Dark days 17/03/20...

Dark days 17/03/20...

Kwa hiyo waendelee na vizazi vyake kula keki na ukwasi wa kutisha..kisa anamuweza KP ..?

Apotee.. ..Ana madeni mengi mno..dhima hasa...

Wa kumkalisha slim wapo ..kwani anamshughulikia yeye peke yake?!

Ana damu za Moto ..kila upande..kumfuga huyu Ni hatari Naye mwisho atakuwa adui..maana kishajiaminisha kwamba bila yeye au mtu wake kampuni itakufa..
Hiyo kuendelea na vizazi vyake hapana siungi mkono kabisa, wapo wengine wanaoweza kutuongoza bila kikundi cha watu fulani. Lakini hekima na busara itumike.

Ila Riwaya bado haijafika mwisho hatujui Fanani atatamatishaje. Ikifika mwisho ndio tutajua alilenga nini, tutachambua mbinu za kifani na muundo wake, pia tutajikita kwenye Falsafa na Lengo la mwandishi.

Huu ni mwanzo wa ngoma ambayo ni Lele. Mwisho kabisa tutachambua kwa uhuru zaidi.
 
Kila KAMPUNI duniani lazima iwe na watu wao kuleta taarifa, KAZI Yao ni taarifa tu, taarifa hizo ni kusaidia wakati wa vita nk.

Nchi hii Iko mbali zaidi ya hapo, inahusika Hadi kuweka ma CEO ktk KAMPUNI nyingi tu Afrika.

Huyo paka ni Mwizi tu, pale Kwa m7 na cngo wanaenda kuiba Kwa kupata msaada wa KAMPUNI za nje na kugawana nao na kubadilishana technology.

Matendo wafanyayo yanajulikana na hayajavuka limits za kiusalama kuwa threat Kwa KAMPUNI yetu.

Hujawahi kujiuliza kwann KAMPUNI yetu inaweka CEO KAMPUNI ingine na haijihusishi kuiba raslimali za huko kama PAKA afanyavyo na kuleta hapa kutatua matatizo ya umaskini wa watu wa kwetu?

Nchi hii ni Police wa Africa nzima kuhakikisha amani inatawala. Kuna muda huyo PAKA alivuka limits pale cngo, anapewa silaha nzito bt alipigwa kama mtoto wanaume waliingia Hadi chumbani kwake na akapewa onyo.

Paka ni mtoto mdogo sana kwetu tukiamua hata kesho tunaweka mtu wetu, Afrika nzima Kwa masuala ya ulinzi na USALAMA yanaanzia na kuthibitishwa hapa.

Nchi hii tuna UPENDO Kwa wengine hatuna TAMAA na ndio chanzo Cha AMANI uionayo. Niamini Nchi hii ni zaidi ya uijuavyo. Mungu wa Mbinguni anapaangalia hapa ndomana viongozi wafanyapo mabaya tunasema tu na mabadiliko yanafanyika Si kama pengine Hadi maandamano na kumwaga Damu.
Mkuu unajua sana kujipa moyo. Hongera.
 
Wamo kibao humu utaona wanavyomtukuza na kumpamba utadhani malaika.Watafutwe wasukumizwe kwenye kamkoa kao watuachie kampuni yetu hatujazoea mambo ya maugomvi wala ubaguzi wa kikanda na ukabila, kokote kwenye kampuni yetu mtu unaishi raha mustarehee hakuna anayeuliza wa wapi labda kwa ajili ya utani au akutambulishe na mtu wa kwenu, ila kwenye kubaguana hakuna kitu kama hicho.
Acha tu mkuu. Roho inaniuma sana

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Kwa nilivyofuatilia mwanzo mwisho wa hii mambo yako yoga...kwangu naona au ningependelea Mr born town aibuke na ushindi katika hii battle.hofu Yangu na nisingependa team Mzee,current CEO,kp washinde maake Huyo kp ni MTU mbaya sana.niliwai ona makala Fulani humu jf ikimzungumzia marehemu Mchungaji mtikila alivyolitahadharisha taifa juu ya pk kupenyeza watu wake.kp ni hatari katika region yetu.kwahivyo ijapokua simpendi Mr born town kwa anachotufanyia..anakula keki ya taifa yeye na familia yake tuuu.tunamuhitaji born town kumstopisha kp au sio wadau???
 
