Dar yageuka `Sodoma` kwa ngono za wazi hadharani

Dar yageuka `Sodoma` kwa ngono za wazi hadharani

HALI HALISI
Mara ya kwanza ukifika eneo la Zakhem jirani na ukumbi maarufu wa burudani (
jinalinahifadhiwa), huwezi kufikiria kama eneo hilo nyakati ya usiku linageuka kuwa eneo lile la Sodoma na Gomora iliyosimuliwa kwenye vitabu vya dini. Eneo hilo lenye hali ya utulivu nyakati za mchana, kuanzia saa 1:00 usiku, hubadilika na kuwa danguro la aina yake linalofanana na ‘soko la wazi la ngono’, ambapo hali hiyo huendelea hadi nyakati za alfajiri.


Acheni kuficha uhalifu, ukumbi ni wa Dar Live. Hata siku moja sijawahi kuona magazeti ya Shigongo yanafanya ufukunyuku wa operation nini sijui pale.
[h=2]Ufuska waigeuza Dar `Sodoma` -2[/h]Vitendo vya ufuska vinavyoendelea katika eneo lililopo Mbagala Zakhem katika manispaa ya Temeke, ambalo ni maarufu kwa kuwavutia wanawake wengi na wanaume wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, vimekuwa tishio siyo tu kwa mazingira, bali pia maambukizi ya ukimwi na athari za madawa ya kulevya.

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa jeshi la polisi wilayani humo linajua yanayofanyika eneo hilo lakino hakuna hatua madhubuti ambazo zimechukuliwa kudhibiti vitendo hivyo haramu ambavyo pamoja na kutishia afya ya binadamu, pia inachafua taswira ya taifa letu ndani na nje ya nchi.

Isitoshe, hata viongozi wengine akiwamo mkuu wa wilaya ya Temeke, Siphia Mjema, inaonekana kushtushwa na taarifa za kuwapo kwa ufuska huo kiasi cha kudondosha machozi kwa kutoamini kwamba hali hiyo ipo katika eneo analosimamia kiutawala

UKIMWI NA DAWA ZA KULEVYA
Pamoja na kuwapo taarifa ya matumizi ya kondomu nyingi katika eneo hilo, miongoni mwa wanawake wanalalamikia vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wateja wao kuzipasua wakati wa kujamiiana.

Msichana mwenye umri wa miaka 20 (jina linahifadhiwa), anayejihusisha na biashara hiyo, anasema kupasuliwa kwa kondomu ni jambo la kawaida kuwatokea, na kwamba inapokuwa hivyo, wanashirikiana kumtoza mteja mhusika faini ya Shilingi 15,000.

Anasema vitendo hivyo vinahatarisha afya yao na kuwaweka katika hatari ya kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Pia msichana huyo anaitaja athari nyingine kuwa ni kondomu kupenya hadi sehemu ya siri, hivyo kusababisha kufanyiwa upasuaji.

"Pamoja na kukumbana na hatari hizo, hatuna la kufanya kwa sababu sisi tunatafuta pesa kwa ajili ya kuhudumia familia zetu," anasema.

Wanakitaja kituo cha afya cha Zakhem kuwa eneo muhimu kwao kwa ajili ya upasuaji wa kuondolewa kondomu zinazonasa, huku wakitozwa fedha nyingi.

Pamoja na hayo, ilibainika kuwa sehemu kubwa ya wahusika wa biashara hiyo ni watumiaji wa dawa za kulevya.

MKUU WA WILAYA AANGUA KILIO
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, alipofuatwa ofisini kwake na kuelezwa uwapo wa soko hilo, aliangua kilio.

Mjema alijikuta akilia baada ya kutoamini taarifa aliyotakiwa kuitolea ufafanuzi, akisema kinaweza kuaminika kwa haraka kama kimeonekana katika picha za mnato na si eneo la utawala wake.

“Jambo hili limenishtua kiasi kikubwa, ni hali ya unyama unaotendeka, haiwezekani binadamu na akili zao wakafanya vitendo hivyo hadharani," alisema na kuanza kuangua kilio.

Alisema hana taarifa kuhusiana na kuwapo kwa biashara haramu hiyo, hivyo atafuatilia na kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.

"Kinachoniumiza kuona vijana hawa wanaangamia huku wenyewe wakijiona, ikiwa leo mtoto anahusika na mambo hayo hali ya baadaye itakuwaje, natahakikisha vitendo hivi vinakoma mara moja," anasema.

