Dark days 17/03/20...

Sigala
 

[emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna vichekesho vya mizengwe
Mkwere kaibiwa simu stendi Dar akaamua kujiongeza auze karanga huku akijifanya bubu

Sasa na mimi niliwahi kumuona Mrundi kaja na staili hiyo hiyo ila yeye anatembea na fimbo huku anaomba hela madukani na haongei anatoa macho mpaka unaogopa na usipompa anakutishia kukupiga

Vijana wamachinga alikuwa anawavunjia bidhaa zao mpaka siku moja wakaandaa fimbo wote
Kilichofuata aliongea kikwao kwa sauti
 
Huyu ana back up na wenye nguvu ndio maana ana jeuri kuwafanyia hivyo. Usalama wa Ukanda wa maziwa makuu jicho ni TZ ,hawako tayar kuona tunaingia matatizoni lasivyo nchi zote zinazotuzunguka zitaingia motoni.

Kuna watu humu Kwa uelewa finyu wanadai Eti jiwe alichukua walinzi wa PK Eti wamlinde!!!!!! Huwa nacheka sn.

Mwaka 2014 nilikwenda kumtembelea Babu yangu DSM, mwaka Ule palikuwa na TETESI kuwa PK angeweza kutuvamia anytime, Jioni moja Si nikatoka kwenda kunyoosha miguu, ushamba mzigo, Si nikapotea njia, naangalia mbele naona ubalozi wa Aust...,

Si nikakunja kushoto, nimetembea weeee, naangalia mbele ghafula nikaanza kuona WAZEE wananipita Kila mmoja Yuko busy na mambo Yao, Cha kushangaza mabaka ktk mavazi Yao sikuwahi kuyaona tangu Kuzaliwa, nikahisi maybe nimeingia ubalozi wa us, uniform zao zilikuwa na mabaka kama Yale yanayovaliwa na wajeda wa us wawapo jangwani, ni khak hv niliogopa sana.

Nilipohisi naelekea eneo la hatari Zaid Si nikapiga u turn nianze kurudi nilikotoka, jamaa mmoja akaniuliza vp unaenda wap?? Au umetumwa na PK uje kutupeleleza? Nikamjibu nimepotea njia.
Siku hiyo nilipigishwa kwata za hatari, kilichonisaidia ni pale nilipomtaja Babu yangu wakastuka kidogo maana alikuwa mmoja wa majuddge kipindi Cha JKN. Wakanitema nikarudi hoi!!

Watu hao niliowaona zamani ktk uniform zile ndo nmekuja kuwaona wakimlinda JPM na watu wasivojua wakahisi amewachukua Kwa PK.
 

Usiruhusu hizo hasira, codes zaweza kufanya mtu akanyamazishwa milele. We're not even safe in here!
 
Yawezekana ni kweli uyasemayo ila siasa za hovyo zimeharibu kabisa sifa za majeshi yetu hasa tiss na polis baada ya kujiusisha moja kwa moja katika kupigania maslahi ya wana siasa na wala sio maslahi ya nchi.

Hili kwangu limenifanya nipoteze kabisa imani na hivi vikosi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ni kweli me nasimama katikati na kwenye maslahi ya nchi basi.
 
Inaonekana mambo ni mengi yaliyotokea ndani, ila huko nje hatuna namna tunamtetea kulinda image yake na Taifa kwa ujumla. Ni uzalendo tu.
 
Usihukumu raia mkuu,hukumu na hawa viongozi wanaotugawa,leo anasimama kiongozi anasema vijana wote wamepatiwa mkopo,ambae hajapatiwa huenda sio mtanzania,hivi huyu anaeza kukuimbia neno uzalendo ukamuelewa??
Niko huru kupokea mawazo ya kila mtu,upo sahihi hata viongozi wetu wanatuangusha badala watetee maslahi ya wananchi wanatetea matumbo yao kwa kuiba rasilimali za nchi.

Watu wakichoshwa na haya maisha uzalendo unawekwa pembeni na kuanza usaliti. Kama Taifa kuna mahali tuliteleza, turudi kwenye misingi yetu ya awali.
 
DRC inateseka mno. Hata vijana wetu tumewapoteza sana sana sana. Roho inaniuma kweli vijana wetu huko congo.

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
Hunishindi mimi roho yangu huwa inauma sana ninapoona vijana wetu wakiteseka kwa ajili ya mtu mmoja.

Mbaya zaidi eti watu wake wana akili sana na dharau kama zote kwa wengine. Ila iko siku yake .
 
Mwamba we ni noma umenivunja mbavu aiseee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Kuna watu wachache hasa utakuta ni wale wanaotoa maamuzi juu ya wengine hawa ndio wanawavunja moyo sana wengine.

Kuna wengine wako smart sana, taarifa wanatoa lakini hazifanyiwi kazi, mambo yakiharibika wanalaumiwa wote. Kumbe ni mtu au kikundi cha watu wachache wasio waadilifu kwa maslahi yao wanaitesa nchi.

Ebu fikiria wasomi wetu wamefanya research wametoa mapendekezo fulani fulani lakini utekelezaji haupo. Siku wakifanya wengine tunasema wasomi wetu hamna kitu. Siyo kweli wenye kutoa maamuzi wanatuangusha sana.

Bado tuendelee kuwa na imani na majeshi yetu hakuna askari anayeweza kufanya kitu kilicho nje ya cheo chake bila idhini ya mkubwa wake.
 
Kweli yaani ulikuwa umepotea hadi ukafika huko [emoji846][emoji846],wale walianza kuvaa vile hadharani kipindi cha jiwe ndio maana watu wakavumisha eti wametoka kwa PAKA.Ninadhani ni kutokujua na hawakuwahi kuwaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…