Daraja kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo limefungwa

Daraja kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo limefungwa

Hapo daraja lilijengwa kutozingatia ukubwa wa pressure ya maji endapo ikitokea mvua kubwa...

Bila shaka udongo wa chini umetembea, ukadisturb egemeo la daraja upande linapokutana na ardhi...
 
Ma engineer wa bongo wanachoweza kufanya kwa usahihi ni kubandika mabango ya "nani kama mama" lakini kazi zingine tukiri wazi tuu kua wameshindwa kwa asilimia zote, kazi wapewe wachina tuu barabara na madaraja waliyo tengeneza hao waswahili ni uchafu na vichekesho kabisa
 
Sijui kingo au miguu ya nguzo ilivyojengwa...

Baada ya kufatilia naona wenye daraja wanasema chanzo ni moja ya nguzo imetitia, hivyo daraja likanepa...
Meku huo mto ni mpana sana wao walijenga daraja jembamba kupitisha pikipiki zinazobeba mkaa....hilo daraja lilipaswa liwe pana pia libebe nguzo kubwa ambazo zinamuda maji yenye kasi yeyote
 
Naanza kupata wasiwasi na pale wami, tanzanite bridge, hata haya madaraja wanaita flyover napata wasiwasi nayo.YALIJENGWA KWA SIFA ZA KIJINGA ENZI ZA MFUGALE NA MAGUFULI. Sasa je, yatatoboa hata miaka 15? Hata barabara za kipindi hicho ni mashimo tupu.
Hacha chuki za kijinga upo kwenu huko mbwinde hukute ata hilo Daraja kajenga MFUGALE HAUJAWAI PITA,Kwa taharifa yako lile daraja ni chuma cha Pua juzi kati Semi la Mafuta limepiga kingo zake likiwa kwenye Speed 80 na bado likabaki strong.
 
Naanza kupata wasiwasi na pale wami, tanzanite bridge, hata haya madaraja wanaita flyover napata wasiwasi nayo.YALIJENGWA KWA SIFA ZA KIJINGA ENZI ZA MFUGALE NA MAGUFULI. Sasa je, yatatoboa hata miaka 15? Hata barabara za kipindi hicho ni mashimo tupu.
Ujinga ni tatizo kubwa sana.
 
Salender Bridge mpaka leo ipo tu

Ujenzi ukijengwa na mtanzania kuhusu uimara sahau,ikitokea jambo
Kisingizio wanacho cha mvua

Na sahvi zile daraja na barabara walizojenga kiupigaji na utapeli
Zote zinaumbukaa kutokana na mambo ya mvua

Ova
Siku lidondoke lile la Kijazi
 
Limeshaanza kupitika upande mmoja,mabasi,malori,magari,madogo,Bajaj,pikipiki,guta,baiskeli,matorori,waenda kwa miguu na wanyama wote kwa Sasa wanapita na ukarabati unaendelea kwa kasi.
 
Salender Bridge mpaka leo ipo tu

Ujenzi ukijengwa na mtanzania kuhusu uimara sahau,ikitokea jambo
Kisingizio wanacho cha mvua

Na sahvi zile daraja na barabara walizojenga kiupigaji na utapeli
Zote zinaumbukaa kutokana na mambo ya mvua

Ova
It was first constructed in 1929 and is named after John Einar Selander , Tanganyika's first Director of Public Works.
 
Mfugale, Kijazi, Tanzanite yako strong kaka.
Nadhani wanafeli katika kupima ardhi na miamba ardhini ili kusimika nguzo kufika kwenye tabaka husika ili zihimili mitetemo, na uzito upitao,study za mikondo ya maji na rekodi zake, nature ya eneo, yote haya ni ya msingi mno kwa engineer kufahamu hasa activities za nature ya eneo!.
 
Mkandarasi aliyejenga hapo awajibike hata kama imepita miaka 5, sheria zetu baadhi ni mbovu sana mkandarasi anapojenga kitu kama daraja hupaswa kuiguarantee serekali "" life time of bridge"" miaka 50-100. Wenzetu ngambo hufanya hivyo!
Inategemea, Saa nyingine design aikufanyika vizuri. Hii pia inatokana pia kama investigation to know the underlying materials ilifanyika na mtu anayejua. Hiyo sehemu kama sikosei underlying material is alluvial soil which normally is very soft or very loose and require friction piles to go a bit deeper depth to support the bridge. Sasa kama hayo hayakufanyika na watu wanaojua basi kunaweza kukatokea settlement ya daraja na uharibifu mwingine.
 
Tanzania mainjinia ni tia maji tia maji,Kuna rafiki yangu alikuwa anasoma ATC,alinisimulia tukio moja hapo ATC kwenye bweni lao.Uongozi wa chuo ulifanya maamuzi ya kubadili sakafu kwenye bweni ambalo lilijengwa na wajerumani,Mwisho ilikuwa vichekesho yaani ni bandika bandua, bandika bandua.

Licha ya chuo kuwa na mainjia kibao wa kibongo lakini walishindwa kuweka sakafu yenye ubora kama ya mjerumani,ikawa wakija kukagua wanaona wapi.Bongo bado sana.
ATC lile bweni la wasichana jipya lililojengwa na wabongo lina rangi kama njano ni bovu lina tap chache za maji zinazofanya kazi wanafunzi wanapiga foleni kuoga asubuhi.
 
View attachment 2837070

Daraja la Mto Mpiji ambalo lipo mpakani na linalounganisha Wilaya ya Bagamoyo na Mkoa wa Dar es salaam limefungwa kutumiwa na Waendesha magari na vyombo vingine vya usafiri baada ya sehemu ya daraja hilo kutitia na kupelekea uwepo wa shimo kubwa ambalo linahatarisha usalama wa Watu.

Kwa sasa wanaoruhusiwa kupita kwenye daraja hili ni Watembea kwa miguu pekee na kama una gari lako au usafiri mwingine utalazimika kuuacha upande wa pili na kupita hapa kwa miguu.

Tayari Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama vipo hapa darajani ili kuimairisha ulinzi na usalama.

AyoTV ipo eneo la tukio kuendelea kukufahamisha yote yatakayojiri. #MillardAyoUPDATES


Kamateni mkandarasi huyo na weka ndani miaka 10 na itangazwe kila wiki kuwa aliibia serikali kwa kujenga daraja chini ya kiwango
 
Back
Top Bottom