RPC: NINAFAHAMU, NIMEONA
Hata hivyo, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo, anathibitisha kulifahamu eneo hilo na biashara ya ngono inayofanyika hapo.

Alisema, mkakati wa kuidhibiti biashara haramu hiyo unaandaliwa kwa vile matumizi ya nguvu peke yake hayawezi kuleta suluhu ya kudumu.

"Suala la dadapoa linatakiwa kutumia akili na elimu zaidi, ukitumia nguvu lazima utashindwa kwa sababu sheria ya nchi haielezi chochote," alisema Kiondo.

Hata hivyo alisema anakerwa kwa kile kinachofanyika katika eneo hilo kwani inadhalilisha na kuondoa utu wa mtu.
 
Ukiishi kwa kufuata sheria ya Mungu haya yote itayaona ni ubatili mtupu...
 
Hao wanawake wanafanya ngono na nani? Wenyewe kwa wenyewe? Mbona wanaume hatuwaoni hapa!!!
attachment.php

Unaweza usiamini lakini ndivyo hali ilivyo katika eneo moja jijini Dar es Salaam, ambalo limegeuzwa kuwa soko la wazi la kufanyia vitendo vya ngono hadharani. Eneo hilo lililopo Mbagala Zakhem katika manispaa ya Temeke, limekuwa maarufu na kuwavutia wanawake wengi na wanaume wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.


Jeshi la polisi limethibitisha kuwa na taarifa za kuwapo kwa eneo hilo na kufanyika kwa biashara ya ngono hadharani. Kamanda wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo anasema, “ninalijua eneo hilo na biashara haramu inayofanyika, tunajipanga kupata namna bora ya kuidhibiti.”

Vitendo hivyo viovu vimekuwa vikifanywa nyakati za usiku. Kutokana na uwepo wa hali hiyo, eneo hilo limekuwa na mlundikano wa mipira ya kiume (kondom) na kusababisha afya za watu hasa watoto kuwa hatarini, huku mazingira yakizidi kuchafuka. Uchunguzi umebaini wanawake wanaofanya biashara hiyo hutembea na wanaume kufikia zaidi ya 10 kwa siku.

HALI HALISI
Mara ya kwanza ukifika eneo la Zakhem jirani na ukumbi maarufu wa burudani (jina linahifadhiwa), huwezi kufikiria kama eneo hilo nyakati ya usiku linageuka kuwa eneo lile la Sodoma na Gomora iliyosimuliwa kwenye vitabu vya dini. Eneo hilo lenye hali ya utulivu nyakati za mchana, kuanzia saa 1:00 usiku, hubadilika na kuwa danguro la aina yake linalofanana na ‘soko la wazi la ngono’, ambapo hali hiyo huendelea hadi nyakati za alfajiri.

Ndani ya ‘soko’ hilo lenye idadi kubwa ya wanawake wanauza miili yao maarufu kama changudoa ama dada poa, hakuna utaratibu wa kufanya vitendo hivyo katika faragha, badala yake inafanyika kwenye maeneo ya wazi. Vitendo hivyo vinapofanyika, vinashuhudiwa na watu waliopo maeneo ya karibu, wengine wakisubiri zamu zao kutoka kwa mwanamke mhusika.

Wakati hali ikiwa hivyo, wanaume waliogundulika kufika kwenye maeneo hayo ni wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 50, wakiwa wenye hadhi na nyadhifa tofauti. Gharama iliyobainika kutozwa kwa kila tendo la ngono linapofanyika mara moja, ni Shilingi 3,000.

Eneo hilo linazungukwa na vibanda vya mama lishe, likiwa na ukubwa takribani mita 25. Mmoja wa wanawake wanaofanya biashara hiyo (jina linahifadhiwa), anasema yupo na wenzake zaidi ya 30 na wana uwezo wa kuwahudumia wanaume kati ya 100 hadi 300.

"Hapa kila mtu anapata fedha kulingana na nguvu yake, sasa ukitafuta chumba utapoteza muda ni bora tuwahudumie hapa kwenye eneo la wazi huku wengine wakitusubiri," anasema mwanamke huyo. Hata hivyo, alisema kwa upande wake, usiku huo alikuwa amekutana na wanaume 25 na kufanikiwa kujikusanyia Shilingi 50,000.

