Dar yageuka `Sodoma` kwa ngono za wazi hadharani

Dar yageuka `Sodoma` kwa ngono za wazi hadharani

Ninachoweza kufahamu ni kwamba Mbunge amejitahidi kutambua na kufuatilia tatizo lililopo, lakini tujue kila mtu ana mipaka yake kiutendaji na si kazi ya mbunge kuwashika na kuwashtaki wahalifu.

Baada ya mbunge kutembelea sehemu hiyo na kuchukua picha za maeneo husika zinazoashiria kuwepo kwa matukio hayo sina shaka anawasiliana na vyombo husika kuchukua hatua katika kukabiliana na tatizo hili. Nasisitizi si kazi ya mbunge kuwashika au kuwashtaki wahusika ila kuwasiliana na vyombo husika. Ni mapema mno maana kasema jana tu ametembelea eneo la tukio na tumpe nafasi ya hatua anazozichukua kuwasiliana na vyombo husika.

CC; Dr F. Ndugulile

Yeye kasema kwamba hana comment. Haya maneno alipaswa ayaseme yeye, au amekuPM akakuomba umsaidie kujibu?
 
We princess hujui kwamba nyie wanawake ndio mnasababisha tunachepuka. Mume anaomba uroda unampatia kama si haki yake vile. mara nyingine unasingizia kichwa au tumbo u kuchoka wakati ndume inataka kuimarisha ndoa. Kesho yake akitoka Darlive lazima apunguze genyege kabla ya kurudi home. bia ya leo buku 2 lazima atafute papuchi ya bei poa.
Kuna kaukweli fulani hivi ndani yake
 
Yeye kasema kwamba hana comment. Haya maneno alipaswa ayaseme yeye, au amekuPM akakuomba umsaidie kujibu?

Mbunge kajibu kifalsafa, kwa maneno mengine bora kunyamaa kuliko kujibizana na watu wasioelewa taratibu za uwajibikaji. Mapema mno kumnyoshea kidole mbunge, kuna ushirikisha vyombo husika vyenye kuchukua jukumu na dalili kwamba mbunge hajaridhishwa na tukio hilo hadi kafunga safari kutembelea eneo husika na kutushirikisha taswira hizo hapa jukwaani kuna credit ambazo anastahili kupewa.
 
Afadhali wewe umeliona hili, maana hawa wafanya ufuska wasingeweka maskani hapo kama kusingekuwa na wateja. Katika miji kadhaa nchini Marekani kulikuwa na tatizo kama hilo la makahaba na ilikuwa vigumu kuvunja ngome zao. Polisi walichofanya ni kuajiri wanawake kadhaa wanaoonekana kuwa na mvuto na mtazamo kama wa kikahaba vile, wakawa wanapozi huku wakiwarembulia wanaume wakati wameficha vinasa sauti ambavyo vilirusha mawimbi ya sauti hadi mafichoni kwa polisi. Kwa nia hii walishikwa wanaume wengi na kutiwa ndani. Kwa njia hii biashara haramu ilikoma kwa vile hakuna mwanaume aliyekuwa tayari kuumbuka.

Ninachoshangaa Tanzania wanashikwa wanawake tu bila wanaume wanaowanunua hao wanawake. Nimepita mara kadhaa mitaa ya huko Kinondoni panakera, Buguruni nako majira ya jioni utaona wasichana ndio kumekucha wanaingia kazini, katikati ya jiji karibu na mahoteli nako wanaojipitishapitisha ni kwa wingi tu, lakini wanaoonwa ni hao wasichana si wanaume wanaowazungukia kuwarubuni.

Kuna watu wanaofanya biashara hiyo ishamiri, mbona mie sijawahi kutongozwa na hao machangu ilipotokea kupita maeneo hayo? Wanaangalia mtu mwenye pepo la ngono, na zaidi wana wateja wao si kila kiruka njia.

Well said! Ni vizuri kuikomesha biashara hii haramu inayodhalalisha heshima na utu wa mwanadamu! Polisi waachane kutumia mbinu za kizamani. wawashughulikie zaidi wale wanaoifanya biashara hii kushamiri ambao ni wanaume.... Wanaume wengi wanachelea sana kuaibika. Wakitiwa msukosuko dada poa watakosa wateja na hivyo kuachana na biashara yenye.. If the demand is curbed automatically the supply will dry up.
Serikali ktk ngazi zote (taifa, jiji, manispaa kata) nayo itengeneze mazingara na fursa kwa wananchi wake kujipatia vipato halali..Nasi wananchi tuchape kazi! Watanzania wote wanastahili kuishi maisha yenye utu na heshima.
 
Hatua zimechukuliwa. Madanguro yamevunjwa na kusafishwa leo mchana.

Mbona sasa nimepita maeneo hayo kazi zinaendelea mkuu! au umepata ripoti vibaya.....

Natokea konge nimeona habar hii nikapita hapo tena wamenirukia nikalala mbio.
 
Mbona sasa nimepita maeneo hayo kazi zinaendelea mkuu! au umepata ripoti vibaya..... Natokea konge nimeona habar hii nikapita hapo tena wamenirukia nikalala mbio.

Hatua zimechukuliwa. Madanguro yamevunjwa na kusafishwa leo mchana.
Kigamboni na Tanzania kwanza

Mh kwanza habari za Bunge la Katiba, au hukuhudhuria
Naomba tena uifuatilie hii Habari ni kweli wamerudi, SAIDIA kusafisha hapo mahali, Tuana watoto huko Dodoma Mama zao wapo hapo Mbagala, wanadai wamepata ajira. inaelekea bado
cc Candid Scope
 
Mbona sasa nimepita maeneo hayo kazi zinaendelea mkuu! au umepata ripoti vibaya.....

