Dar: Washukiwa wa biashara ya dawa za kulevya watiwa mbaroni

Dar: Washukiwa wa biashara ya dawa za kulevya watiwa mbaroni

Nipeni hata niwatie jeraha, wameniharibia mwanangu,


Sent using Jamii Forums mobile app
pole madam, mie mdogo wangu wa kunifata kabisa ameharibiwa na haya makitu.

kama si bahati mbaya mmoja wa watuhumiwa kwa ubini wake ni mtoto wa Mzee na rafiki yangu Marehemu Prof. Amon Mbele, mwanataaluma na mtu wa haki na muwazi kusema analoona ni sahihi.
 
duh!!..huyo alistair mbele sijui ni tamaa au kitu gani.

hakuwa wa kujiingiza kwenye biashara hii haramu maana kama elimu anayo na pesa ya kula na ya kuvimbia mjini pia alikuwa nayo. licha ya hivyo mshua wake ambae kwa sasa ni marehemu alikuwa ni senior academician wa chuo kikuu.
 
MAMLAKA ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya jana tarehe 15 April 2020, imefanikiwa kumkamata kigogo wa dawa za kulevya raia wa Nigeria Kanayo David Chukwu (39) mkazi wa Masaki jijini Far we Salaam.

Pia inawashikilia raia wawili wa Tanzania Alistair Amon Mbele(38) ambaye ni mkutubi wa Chuo Kikuu cha Aghakan jijini Dar es Salaam, mkazi wa Mbezi Kibanda cha mkaa na Isso Romward Lupembe (49) ambaye Ni mkazi wa Mbezi Louis na Changanyikeni jijini.

Watuhumiwa wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin zinazokadiliwa kuwa na zaidi ya kilogramu 270 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye moja ya nyumba iliyopo Mbezi kibanda cha mkaa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa muda mrefu nchini na kwamba Mamlaka imefanikiwa kukamatwa kutokana na jitihada ushirikiano uliopo kati ya nchi yetu na nchi nyingine katika kupambana na tatizo la dawa za kulevya duniani kutokana na utaratibu wa kubadirishana taarifa ambazo husaidia kurahisha ukamataji huo.

“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyombo mbalimbali vya usalama ndani na nje ya nchi tulianza kuwafuatilia toka tarehe nane na kufanikiwa kuwaweka mtegoni tangu wakiwa wanateremsha mzigo na kufanikiwa kuwakamata.

"Pia watuhumiwa hao walikuwa wamefanya maandalizi ya kupokea mzigo huo kwa kujenga tenki la maji machafu ambalo liliwekwa chemba juu ya kuhifadhia dawa hizo na bahati mbaya mzigio uliwahi kufika kabla tenki halijakamilika, hivyo kulazimika kuzihhifadhi ndani ya nyumba,"amesema
Kamishna Kaji.

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania kwa kutoa taarifa pale wanapoona matukio yasiyo ya kawaida kwa usalama.

“Kilo hizi ni nyingi sana zingeingia mtaani zingeathiri nguvu kazi ya vijana wetu huko mitaani kwa kiasi kikubwa. Ninasikitika kuona bado kuna watu wasio na utu wanaendelea kujitafutia kipato kwa njia hii haramu bila kujali. Ninatoa rai kwa watanzania walio tayari kuwapambania watoto wao kuendelea kushirikiana na Mamlaka kuwafichua watu hawa bila woga," amefafanua.

Ameongeza kuwa watuhumiwa wako mikononi mwa Mamlaka na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika ili sheria ichukue mkondo wake. #swahibablog

85036a40-6c14-426e-bcbd-9713b9c07805.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Far We Salaam ni wapi!??

Unawahi wapi mkuu..!?
 
Wangefanikiwa kuuza huo mzigo... Looh salale wangekuwa wanalala kwenye magunia yaliyojaa manoti
Kweli biashara haramu kuisha duniani ni jambo gumu sana. Ni mwendo wa kubadili tu mbinu. Ukiziba huku, wanapita kule. Kazi kweli kweli. Na uzuri ndizo zinazoleta faida kubwa zaidi kwa wahusika, kuliko biashara halali.

Jr[emoji769]
 
Nigeria ndo nchi inayoongoza kua na idadi kubwa ya watu. Wapo 190,000,000. Wasomi wengi Ajira hamna imewalazimu wajiongeze. Watanzania tupo 60,000,000 tu lakini soko la ajira hali ni tete. Na sisi tunaelekea huko huko.

Sent From Galaxy S9
 
Back
Top Bottom