Tatizo ni kituo cha mafuta sio genge ni lazima vijengwe kwa utaratibu bila hivyo tutaishia kuunguza mitaa mizima na mali za watu. Hiwezi kujenga vituo vya mafuta yanayoweza kulipuka kiholela holela eti kwasababu ya kodi. Kwani wananchi na maisha yao sio muhimu. Maisha ya watu sio ya kuchezea na utamaduni wa rushwa ndiyo umetufikisha hapa.
Mkuu tuwe wa kweli, kuna maeneo mangapi kwenye kila mtaa yaliyotengwa mahdusi kwa ajili ya vituo vya mafuta na mahitaji mengine muhimu ya jamii?
Je mwenye jukumu la kutenga hayo maeneo katekeleza wajibu wake kiasi cha kulaumu mwekezaji mzawa kuwa kakaidi kutotumia eneo mtalaamu kwa ya shughuli yake?
Mkuu umeme na mishumaa inaongoza kwa kuunguza nyumba za watu ha mjini, mbona hupigi kelele na kutoa povu namna hii hapa?
Kwenye nyumba na familia nyingi mijini kuna magari yakiwa na petrol/gesi kwenye matenki na mitungi yenye gesi tunalala nayo na hailipuki?
Kuna mpango wa serikali na sehemu kadhaa mjini majaribio yalishaanza ya kusambaza gesi kwa kutumia mabomba, mbona hofu ya kulipuka kwa gesi na kuunguza mitaa haipo??
Je wajua kuwa ili Kituo cha mafuta kijengwe lazima pawepo na kibali cha ardhi, mazingira, Moto na uokoaji, Ewura, Serikali ya mtaa, Brela, TRA, Mipango miji, Manispaa? Yote hayo ni kuthibitisha usalama wa uwekezaji.
Mkuu suala hapa ni kuwezesha wawekezaji kufanya uwekezaji salama na endelevu kwa kuzingatia teknolojia ya kuzuiwa na kudhibiti janga la moto. Pili, ni kutoa elimu na mafunzo maalum na ya mara kwa mara kwa mwekezaji na wa kazi majirani.
Faida ya uwekezaji ni kubwa kuliko hofu ya kufikirika kwa dunia ya sasa. Uwekezaji wa namna hii huleta huduma mchanganyiko karibu na watu, huajiri vijana na serikali kupata kodi yake kuinua uchumi wa taifa.
Tuachane na hizi ni fikra za kijinga, kijima, kijamaa, kurudisha nyuma, kukwamizana na kufilisiana. Rais ana hangaika kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ila wananchi tumekazana kuchukia na kufukuza wawekezaji wazawa.