Katika idadi ya Watanzia wote (kwa mujibu wa sensa), jaribu kuangalia uwano kati ya waliosoma na wasiosoma kisha linganisha hali za maisha yao.Una point lakini kibongo bongo elimu kama hela huna unaonekana kichaa tu.
Wewe hela huna ulete kisomi kwenye vikao vya familia utaambiwa unataka kuanzisha vurugu na utakuwa unatengwa.
Tafuta kitabu kinaitwa "Why A's students works for C's students"Inachosha sanaa
Mtu anafeli la saba na kuanza kujishughulisha kufanya kazi za hapa na palee mwisho anapata mtaji anajiajiri safar ya maisha inaanza baada ya miaka kumi anajiweza mpaka anafikia kuwaajili wahitimu wa chuo Kwa mishahara mikubwa tu
Ila unakuta mtu anahitimu chuo yupo mitaani tu mpaka miaka 15 hana ajira wala ajajiajiri yupo tu anaangaika mitaani yaani amemaliza chuo ana elimu kubwa tu lakini anapitwa na darasa la saba , sijui wakoje hawa watoto wetu tunawasomesha bure tu
Wapo tu mitaani kazi yao kubeti tu wakike Kwa wakiume hawaeleweki wakisikia ajira imetangazwa wanatakiwa watu 20 wao wanaenda kama 500 kwenye interview sasa mnashindwaje kujiajiri
Amemaliza chuo hata kuunda kikombe cha mbao hawezi, ubongo elimu makamasi
Kazi mkisikia mtu ameanza na mtaji wa elf 50 amepambana mpaka amefikisha ml 20 mnaanza kumtukana mitandaoni
Na bado mpo tu
Hao watu aina ya kina Msukuma wapo wangapi kati ya 66M ya Watz?Mfano mzuri ni mbunge Msukuma. Ila darasa la Saba kwa "kuthubutu" katika utajiri anaweza kuliko msomi.
Mtoto wako atoke la saba, umpe course ya kiingereza kisha umuulize anataka kuwa nani na umfanye kuwa anachotaka?
Labda kama umpe auze duka, maana hata kwenye biashara kubwakubwa (makampuni) kunahitajika akili, ndiomaana hata hao mtajiri mnaosema hawakusoma, wametambua mkosa yao na wanalipa pesa ndefu kama ada ili watoto wao wasome.
Hilo toto lako likimaliza la saba, kisha litake kuwa Doctor,Engineer, Pharmacist au kazi nyingine za kitaalamu, hiyo course ya kiingereza itamsaidia nini.?
BALEHE INAKUSUMBUA WEWE, UKIKUA HATAKUJA NA MADA ZA KIPUMBAVU HIVI.