Daraja la Tanzanite kufungwa kuangalizia fainali UEFA, Serikali iko wapi?

Daraja la Tanzanite kufungwa kuangalizia fainali UEFA, Serikali iko wapi?

Hili suala la kufunga daraja kwa ajili ya mechi ya UEFA limekaaje kitaalam mbona kama haliko sawa hivi.

Serikali iko wapi maana hili sio la kufumbia macho.

Huduma muhimu zinasitishwa kwa ajili ya anasa.

Je? daraja lilijengwa ili iwe ni sehemu ya kuangalizia mpira.
View attachment 2242047
Mkuu
Kama una pesa yako ni ruksa kulipia na kufunga barabara ambayo ikifungwa haitaleta athali kwa watumia road
 
Ajira za muda ni ngapi zimetengenezwa kama kuuza vyakula? mambo ya usafiri kama bajaj na bodaboda na wale wa little ride au bolt!
Nimefika hapo, hakuna mlalahoi anayeruhusiwa kuingia tofauti na walivyotangaza! Watu wengi wamesimama round bout kwakuwa hawana kadi ambazo hawakusema kama zinauzwa au la! Sasa hizo ajira za muda mfupi ni zipi?

Wanaoruhusiwa kuingia, kila mmoja kafika na ndinga lake, sasa hizo bolt, bajaj na zifananazo zitambeba nani?
 
Sio lazima wainge, acha ushamba wa Mbagala
Nyie mnashadadi mipira ya wenzenu waliokaa chini na kutumia akili kitengeneza product ambayo mnaitamani.

Baadaya ya nyie mtumikishe mayele yenu kazi kupiga porojo tuu....tungekuwa na akili mechi ya simba na yanga ndio ingekuwa inaatizamwa apo tanzanite beidge huku game likiwa linapogwa ccm kiruma usiku kwenye pirch kali na mataa yanawaka...tukitumia gesi yetu ya mtwara. Hizo ndio akili.
 
Swali la kujiuliza ni kuwa uzito ukielemea sehemu Moja kwa muda mrefu je haitaleta madhara maana sio baada ya hapo mara daraja lina ufa au mkaja kutumbukia baharini mkaangalie UEFA na samaki
Pitia hapo dukani kwa mangi faster uagizie chochote ntapita hapo baadaye na range yangu autobiography 2022 kulipia.
 
Sioni tatizo hilo daraja kutumika kuonyesha hiyo mechi kwa sababu daraja lenyewe linatumika na wachache mno. Pia kuna option ya kupita Ali Hasan Mwinyi kirahisi tu. Kama ulinzi ni wa kutosha sioni tatizo lolote kwenye huo ubunifu.
 
Back
Top Bottom