Daraja kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo limefungwa

Kindeena

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2017
Posts
11,462
Reaction score
21,124
1702069013976.jpg

Daraja la Mto Mpiji ambalo lipo mpakani na linalounganisha Wilaya ya Bagamoyo na Mkoa wa Dar es salaam limefungwa kutumiwa na Waendesha magari na vyombo vingine vya usafiri baada ya sehemu ya daraja hilo kutitia na kupelekea uwepo wa shimo kubwa ambalo linahatarisha usalama wa Watu.

Kwa sasa wanaoruhusiwa kupita kwenye daraja hili ni Watembea kwa miguu pekee na kama una gari lako au usafiri mwingine utalazimika kuuacha upande wa pili na kupita hapa kwa miguu.

Tayari Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama vipo hapa darajani ili kuimairisha ulinzi na usalama.

AyoTV ipo eneo la tukio kuendelea kukufahamisha yote yatakayojiri. #MillardAyoUPDATES
 
Daah wenzetu Majerumani ukienda hapo Humburg wana madaraja yametengenezwa miaka 1400 iliyopita na bado yanatumika na wanawaenzi Wasomi wao kwa kuweka sanamu zao sisi daraja la juzi tuu limefungwa Vima kweli...
 
Salender Bridge mpaka leo ipo tu

Ujenzi ukijengwa na mtanzania kuhusu uimara sahau,ikitokea jambo
Kisingizio wanacho cha mvua

Na sahvi zile daraja na barabara walizojenga kiupigaji na utapeli
Zote zinaumbukaa kutokana na mambo ya mvua

Ova
 
Ujenzi wao huwa hautegemei Mvua ikinyesha kidogo unaona makosa Nchi ngumu sana hii...
 
Naanza kupata wasiwasi na pale wami, tanzanite bridge, hata haya madaraja wanaita flyover napata wasiwasi nayo.YALIJENGWA KWA SIFA ZA KIJINGA ENZI ZA MFUGALE NA MAGUFULI. Sasa je, yatatoboa hata miaka 15? Hata barabara za kipindi hicho ni mashimo tupu.
 
Mkuu, Tanzanite, Mfugale zimejengwa haswaaaa.

Weka siasa na mapenzi kando, sahau maumivu uliyopitia!

Hakuna awamu yoyote ile iliyojengwa barabara nyingi(kwa urefu) na mbovu kama ya MPIGAJI MKUU wa taifa na genge lake; nadhani ndo awamu unayoipenda hata wewe!
 
Daah wenzetu Majerumani ukienda hapo Humburg wana madaraja yametengenezwa miaka 1400 iliyopita na bado yanatumika na wanawaenzi Wasomi wao kwa kuweka sanamu zao sisi daraja la juzi tuu limefungwa Vima kweli...
Ukisema hivyo watadai unajidai, wakati ni ukweli usiopingika. Watakusema wajifanya mjuaji na kujigamba umefika Germany...
 
Mara nyingi natoa mifano ya Afrika kama Chirundu bridge lililotengenezwa na wakina Dr Livingstone au Beit Bridge la SA huko German wana vitu imara sana aisee hawatengenezi kwa ajili ya leo wanatengeneza kwa ajili ya vizazi vijavyo sijui pirate au kwenye miji midogo kama happy city utabaki kushangaa tuu wakati sisu tuna miji mikubwa ila ni style ya hovyo hovyo tuu..
 
Mkandarasi aliyejenga hapo awajibike hata kama imepita miaka 5, sheria zetu baadhi ni mbovu sana mkandarasi anapojenga kitu kama daraja hupaswa kuiguarantee serekali "" life time of bridge"" miaka 50-100. Wenzetu ngambo hufanya hivyo!
 
Mara nyingi natoa mifano ya Afrika kama Chirundu bridge lililotengenezwa na wakina Dr Livingstone au Beit Bridge la SA huko German wana vitu imara sana aisee hawatengenezi kwa ajili ya leo wanatengeneza kwa ajili ya vizazi vijavyo sijui pirate au kwenye miji midogo kama happy city utabaki kushangaa tuu wakati sisu tuna miji mikubwa ila ni style ya hovyo hovyo tuu..
Tanzania mainjinia ni tia maji tia maji,Kuna rafiki yangu alikuwa anasoma ATC,alinisimulia tukio moja hapo ATC kwenye bweni lao.Uongozi wa chuo ulifanya maamuzi ya kubadili sakafu kwenye bweni ambalo lilijengwa na wajerumani,Mwisho ilikuwa vichekesho yaani ni bandika bandua, bandika bandua.

Licha ya chuo kuwa na mainjia kibao wa kibongo lakini walishindwa kuweka sakafu yenye ubora kama ya mjerumani,ikawa wakija kukagua wanaona wapi.Bongo bado sana.
 
Salender Bridge mpaka leo ipo tu

Ujenzi ukijengwa na mtanzania kuhusu uimara sahau,ikitokea jambo
Kisingizio wanacho cha mvua

Na sahvi zile daraja na barabara walizojenga kiupigaji na utapeli
Zote zinaumbukaa kutokana na mambo ya mvua

Ova
Tena salender ndio kabisa, zinanyesha el Nino na bado mzigo unadunda japo wa zama za mawe za kati huko

Ila sasa hawa wenzetu wa karne ya 21 sijui wanafeli wapi?😂
 
Tanzania mainjinia ni tia maji tia maji,Kuna rafiki yangu alikuwa anasoma ATC,alinisimulia tukio moja hapo ATC kwenye bweni lao.Uongozi wa chuo ulifanya maamuzi ya kubadili sakafu kwenye bweni ambalo lilijengwa na wajerumani,Mwisho ilikuwa vichekesho yaani ni bandika bandua, bandika bandua.

Licha ya chuo kuwa na mainjia kibao wa kibongo lakini walishindwa kuweka sakafu yenye ubora kama ya mjerumani,ikawa wakija kukagua wanaona wapi.Bongo bado sana.
Na hili ndio tatizo unakuta Chuo kinatoa Mainjia wa mambo mengi unakuta hapo hapo Chuoni nao wanahangaika na mgao wa umeme au kukatika kwa maji wakati wao ilitakiwa wawe mfano aisee..
 
Back
Top Bottom