Daraja jipya la Selander lakamilika, Kufunguliwa Desemba 27, 2021

MrRight

New Member
Joined
Dec 20, 2017
Posts
4
Reaction score
21
Kampuni ya kikorea GS E& C wamemaliza ujenzi wa Daraja jipya la Selander ..mradi huu mkubwa utafunguliwa tarehe 27 Dec 2021.

Hii ni hatua njema ya ukamilishaji wa miradi yetu kama ilivyo kwenye Ilani ya ccm ya mwaka 2020-2025.

Daraja hili lina urefu wa mita 670 Ni aina mpya ya daraja ambayo imechanganya sifa za daraja la mhimili na daraja lililokaa kwa kebo ili kuifanya iwe nyepesi. Mbinu hiyo huongeza uwezekano wa ujenzi na kiuchumi, kulingana na mjenzi.

Mradi huu ulikuwa sehemu ya mradi wa Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea Kusini, ambao ulitoa dola milioni 107 kwa ujenzi huo.

 
DARAJA LA

SURRENDER

SELANDER

SALENDAR
 
... hela iliyotupwa hapo ingetosha kupanua barabara ya Mwenge hadi Posta Mpya njia nne kila upande; ingetosha kupanua barabara ya Morogoro toka Kimara hadi Posta Mpya njia nne tukasahau foleni completely. Mradi wa Daraja la Selander hautamaliza tatizo lililokuwepo kwa kiwango kikubwa!
 
Wangepanua hizo barabara bado ungesema wangejenga flyover makutano ya kawawa road njia nne, jifunzeni kupongeza pia
 
Lile limejengwa special kwa madon wa Oysterbay, Mikocheni, Masaki, Msasani na Kawe.
Nyie walalahoi mtapita barabara ya UN
 
Ni mradi wa urembo zaidi na sio kutatua tatizo la foleni.
 
Mkuu,ingetosha kuweka daraja pale Jangwani ili mvua zikinyesha maisha yaendelee bila shida,Ingetosha na chenchi kubaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…