Dar: Watu wanne wa familia moja wafariki baada ya kuvuta hewa chafu ya jenereta

Nanukuu "kuvuta hewa iliyochafuka kwa carbonmonoxide na kuishia kupoteza maisha." Hapo umetoa Scientific explanation ya kisababishi (cause)cha vifo hivyo.
Lakini uchunguzi wa Polisi eti unaendelea 🙄 🙄
 
Jiko la mkaa ni baya sana kulala nalo chumbani, ukipitiwa na usingizi ukalala huku jiko hilo likiwa linawaka unalala moja kwa moja, yaani unafia usingizini. Ukishituka ukabahatika kunyanyuka utajikuta huna nguvu za kutembea na unaweza kudondoka chini kama umepalalaizi, ukipata hewa safi nguvu zinarejea. Madirisha yafunguliwe hewa safi iingie ndani
 
Upo sahihi kabisa , iliwahi kunitokea, Nikiwa mtoto huko mkoani njombe .tulilala na jiko la mkaa na nyumba za kijijini hazina ventilation, bahati yetu ni ilikuwa msibani kuna watu walilala nje ya nyumba wakasikia dada anakohoa na kuhangaika ndo kuja kufungua mlango na kutuokoa .
It is a very easy way of dying , maana unalala unapitilizia kwenye comma na kuondoka zako duniani.
 
Jiko la Mkaa unalala nalo ndani ili iweje? Hujaenda shule hata kidogo?
 
Duuh! Ajali kama hiyo ya Moshi wa jenereta iliwahi kutokea Zanzibar mwaka Fulani hivi,wanafamolia 8 walipoteza maisha.
Moshi wa jenereta ni mbaya sana, yani ukika hata nje tu karibu na jenereta moshi wake unakera. Seuze ulale nalo aisee ni shida. Its better kulichimbia underground kisha ukalifungia huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…