Dar: Washukiwa wa biashara ya dawa za kulevya watiwa mbaroni

Dar: Washukiwa wa biashara ya dawa za kulevya watiwa mbaroni

MAMLAKA ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya jana tarehe 15 April 2020, imefanikiwa kumkamata kigogo wa dawa za kulevya raia wa Nigeria Kanayo David Chukwu (39) mkazi wa Masaki jijini Far we Salaam.

Pia inawashikilia raia wawili wa Tanzania Alistair Amon Mbele(38) ambaye ni mkutubi wa Chuo Kikuu cha Aghakan jijini Dar es Salaam, mkazi wa Mbezi Kibanda cha mkaa na Isso Romward Lupembe (49) ambaye Ni mkazi wa Mbezi Louis na Changanyikeni jijini.
Watuhumiwa wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin zinazokadiliwa kuwa na zaidi ya kilogramu 270 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye moja ya nyumba iliyopo Mbezi kibanda cha mkaa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa muda mrefu nchini na kwamba Mamlaka imefanikiwa kukamatwa kutokana na jitihada ushirikiano uliopo kati ya nchi yetu na nchi nyingine katika kupambana na tatizo la dawa za kulevya duniani kutokana na utaratibu wa kubadirishana taarifa ambazo husaidia kurahisha ukamataji huo. “Baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyombo mbalimbali vya usalama ndani na nje ya nchi tulianza kuwafuatilia toka tarehe nane na kufanikiwa kuwaweka mtegoni tangu wakiwa wanateremsha mzigo na kufanikiwa kuwakamata. "Pia watuhumiwa hao walikuwa wamefanya maandalizi ya kupokea mzigo huo kwa kujenga tenki la maji machafu ambalo liliwekwa chemba juu ya kuhifadhia dawa hizo na bahati mbaya mzigio uliwahi kufika kabla tenki halijakamilika, hivyo kulazimika kuzihhifadhi ndani ya nyumba,"amesema
Kamishna Kaji.
View attachment 1420869View attachment 1420870View attachment 1420871View attachment 1420872
Kilo 270 ni sawa na debe 13.5 za mahindi sawa na pipa la debe kumi na mbili. Hao ni wauaji wa watoto wetu
 
Mkuu hesabu za wap hizo.. Kwahiyo 50mx270 ni 1.3b!??
 
Hawa Naijas ndo watabe wa mambo haramu Africa... .Udukuzi,drug trafficking nk
 
Back
Top Bottom