Dar: Wananchi wamelalamikia kujengwa kwa Kituo cha kuuza mafuta cha Barrel Petrol Station karibu na makazi yao

Dar: Wananchi wamelalamikia kujengwa kwa Kituo cha kuuza mafuta cha Barrel Petrol Station karibu na makazi yao

Nchi inahitaji kodi kuliko chochote, kuliko hata uwaziri wa Jerry Silaa. Bora Silaa aondoke kituo cha mafuta kibaki, vikodi vya mshahara wa Silaa havifiki milioni 10 kwa mwezi, kituo cha mafuta kinaweza kuingiza hata milioni 500 kwa mwezi.

Hata kliniki za ardhi ni njia yake ya kutegeshea rushwa
Haijalishi kuna vituo vingapi. Kodi ya serikali ni ile ile kwani matumizi ya mafuta kwa nchi hayaongezeki kwa kuongeza vituo.
 
Kuna ka "ujinga" kanapita mitandaoni eti kuna watu walijaribu kumuhonga waziri Jerry Silaa. Takukuru wapo, na namba zao anazo, na huwa wanaweka mitego kunasa watoa rushwa.

Waziri ni kiongozi wa ngazi ya kitaifa, ana namba ya boss wa takukuru, kwa nini hakuweka mtego?

Walijadiliana halafu hazikutosha akaona awahi kuwalipua? Aliwaomba hizo hela wakasema hawana akaona awawahi?

Waziri analalamika, wanajimbo wake wafanyeje? Waziri yuko karibu na kila taasisi?

Huyu ataongoza vita ya rushwa wizara ya ardhi wakati hajui sehemu ya kuripoti rushwa?

Useless,aliomba akanyimwa, mawaziri vijana, acheni tamaa, Samia,kazi kwako.

Naona kaitisha umiliki wa ardhi wa vituo vya mafuta nchi nzima, maokoto yake sio mchezo, kamishna wa ardhi atakayepeleka maokoto mengi ndiye atadumu. Anadhani watampa hela za bure (rushwa) ili asivunje vituo vyao

Ajue tu, kodi ya mafuta ndio injini ya bajeti, na mafuta yameangusha wanasiasa wa mashariki ya kati, kabla hajaangusha serikali ya samia, ataanguka yeye. Kama kajipanganga kubomoa vituo vya mafuta nchi nzima, nchi nzima itambomoa yeye.
Kimsingi, Jerry Silaa hatoshi kwenye hiyo nafasi ya Waziri wa Ardhi, yaani hatoshi kabisa.
Rais endapo kama bado anampenda sana Jerry Silaa kuendelea kuwepo kwenye Baraza lake la Mawaziri, basi ni vyema akambadilishia Wizara.
Naongea bila unafiki moyoni mwangu: William Lukuvi alijitahidi sana kwenye nafasi hiyo ya Waziri wa Ardhi, ikiwezekana arudishwe.
 
Nchi yetu ni muhimu kuliko yeyote.Mwekezaji asiefuata taratibu,sheria,kanuni na mila Za nchi hatufai..

Ifike wakati kila mmoja wetu awajibike Kwa mujibu wa Matakwa ya Katiba,utaratibu na sheria au miongozo ya nchi..Juzi tulikuwa na Mh Lukuvi,Leo tuna Slaa,Yamkini kesho tukawa na Mwambukusi..Au Vivek..

Upindishaji wa mambo na shortcuts gharama yake ni kubwa.Yamkini Una vinasaba na utawala A,B,C.. ipo Siku utakuja utawala D ulio kinyume na urafiki/kujuana/Rushwa/ufisadi..ikiwa uliishi kinyume au kufanya biashara Kwa kupendelewa au kufumbiwa macho lazima kuwe na vilio na kisaga meno..
Mkuu kama ulifuatilia mahojiano ya mkuu wa mkoa ndugu Chalamila na ndugu Tibaijuka, mkuu wa mkoa alibainisha kuwa mwekezaji ana vibali vyote na ni halali.

Mkuu ukisikilizaji maelezo ya Tibaijuka and Co kwa makini hayana mashiko. He who alleges bear the burden of proof.

They just are hell bent kuzuia mwekezaji kwa sababu na chuki zao binafsi.
 
Kuna ka "ujinga" kanapita mitandaoni eti kuna watu walijaribu kumuhonga waziri Jerry Silaa. Takukuru wapo, na namba zao anazo, na huwa wanaweka mitego kunasa watoa rushwa.

Waziri ni kiongozi wa ngazi ya kitaifa, ana namba ya boss wa takukuru, kwa nini hakuweka mtego?

Walijadiliana halafu hazikutosha akaona awahi kuwalipua? Aliwaomba hizo hela wakasema hawana akaona awawahi?

Waziri analalamika, wanajimbo wake wafanyeje? Waziri yuko karibu na kila taasisi?

Huyu ataongoza vita ya rushwa wizara ya ardhi wakati hajui sehemu ya kuripoti rushwa?

Useless,aliomba akanyimwa, mawaziri vijana, acheni tamaa, Samia,kazi kwako.