Alisema wateja wao wameshazoea kufanya ngono kwenye eneo la wazi. "Si unaona watu wote wale wanasubiri wenzao wamalize, ni vyema wakaangalia, wanapoona mwenzao amemaliza yeye aingie," aliongeza kusema huku akionyesha kundi la watu zaidi ya 20 wakiwa pembeni wakisubiri.

BABU AONGOZA
Kwenye eneo hilo kuna kiongozi wao ambaye anafahamika kwa jina moja la Babu, yeye ndiye mwenye mamlaka ya ulinzi na kutoza faini kwa anayekiuka taratibu walizojiwekea. Hata hivyo, kazi nyingine ya Babu ni kukusanya kondom zinazotumika ama kutupwa hovyo kwenye eneo hilo.

Babu, anasema kwa kawaida anaokota kiasi ndoo tatu za kondomu zilizotumika. "Kazi yangu ni kuwalinda (wanaofa
nya ngono) dhidi ya vurugu zinazoweza kutokea, na kufanya usafi,” anasema.

Hisani ya Nipashe, na itaendelea......
 
Hao wanawake wanafanya ngono na nani? Wenyewe kwa wenyewe? Mbona wanaume hatuwaoni hapa!!!

Afadhali wewe umeliona hili, maana hawa wafanya ufuska wasingeweka maskani hapo kama kusingekuwa na wateja. Katika miji kadhaa nchini Marekani kulikuwa na tatizo kama hilo la makahaba na ilikuwa vigumu kuvunja ngome zao. Polisi walichofanya ni kuajiri wanawake kadhaa wanaoonekana kuwa na mvuto na mtazamo kama wa kikahaba vile, wakawa wanapozi huku wakiwarembulia wanaume wakati wameficha vinasa sauti ambavyo vilirusha mawimbi ya sauti hadi mafichoni kwa polisi. Kwa nia hii walishikwa wanaume wengi na kutiwa ndani. Kwa njia hii biashara haramu ilikoma kwa vile hakuna mwanaume aliyekuwa tayari kuumbuka.

Ninachoshangaa Tanzania wanashikwa wanawake tu bila wanaume wanaowanunua hao wanawake. Nimepita mara kadhaa mitaa ya huko Kinondoni panakera, Buguruni nako majira ya jioni utaona wasichana ndio kumekucha wanaingia kazini, katikati ya jiji karibu na mahoteli nako wanaojipitishapitisha ni kwa wingi tu, lakini wanaoonwa ni hao wasichana si wanaume wanaowazungukia kuwarubuni.

Kuna watu wanaofanya biashara hiyo ishamiri, mbona mie sijawahi kutongozwa na hao machangu ilipotokea kupita maeneo hayo? Wanaangalia mtu mwenye pepo la ngono, na zaidi wana wateja wao si kila kiruka njia.
 
kasheshe...
sodoma na gomora kabisa. Mungu atunusuru.
 
Nasikia wakati mwingine hata askari wanaowakamata wanaomba rushwa ya ngono. Kwa mtindo huu biashara hii haitaisha. Wakifanya ulichoandika hapa kwa kweli hii biashara itaisha. Biashara yeyote hutegema wateja, wasipokuwepo hakuna biashara itakufa tu!!! It is high time serikali ikabadili tactics ili kuua hii biashara for good!!!
Afadhali wewe umeliona hili, maana hawa wafanya ufuska wasingeweka maskani hapo kama kusingekuwa na wateja. Katika miji kadhaa nchini Marekani kulikuwa na tatizo kama hilo la makahaba na ilikuwa vigumu kuvunja ngome zao. Polisi walichofanya ni kuajiri wanawake kadhaa wanaoonekana kuwa na mvuto na mtazamo kama wa kikahaba vile, wakawa wanapozi huku wakiwarembulia wanaume wakati wameficha vinasa sauti ambavyo vilirusha mawimbi ya sauti hadi mafichoni kwa polisi. Kwa nia hii walishikwa wanaume wengi na kutiwa ndani. Kwa njia hii biashara haramu ilikoma kwa vile hakuna mwanaume aliyekuwa tayari kuumbuka.

Ninachoshangaa Tanzania wanashikwa wanawake tu bila wanaume wanaowanunua hao wanawake. Nimepita mara kadhaa mitaa ya huko Kinondoni panakera, Buguruni nako majira ya jioni utaona wasichana ndio kumekucha wanaingia kazini, katikati ya jiji karibu na mahoteli nako wanaojipitishapitisha ni kwa wingi tu, lakini wanaoonwa ni hao wasichana si wanaume wanaowazungukia kuwarubuni.