Natokea konge nimeona habar hii nikapita hapo tena wamenirukia nikalala mbio.

Tumplekee habari hiyo Mbunge Faustine aende akafanye ukaguzi tena maana hawa polisi jamii hawaeleweki huenda ndio wateja wakuu pale maana biahsara hizo ni za majira ya jua likishazama na wao polisi ndio wako zamu.
 
attachment.php

Unaweza usiamini lakini ndivyo hali ilivyo katika eneo moja jijini Dar es Salaam, ambalo limegeuzwa kuwa soko la wazi la kufanyia vitendo vya ngono hadharani. Eneo hilo lililopo Mbagala Zakhem katika manispaa ya Temeke, limekuwa maarufu na kuwavutia wanawake wengi na wanaume wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

Jeshi la polisi limethibitisha kuwa na taarifa za kuwapo kwa eneo hilo na kufanyika kwa biashara ya ngono hadharani. Kamanda wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo anasema, "ninalijua eneo hilo na biashara haramu inayofanyika, tunajipanga kupata namna bora ya kuidhibiti."

Vitendo hivyo viovu vimekuwa vikifanywa nyakati za usiku. Kutokana na uwepo wa hali hiyo, eneo hilo limekuwa na mlundikano wa mipira ya kiume (kondom) na kusababisha afya za watu hasa watoto kuwa hatarini, huku mazingira yakizidi kuchafuka. Uchunguzi umebaini wanawake wanaofanya biashara hiyo hutembea na wanaume kufikia zaidi ya 10 kwa siku.

HALI HALISI
Mara ya kwanza ukifika eneo la Zakhem jirani na ukumbi maarufu wa burudani (jina linahifadhiwa), huwezi kufikiria kama eneo hilo nyakati ya usiku linageuka kuwa eneo lile la Sodoma na Gomora iliyosimuliwa kwenye vitabu vya dini. Eneo hilo lenye hali ya utulivu nyakati za mchana, kuanzia saa 1:00 usiku, hubadilika na kuwa danguro la aina yake linalofanana na ‘soko la wazi la ngono', ambapo hali hiyo huendelea hadi nyakati za alfajiri.

Ndani ya ‘soko' hilo lenye idadi kubwa ya wanawake wanauza miili yao maarufu kama changudoa ama dada poa, hakuna utaratibu wa kufanya vitendo hivyo katika faragha, badala yake inafanyika kwenye maeneo ya wazi. Vitendo hivyo vinapofanyika, vinashuhudiwa na watu waliopo maeneo ya karibu, wengine wakisubiri zamu zao kutoka kwa mwanamke mhusika.

Wakati hali ikiwa hivyo, wanaume waliogundulika kufika kwenye maeneo hayo ni wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 50, wakiwa wenye hadhi na nyadhifa tofauti. Gharama iliyobainika kutozwa kwa kila tendo la ngono linapofanyika mara moja, ni Shilingi 3,000.

Eneo hilo linazungukwa na vibanda vya mama lishe, likiwa na ukubwa takribani mita 25. Mmoja wa wanawake wanaofanya biashara hiyo (jina linahifadhiwa), anasema yupo na wenzake zaidi ya 30 na wana uwezo wa kuwahudumia wanaume kati ya 100 hadi 300.

"Hapa kila mtu anapata fedha kulingana na nguvu yake, sasa ukitafuta chumba utapoteza muda ni bora tuwahudumie hapa kwenye eneo la wazi huku wengine wakitusubiri," anasema mwanamke huyo. Hata hivyo, alisema kwa upande wake, usiku huo alikuwa amekutana na wanaume 25 na kufanikiwa kujikusanyia Shilingi 50,000.

Alisema wateja wao wameshazoea kufanya ngono kwenye eneo la wazi. "Si unaona watu wote wale wanasubiri wenzao wamalize, ni vyema wakaangalia, wanapoona mwenzao amemaliza yeye aingie," aliongeza kusema huku akionyesha kundi la watu zaidi ya 20 wakiwa pembeni wakisubiri.

BABU AONGOZA
Kwenye eneo hilo kuna kiongozi wao ambaye anafahamika kwa jina moja la Babu, yeye ndiye mwenye mamlaka ya ulinzi na kutoza faini kwa anayekiuka taratibu walizojiwekea. Hata hivyo, kazi nyingine ya Babu ni kukusanya kondom zinazotumika ama kutupwa hovyo kwenye eneo hilo.

Babu, anasema kwa kawaida anaokota kiasi ndoo tatu za kondomu zilizotumika. "Kazi yangu ni kuwalinda (wanaofanya ngono) dhidi ya vurugu zinazoweza kutokea, na kufanya usafi," anasema.


Hisani ya Nipashe, na itaendelea......
Aseee
 
Tumplekee habari hiyo Mbunge Faustine aende akafanye ukaguzi tena maana hawa polisi jamii hawaeleweki huenda ndio wateja wakuu pale maana biahsara hizo ni za majira ya jua likishazama na wao polisi ndio wako zamu.
 
Kazi ya Babu nyingine ni kuchukua shilingi elfu moja kwa kila mwanaume anayeingia kufanya ngono kwenye chumba ambacho kinawachukuwa watu ishirini ambao wanafanya ngono kwa wakati moja. Pesa anayoichukuwa Babu ni kwa ajili ya kuwalipa Polisi wa doria pindi wakipita kuchukuwa makusanyo as well kuwalipa polisi jamii.
Duuh
 
Back
Top Bottom