Wanabodi!
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania, yaani Tanzanian National Day, na sio Tanganyika. Kumbukumbu ndio ya Uhuru wa Tanganyika lakini maadhimisho na sherehe ni ya uhuru wa Tanzania!.
Kufuatia baadhi ya watu kuwa kwenye sintofahamu ni maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika ama Tanzania?.
Hivyo nimejitolea kutoa somo hili ambalo naamini litakuwa ni very benefisho kwako.
Wajameni ni katika kukumbushana tuu kuwa maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania, na sio wa Tanganyika!.
Nawatakia sikukuu njema ya Uhuru na Jamhuri.
Paskali
Update;
Kiukweli humu jf, tuna vilaza wengi kuliko tunavyo jidhania!. Watu ni wazito kuelewa mpaka basi!.
Mkuu Mti wa Muwese,
The Palm Tree , huu ndio uelewa wa baadhi ya Watanzania, wewe ukiwemo, halafu mkiambiwa ukweli mna uwezo finyu wa uelewa, mnakasirika.
You are absolutely right, kumbukumbu ni za uhuru wa nchi iliyokuwa Tanganyika, lakini maadhimisho ni maadhimisho ya uhuru wa Tanzania!.
Kuna mambo mawili.
1. Kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika.
2. Maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania ambayo hapo zamani ilikuwa Tanganyika.
Sasa najaribu kukuelewesha kwa kutumia kiwango cha chekechea, usipoelewa sasa, utanisamehe bure.
Mfano,
- Kuna binti mmoja anaitwa Binti Mti wa Muwese, kila siku yake ya kuzaliwa anaisherehekea kama kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Binti Mti wa Muwese.
- Kila akisherehekea siku hiyo, ni sherehe za kukumbuka ile siku yake ya kuzaliwa, na anayesherehekea siku hiyo ni Binti wa Muwese.
- Ikatokea mimi Pasco Mayalla, nimempenda Binti Mti wa Muwese, nikamuoa, akabadili jina sasa haitwi tena Binti Mti wa Muwese, sasa anaitwa Mrs. Pasco Mayalla na nyumbani anaitwa Mama Junior, maana kanizalia kidume kinaitwa Pasco Junior.
- Siku ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Binti Mti wa Muwese, ila sherehe ni ya Mama Junior.
- Kumbukumbu ni ya kile kilichofanyika wakati kikifanyika, ni kumbukumbu ya kuzaliwa kale kachanga kalikoitwa Binti Mti wa Muwese, lakini sherehe, yaa birthday party, sio party ya binti Mti, ni party ya Mama Junior (Mrs Pasco)
Hivyo nchi iliyopata uhuru ile tarehe 9 Desemba 1961 ni Tanganyika, hivyo kumbukumbu ndio ya uhuru wa Tanganyika, lakini maadhimisho, sherehe, ni ya Tanzania, kwasababu yule Tanganyika amebadili jina na kuwa Tanzania Bara, kwa kifupi Tanzania.
P.