Kuna watu wanaofanya biashara hiyo ishamiri, mbona mie sijawahi kutongozwa na hao machangu ilipotokea kupita maeneo hayo? Wanaangalia mtu mwenye pepo la ngono, na zaidi wana wateja wao si kila kiruka njia.
 
Hizi ni Picha nilizopiga jana mchana nilipotembelea eneo hilo. Ni jambo la kusikitisha na linachafua sura ya eneo la Mbagala.

Muheshimiwa huku kibada kwenye mradi wa viwanja elfu 20 tunavuwa kambale na papa njoo ushuhudie, haswa upande wa shangwe kushoto kama unatoka mji mwema. Hivi serikali ilifanya due diligence wakati wa upimaji wa hivi viwanja? na ukizingatia haya yalikuwa ni mabonde ya mpunga hapo zamani?
 
Kazi ya Babu nyingine ni kuchukua shilingi elfu moja kwa kila mwanaume anayeingia kufanya ngono kwenye chumba ambacho kinawachukuwa watu ishirini ambao wanafanya ngono kwa wakati moja. Pesa anayoichukuwa Babu ni kwa ajili ya kuwalipa Polisi wa doria pindi wakipita kuchukuwa makusanyo as well kuwalipa polisi jamii.

Du! Hapa ndio patamu. Hebu rudia tena mkuu.
 
Mgambo wanapatikana nchi ipi tena?

Haya ndiyo mambo ya mitandao? George Orwell's 1984? It seems.

Posting ya kwanza haikuwa na picha za wanamgambo bali mji uliojengeka na mandhari mazuri kabisa. Sasa wamewekwa hao wanamgambo.
 
Ama! Ina maana hata mchana wanauza? Kwa kweli dunia imekwisha!

Washikwe wanaume wanaoenda kwa hao machangu, naona hawa akina mama wanaonewa, labda polisi wenyewe ndio wateja wao wakubwa.
 
Khaa!! Kwani kuna shida gani?? Acheni pesa ifanye mzunguko. Mnajilipa laki3 kwa siku hawa waende wapi?? Ala!!
 
Khaa!! Kwani kuna shida gani?? Acheni pesa ifanye mzunguko. Mnajilipa laki3 kwa siku hawa waende wapi?? Ala!!
Tatizo humjui mkweli na aliyeathirika naamini sio wote wanatumia Condom kwani ukipanda dau la nyama kwa myama au kuichana condom Bint hatabisha ila ni Mshiko wake tu atapokea
Candid Scope Asante sana kwa taarifa, maana imetufungua sana na kuanza kuogopa
huku Dodoma, mtaani kwetu kuna kina Dada wawili (mmoja ameathirika) walitoka huku mtaani na kuacha watoto wawili kila mmoja kuja Mbagala Zakheem kutafuta kazi, yule mwenye ugonjwa karudi huku Dodoma na juzi 12/04/2014 nimemtafuta na leo amekiri huwa ndio kazi yao hiyo hapo Mbagala. Sasa hivi nimempigia huyo mwenzake kuwa habari hizi zimewafichua nimeambulia matusi (KWA HIYO NI KWELI HAJAAJIRIWA HOTELINI Zakheem Mbagala)
Kweli ni uchungu acheni huyo Mkuu wa Wilaya alie kwani huyu Bint ana mtoto wa kike form 2 amesimamishwa na wa kiume STD 7
Binti ukimuona hutamkataa ana asili ya Kisomali na kitutsi, Baba yake ni dreva wa malori huko Rwanda - TZ
siwezi mtaja zaidi kwa simu wala jina lakini taarifa hii imesaidia sana, inepelekwa kwenye Vyombo vya habari hasa magazeti kwani wanaambukizana mwenzao huku anahesaabu siku kasikitika na kufurahi
  1. hela wanaoyapata haitoshelezi mahitaji yoyote hata kuitunza familia.
  2. Wapo wanaume wanaolazimisha bila Condom
  3. bila Serikali hawataacha kwani hela ya chakula hawana
 
Chukua changu wako peleka guest ya heshma kula hadi uingie chumvini hakuna atakae kubughudhi.

Guest hawataka mkuu, wanataka chapchap ndipo wanapiga hela ndefu. Umeona eeh?
 
Back
Top Bottom