Darasa la saba waanza Mitihani

Darasa la saba waanza Mitihani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
JUMLA ya wanafunzi 1,132,143 wa darasa la saba waliosajiliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), leo na kesho watafanya mitihani ya taifa ya kuhitimu elimu ya msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mitihani hiyo Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema maandalizi yamekamilika na mitihani imeshazambazwa kwenye vituo.

“Watahiniwa 1,132,143 wamesajiliwa kufanya mtihani mwaka 2021, kati ya hao 1,079,943 sawa na asilimia 95.39 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na 52,200 sawa na asilimia 4.61 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia,” alisema Dk Msonde.

Alisema katika mtihani huo idadi ya masomo itakayotahiniwa imeongezeka kutoka masomo matano ya mwaka jana na kuwa sita na hiyo ni kwa mujibu wa mtaala mpya ambao ulianza kutumika wanafunzi hao wakiwa darasa la kwanza.

Somo lililoongezeka linaitwa uraia na maadili ikiwa ni sehemu ya maboresho ya masomo na kwamba masomo mawili yameboreshwa maudhui yake ambayo ni sayansi ambalo sasa linaitwa sayansi na teknolojia na maarifa ambalo sasa linaitwa maarifa ya jamii na stadi za kazi.
 
Bavicha , ambayo ni Taasisi bora ya vijana barani Afrika, imetuma salamu za heri na fanaka kwa vijana wa Darasa la 7 nchi nzima wanaoanza mitihani ya kumaliza elimu ya msingi leo .

Ujumbe : HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA
Erythrocyte n Mjumbe wa kamat kuu Bavicha nini
 
Ila hao maafisa wa elimu wanao pita pita mashuleni kuangalia ufanyikaji wa mitihani hiyo wajizuie kwenda na magari yao wakati watoto wakiwa ndani ya vyumba vya mitihani kwani watoto hao wanaweza kutoka nduki wakidhani wanataka kuwachanja Chanjo ya COVID 19.Ni mtizamo tu.
 
Kila la khery,
Ila katika milioni moja ni 52,000 tu wa kiinglish?
Hongera sana
 
Huu muziki una impact mwezi January

Tozo zitahusika hapa, watu watalia-lia humu na wa kuwasaidia atakuwa hayupo

What goes around bhana!

Ngoja uone mazee!!
 
Tupo nyuma yao wasikonde atakae fail kazi za ulinzi zipo kibao sisi wajomba zao tutawapokea
 
Leo Wanafunzi 1.1million wa Shule za Misingi Wanafanya Mitihani yao ya Kumaliza Elimu ya Msingi.

Kati ya Hao Wanafunzi 500,000 Wanatarajiwa kuchaguliwa Kuendelea na Masomo ya SEKONDARI.Je Wanafunzi Waliobaki yaani 600,000 mini HATIMA yao?

Je SERIKALI ina Mipango gani kwa Hao Wanafunzi?
Au Mzigo ni WA WAZAZI husika?
Au Ndio MACHINGA,BODABODA na WAPIGA DEBE kwenye STENDI za MABASI?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
1.1 milioni????? Mbonaidadi kubwa sanaa nisawa na population ya nchi Fulani kabisa😂
 
Hii spidi za kuzaana Kama mbwa hatutakaa tusonge mbele… 4 years back shule za kata zilizidi kuwa nyingi kuliko idadi ya wanaohitajika Leo itabidi tuongeze hizo shule zaidi ya zilizopo!

Serikali itakua inacheza kushoto kulia kila siku kazi ipo!

Watanzania wanazaliana Kama mchwa maendeleo itakua ni ndoto!
 
Leo Wanafunzi 1.1million wa Shule za Misingi Wanafanya Mitihani yao ya Kumaliza Elimu ya Msingi.
Kati ya Hao Wanafunzi 500,000 Wanatarajiwa kuchaguliwa Kuendelea na Masomo ya SEKONDARI.Je Wanafunzi Waliobaki yaani 600,000 mini HATIMA yao?
Je SERIKALI ina Mipango gani kwa Hao Wanafunzi?
Au Mzigo ni WA WAZAZI husika?
Au Ndio MACHINGA,BODABODA na WAPIGA DEBE kwenye STENDI za MABASI?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Ni wakata viuno kwenye mikutano ya CCM, huwezi kukuta F6 anakata kiuno labda awe analipwa
 
Back
Top Bottom