Daraja la Tanzanite upotevu mkubwa wa pesa ambazo zingetumika kuimarisha sekta ya afya tungeokoa maisha ya akina mama wengi vijijini

Daraja la Tanzanite upotevu mkubwa wa pesa ambazo zingetumika kuimarisha sekta ya afya tungeokoa maisha ya akina mama wengi vijijini

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Unajenga daraja la bil 243 ili kurahisisha usafiri wa viongozi wa CCm kwenda kwao huko Osyterbay na masaki huku ukisahau kuwa kuna sekta ya afya ambayo bado ipo nyuma kabisa.

Vituo vingi vya afya havina vifaa tiba na watumishi. Ni majengo tu ambayo yanafugia popo. Na hata raia wengi vijijini wanatembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya. Sasa tungejenga kituo cha afya cha Bil mbili kwa hiyo Bil 243 tungepata vito vya afya kibao.

Hili daraja ni kwa ajili ya vibosile wa CCM ili wapate shortcut kufika Masaki na Oysterbay kwa urahisi. Hii ni Nonsense kabisa.
 
Nchi haina vipaumbele, walipa kodi awashirikishwi juu ya matumizi ya kodi zao.

Matrekta ni muhimu kuliko ndege na yanazalisha uchumi mkubwa kuliko ndege ,yanarudisha pesa haraka kuliko ndege.

Soko kubwa lipo China lima, peleka chochote kule.

Kutwa kuwalaumu wazungu juu ya kushindwa kwetu, wakati wanasiasa ndio chanzo.
 
Unajenga daraja la bil 243 ili kurahisisha usafiri wa viongozi wa CCm kwenda kwao huko Osyterbay na masaki huku ukisahau kuwa kuna sekta ya afya ambayo bado ipo nyuma kabisa...
Au, hizo hela tunge wapa wauza vitumbua - kusudi kila familia ipate angalau vitumbua vya kuywea chai kila siku! Je! Ni siku ngapi kila familia nge kuwa na mlo huo? Serikali inapoteza hela kwenye miundo mbinu isiyo ya lazima!
 
Tambua kuwa Masaki na Oysterbay ni maeneo ambayo ni makazi ya mabalozi, makazi ya MaCEO wa makampuni makubwa, kuna mahoteli makubwa...wanakaa think tanks wengi wa nchi hii....hawa ni watu muhimu ambao muda wao lazima uzingatiwe maana pia mchango wao kwa maendeleo ya Taifa hili ni mkubwa...
 
Nchi haina vipaumbele, walipa kodi awashirikishwi juu ya matumizi ya kodi zao.
Matrekta ni muhimu kuliko ndege na yanazalisha uchumi mkubwa kuliko ndege ,yanarudisha pesa haraka kuliko ndege.
Soko kubwa lipo China lima, peleka chochote kule.
Kutwa kuwalaumu wazungu juu ya kushindwa kwetu, wakati wanasiasa ndio chanzo.
Ni vijiji vingapi ambavyo vina zile trekta za kila kijiji zinazofanya kazi mpaka sasa?
 
Ni vijiji vingapi ambavyo vina zile trekta za kila kijiji zinazofanya kazi mpaka sasa?
Zilishakufa Hizo trekta zilinunuliwa ujazaliwa bado, zinatakiwa mpya zingine.

Serikali inatoa ruzuku mfano bilioni 400 kwenye viwanda vya matrekta wanayatengeza yanakuja uzwa kwa nusu bei mfano nyingi nchini hp 50 ni milioni 30 hadi 40 so watz wanauziwa milioni 10 au 12 umiliki binafsi.
 
Nchi haziendeshwi hivyo, huwezi kuacha kufanya miradi ya miundombinu kisa hujamaliza mambo ya afya. Lile daraja ni uwekezaji, utarudisha fedha zitakazonunua hizo dawa.
 
Wazo lako ni zuri sana ila acha kuingiza uchama kwenye maendeleo off course pia hata kwenye maji wangeweza peleka huko vijijini

Lile Daraja naimani IPO siku utapita wewe ama ndugu Yako.
Maji vijijini kote huko while dar hapa hapa mpaka leo miaka 60 ya uhuru hakuna maji safi ya uhakika maeneo kibao
 
Unajenga daraja la bil 243 ili kurahisisha usafiri wa viongozi wa CCm kwenda kwao huko Osyterbay na masaki huku ukisahau kuwa kuna sekta ya afya ambayo bado ipo nyuma kabisa...
Huko ndiko wanaishi wawekezaji tusipopajali wataondoka na tutakosa kodi, name madawa ya kuhudumia wajawazito yanayokana na kodi
 
Back
Top Bottom