiwa adhabu na wakunyongwa atakuwa mmoja tuu.
 
Kama wanajua kuwa kuna injinia wa hiyo kitu kwann hawakueataja mahakamani, hivi wewe unaweza kukubali kunyongwa na ukamuacha aliyesababisha wewe uingie hatiani anadunda uaraiani
waliaminishwa ni kesi ndopo itakuwa hamna kunyongwa
 
Hao waliokamatwa wana connection yeyote ya muingiliano wa kikazi na marehemu?

Isije ikawa walengwa wapo kidimbwi wanakula Bata,

Jumba bovu wameangushiwa wengine ambao hawana hatia.

Bongo hii hakuna linaloshindikana ikiwa zipo kesi kibao zinasuburi kupewa watu ambao hawana hatia.

Mimi Bado nina mashaka sn kutokana na udhaifu wa upelelezi wetu inchini.
Sasa kama kashiriki nayeye si yumo unakubalije kula nyama ya binadamu, hata kama umekunywa mchuzi nawewe pia umekula nyama, tamaa hizo.
 
Ni ukweli sio pingika, Hiyo Mafia ya kichina inajulikana sana, hata Enzi ya Kikwete walijaribu kupakia ndege ya kiongozi wa china Meno ya Tembo, ambayo yalikamatwa na mambo yakazimwa ili kufunika kashfa hiyo, Huyo kiongozi wa kichina alikasirishwa sana na jambo hili, na akaitaka serekali yetu ichukue hatua kali kwa wahusika. Lakini Rushwa iliishinda kauli hiyo.

Kitu cha kusikitisha kuna watu 4 kati ya hao 11 hawahisiki kabisa na ni kesi ya kubambikizwa, na kati ya hao walioachiwa huru kuna 4 wanahusika vizuri sana.

Hii kesi inafaa kuchunguzwa vizuri, kwanza hao watu wamekaa Rumande zaidi ya miaka 5.
Makubwa haya, unajua ukiona rafiki hana mwenendo mzuri bora kuachana naye kabisa.
 
Ismail machipsi na makoi wameangukiwa na jumba bovu. Hawa watu hawawezi kula njama hata ya kuuwa mende.

Makoi mda wote yupo Arusha kwenye duka lake la dawa anauza.
Moyo wa mtu kichaka
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Ismail machipsi na makoi wameangukiwa na jumba bovu. Hawa watu hawawezi kula njama hata ya kuuwa mende.

Makoi mda wote yupo Arusha kwenye duka lake la dawa anauza.
Machips mtoto mdogo sana wa kiswahili/msomali wa kaloleni hawezi kuwa na hii misheni kubwa namna hii. Machips anafahamika ni jina maarufu mitaa ya hapo mjini kwa waswahili.
 
Walimuua kwa sababu gani?
Yapo mengi ya kujiuliza ukizingatia ulikuwa ni mwaka 2017, je taasisi yao ilikuwa na kiasi kikubwa cha fedha bank?. Hao wahalifu waliochangamana na warundi je hawana uhusiano na mauaji/mashambulio mengine yaliyokuwa yakitokea nyakati hizo?,
#YAPO MENGI YA KUHOJI KWA WATU HAWA!.
 
Obama ni kweli Hii kesi inawahusu wengi ambao wamefanya njama ya kuwabambikisa watu wasiohusika. Hii kesi wanaohusika ni mawaziri, vigogo wa idara ya wanyama pori, na wachina wakiongozwa na yule Malkia wa ujangili wa meno ya tembo ambaye alishikwa akahukumiwa jela, lakini sasa alitolewa kisirisiri na yuko Hong Kong. Hii kesi ilianza Mwigule alipokuwa waziri wa mambo ya ndani na anaijua vizuri na hata hao walio bambikizwa
umesema ukweli hii issue inahusisha idara mbalimbali za Mali asili na utalii. hawa walio hukumiwa sio hawa wanafahamu tu lakini wachora ramani wakubwa wa hii Biashara ni vigogo nadhani hata ndio waliodhamini hii ishu ya Lotter mtu kama Ismael Machips ambaye anaishi kwenye kiwanja cja urithi na nyumba ya familia wazazi. hawezi kuchora ramani kubwa hivi. ya kum dedisha mtu. wakate Rufaa.
kama unakumbuka vizuri sana Aliyekuwa waziri wa Utalii dr Kigwangalla aliwahi kusema na hata uzi wake upo humu JF yakwamba wauaji wa Wyne Lotter wapo uraiani wanadunda na ni vigogo. sasa ukiangalia hizo sura hapo za waliohukumiwa kuna kigogo hata mmoja hapo?
hawa wamehukumiwa tu kwa ushahidi wa kimazingara. ukiangalia jinsi hakimu anamalizia hukumu yake anadai huko polisi baada ya kukamatwa walipokea onyo ( ni kama vile Waliminywa wakakiri) pengine walikiri sababu ya kipigo. nashauri wakate Rufaa watafutwe wanasheria wazuri. kesi ianze upya.
 
Hivi kwanini mpaka leo, hukumu za kesi hapa Tanzania zinatolewa kwa lugha ya kigeni na sio kwa lugha yetu ya kiswahili ili wadau tuweze kusoma na kuelewa vizuri? haya mambo ya ajabu sana. [emoji2307]
 
Hivi kwanini mpaka leo, hukumu za kesi hapa Tanzania zinatolewa kwa lugha ya kigeni na sio kwa lugha yetu ya kiswahili ili wadau tuweze kusoma na kuelewa vizuri? haya mambo ya ajabu sana. [emoji2307]
nakazia hoja.


Hata hivyo, uhalifu haulipi, matokeo yake ni kuozea garezani na kuacha familia ikisambaratika.
 
Sasa kama kashiriki nayeye si yumo unakubalije kula nyama ya binadamu, hata kama umekunywa mchuzi nawewe pia umekula nyama, tamaa hizo.
Mkuu hujawahi kwenda mahabusu Kwa kesi ya uzururaji ,
Kufika mahakamani ukapewa murder Case?
Tena mpo 10 kwenye kesi na wote hamjuani.

Kesi za kubambikiwa zipo sn bongo.
 
Back
Top Bottom