Naona kaitisha umiliki wa ardhi wa vituo vya mafuta nchi nzima, maokoto yake sio mchezo, kamishna wa ardhi atakayepeleka maokoto mengi ndiye atadumu. Anadhani watampa hela za bure (rushwa) ili asivunje vituo vyao

Ajue tu, kodi ya mafuta ndio injini ya bajeti, na mafuta yameangusha wanasiasa wa mashariki ya kati, kabla hajaangusha serikali ya samia, ataanguka yeye. Kama kajipanganga kubomoa vituo vya mafuta nchi nzima, nchi nzima itambomoa yeye.
Mkuu ameyaweka mafuta ya kumchemsha mwenyewe kikaangoni, ni suala la muda tu ajikaange! Tusubiri tu, yetu macho!
 
Nchi inahitaji kodi kuliko chochote, kuliko hata uwaziri wa Jerry Silaa. Bora Silaa aondoke kituo cha mafuta kibaki, vikodi vya mshahara wa Silaa havifiki milioni 10 kwa mwezi, kituo cha mafuta kinaweza kuingiza hata milioni 500 kwa mwezi.

Hata kliniki za ardhi ni njia yake ya kutegeshea rushwa

Tatizo ni kituo cha mafuta sio genge ni lazima vijengwe kwa utaratibu bila hivyo tutaishia kuunguza mitaa mizima na mali za watu. Hiwezi kujenga vituo vya mafuta yanayoweza kulipuka kiholela holela eti kwasababu ya kodi. Kwani wananchi na maisha yao sio muhimu. Maisha ya watu sio ya kuchezea na utamaduni wa rushwa ndiyo umetufikisha hapa.
 
Mkuu tuwe wa kweli, kuna maeneo mangapi kwenye kila mtaa yaliyotengwa mahdusi kwa ajili ya vituo vya mafuta na mahitaji mengine muhimu ya jamii?

Je mwenye jukumu la kutenga hayo maeneo katekeleza wajibu wake kiasi cha kulaumu mwekezaji mzawa kuwa kakaidi kutotumia eneo mtalaamu kwa ya shughuli yake?

Mkuu umeme na mishumaa inaongoza kwa kuunguza nyumba za watu ha mjini, mbona hupigi kelele na kutoa povu namna hii hapa?

Kwenye nyumba na familia nyingi mijini kuna magari yakiwa na petrol/gesi kwenye matenki na mitungi yenye gesi tunalala nayo na hailipuki?

Kuna mpango wa serikali na sehemu kadhaa mjini majaribio yalishaanza ya kusambaza gesi kwa kutumia mabomba, mbona hofu ya kulipuka kwa gesi na kuunguza mitaa haipo??

Je wajua kuwa ili Kituo cha mafuta kijengwe lazima pawepo na kibali cha ardhi, mazingira, Moto na uokoaji, Ewura, Serikali ya mtaa, Brela, TRA, Mipango miji, Manispaa? Yote hayo ni kuthibitisha usalama wa uwekezaji.

Mkuu suala hapa ni kuwezesha wawekezaji kufanya uwekezaji salama na endelevu kwa kuzingatia teknolojia ya kuzuiwa na kudhibiti janga la moto. Pili, ni kutoa elimu na mafunzo maalum na ya mara kwa mara kwa mwekezaji na wa kazi majirani.

Faida ya uwekezaji ni kubwa kuliko hofu ya kufikirika kwa dunia ya sasa. Uwekezaji wa namna hii huleta huduma mchanganyiko karibu na watu, huajiri vijana na serikali kupata kodi yake kuinua uchumi wa taifa.

Tuachane na hizi ni fikra za kijinga, kijima, kijamaa, kurudisha nyuma, kukwamizana na kufilisiana. Rais ana hangaika kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ila wananchi tumekazana kuchukia na kufukuza wawekezaji wazawa.
 
Nchi inahitaji kodi kuliko chochote, kuliko hata uwaziri wa Jerry Silaa. Bora Silaa aondoke kituo cha mafuta kibaki, vikodi vya mshahara wa Silaa havifiki milioni 10 kwa mwezi, kituo cha mafuta kinaweza kuingiza hata milioni 500 kwa mwezi.

Hata kliniki za ardhi ni njia yake ya kutegeshea rushwa
Hizi akili za Chipukizi zimekuwa tatizo hapa jukwaani!
Ni sheria ipi inayoruhusu kituo kujengwa kwenye makazi ya watu?
Hiyo Petrol station ipo hapo kwa rushwa kama ambavyo wametaka kumuonga Waziri.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo aliyojenga amefanya hivyo bila vibali au?
Rushwa ndio inafanya wapate vibali vinavyokinzana na sheria.

Tuseme jambo kubwa linalotakiwa kufanyika ni Serikali kukubali kuwakabili na kushitaki watu wake ndani ya ofisi za umma ambao ndio wanatoa vibali vilivyo kinyume na sheria

Pengine zaidi ya nusu ya vituo vyote vya mafuta havikidhi matakwa ya sheria ya kuwepo maeneo vilipo. Vituo vipo katika umbali wa mita 200 kutoka kimoja hadi kingine, huku sheria inataka viwe umbali wa kilomita 50
 
Hizo sheria zinazingatiwa mikocheni tu? Uswahilini kuna vituo kibao kwenye makazi ya watu wilaya zote za Dar es salaam mbona hajashupalia huko?
Why mikocheni? Only.Mmm au alitaka dau kubwa zaidi akamwambia mimi.nina milioni.300 tu akagoma
Hahah ina maana watu wa tandale huko ni mazoba,maana wamejaziwa vituo mpaka vibarazani

Ova
 
Back
Top Bottom