Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Unaweza usiamini lakini ndivyo hali ilivyo katika eneo moja jijini Dar es Salaam, ambalo limegeuzwa kuwa soko la wazi la kufanyia vitendo vya ngono hadharani. Eneo hilo lililopo Mbagala Zakhem katika manispaa ya Temeke, limekuwa maarufu na kuwavutia wanawake wengi na wanaume wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.
Jeshi la polisi limethibitisha kuwa na taarifa za kuwapo kwa eneo hilo na kufanyika kwa biashara ya ngono hadharani. Kamanda wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo anasema, "ninalijua eneo hilo na biashara haramu inayofanyika, tunajipanga kupata namna bora ya kuidhibiti."
Vitendo hivyo viovu vimekuwa vikifanywa nyakati za usiku. Kutokana na uwepo wa hali hiyo, eneo hilo limekuwa na mlundikano wa mipira ya kiume (kondom) na kusababisha afya za watu hasa watoto kuwa hatarini, huku mazingira yakizidi kuchafuka. Uchunguzi umebaini wanawake wanaofanya biashara hiyo hutembea na wanaume kufikia zaidi ya 10 kwa siku.
HALI HALISI
Mara ya kwanza ukifika eneo la Zakhem jirani na ukumbi maarufu wa burudani (jina linahifadhiwa), huwezi kufikiria kama eneo hilo nyakati ya usiku linageuka kuwa eneo lile la Sodoma na Gomora iliyosimuliwa kwenye vitabu vya dini. Eneo hilo lenye hali ya utulivu nyakati za mchana, kuanzia saa 1:00 usiku, hubadilika na kuwa danguro la aina yake linalofanana na ‘soko la wazi la ngono', ambapo hali hiyo huendelea hadi nyakati za alfajiri.
Ndani ya ‘soko' hilo lenye idadi kubwa ya wanawake wanauza miili yao maarufu kama changudoa ama dada poa, hakuna utaratibu wa kufanya vitendo hivyo katika faragha, badala yake inafanyika kwenye maeneo ya wazi. Vitendo hivyo vinapofanyika, vinashuhudiwa na watu waliopo maeneo ya karibu, wengine wakisubiri zamu zao kutoka kwa mwanamke mhusika.
Wakati hali ikiwa hivyo, wanaume waliogundulika kufika kwenye maeneo hayo ni wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 50, wakiwa wenye hadhi na nyadhifa tofauti. Gharama iliyobainika kutozwa kwa kila tendo la ngono linapofanyika mara moja, ni Shilingi 3,000.
Eneo hilo linazungukwa na vibanda vya mama lishe, likiwa na ukubwa takribani mita 25. Mmoja wa wanawake wanaofanya biashara hiyo (jina linahifadhiwa), anasema yupo na wenzake zaidi ya 30 na wana uwezo wa kuwahudumia wanaume kati ya 100 hadi 300.
"Hapa kila mtu anapata fedha kulingana na nguvu yake, sasa ukitafuta chumba utapoteza muda ni bora tuwahudumie hapa kwenye eneo la wazi huku wengine wakitusubiri," anasema mwanamke huyo. Hata hivyo, alisema kwa upande wake, usiku huo alikuwa amekutana na wanaume 25 na kufanikiwa kujikusanyia Shilingi 50,000.
Alisema wateja wao wameshazoea kufanya ngono kwenye eneo la wazi. "Si unaona watu wote wale wanasubiri wenzao wamalize, ni vyema wakaangalia, wanapoona mwenzao amemaliza yeye aingie," aliongeza kusema huku akionyesha kundi la watu zaidi ya 20 wakiwa pembeni wakisubiri.
BABU AONGOZA
Kwenye eneo hilo kuna kiongozi wao ambaye anafahamika kwa jina moja la Babu, yeye ndiye mwenye mamlaka ya ulinzi na kutoza faini kwa anayekiuka taratibu walizojiwekea. Hata hivyo, kazi nyingine ya Babu ni kukusanya kondom zinazotumika ama kutupwa hovyo kwenye eneo hilo.
Babu, anasema kwa kawaida anaokota kiasi ndoo tatu za kondomu zilizotumika. "Kazi yangu ni kuwalinda (wanaofanya ngono) dhidi ya vurugu zinazoweza kutokea, na kufanya usafi," anasema.
Hisani ya Nipashe, na itaendelea......