Ninaweza kukubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo ambayo majeshi yetu huyafanya pasipo watu wengine kujua. Tanzania imefanya operations nyingi sana na zenye mafanikio makubwa. Hata hili la kumuonyesha bwana Paka ni mjanja wa Intelijiensia lina sababu zake na kwa maksudi maalumu.

Kipindi kile cha 2014 alivyojifanya kwamba anaweza kuipiga kampuni yetu, watu wetu wa kazi waliweka mitambo kwenye kakichuguu na wakawa wanaichungulia kampuni yake.

Wakati anawaza kuipiga kampuni yetu tayari vijana wetu wa kazi walishahamisha baadhi ya watu wetu na kutengeneza shelters ili akirusha tu hakuna raia hata mmoja, sasa ushangae kule kwake hakuwa amejipanga hivyo, so angeleta madhara makubwa kwa wananchi wake na kampuni yake.

But thanks God alipigwa kwa diplomasia tu.Jamani fuatilieni historia ya nchi yetu, ni nzuri sana n ya kusimumua, ukiijua mtu hawezi kukudanganya kwamba tu dhaifu. Tuko imara sana.

Kitu kingine ambacho hakujua alidhani infos alizonazo zimemtosha kuijua kampuni yetu, kumbe hakuwa anajua kama alivyojiaminisha, alijua vichache huku vijana wa kampuni yetu wakijua mengi ya kwake.

Kampuni yetu siyo hivyo jinsi ilivyo madhaifu yetu ya ndani haina maana kwamba hata huko nje ndivyo tulivyo. Siyo kila mlevi amelewa. Mambo mengi huachwa hivyo hivyo kwa maksudi.

Kule porini kuna mambo nyinyi acheni kabisa, mmewahi kusikia pango la wanyang'anyi ambalo lilikuwa likifanya uharamia? Linavamia watu linaiba mbuzi,ng'ombe, kuku, bata mpaka nafaka kisha wanatumwa wazawa kwenda kusaga halafu wanawapelekea kwa kuogopa kuuawa?

Hili genge lilijiona untouchable wakati huo, walikuwa ni wengi kama kijiji, kuna wake, watoto na watu wengine kibao wanaoshirikiana nao, mnajua walifanywa nini?

Saa 2 za usiku ,walijikuta wamefukiwa pasipo kusema hata kwaheri, na mnajua kwanini ilikuwa ni saa 2 za usiku? Kwasababu ulikuwa muda wa msosi wa usiku wamekusanyika pamoja.

Kisa kingine huko huko,majambazi yalikuwa yamejificha porini na yameleta usumbufu mkubwa sana, kila yakitafutwa hayaonekani lakini utekaji unaendelea.

Akatumwa Komandoo mmoja kutoka JWTZ wakamdrop porini akaanza kuwatafuta, ghafla hawa hapa, akawasoma na kujua idadi yao, nao bwana vile vile wanaota moto wamejikusanya. Alipiga risasi moja kwenye ule moto si mnajua baruti na moto. It was the end.

Watanzania wenzangu JWTZ, TISS na POLISI ni vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo viko imara sana hizi changamoto za ndani zisitufanye tukose navyo amani, vinafanya kazi nzuri sana ila kwa kuwa hazitangazwi si rahisi kujulikana. (Hawa wachache wanaoharibu ndio waondolewe)

Mambo yao ni mengi hapa nimeandika kwa ufupi tu. Kama nilivyosema huyu mtu huenda anapaishwa tu lakini kwamba ana nguvu kiasi cha kutupangia cha kufanya sidhani kwa jinsi ninavyoijua na ninavyoielewa nchi yetu kwa historia yake.
Changamoto za ndani zimefanya hivi vyombo Raia wa kampuni wapunguze imani. Maana inasikitisha wizi na uharifu ndani ya kampuni unafanyika kila siku vyombo vipo. Vitaaminika vipi sasa? kweli huenda wanafanya kazi nzuri lakini mapungufu yamekuwa very obvious.
 
Kwa nilivyofuatilia mwanzo mwisho wa hii mambo yako yoga...kwangu naona au ningependelea Mr born town aibuke na ushindi katika hii battle.hofu Yangu na nisingependa team Mzee,current CEO,kp washinde maake Huyo kp ni MTU mbaya sana.niliwai ona makala Fulani humu jf ikimzungumzia marehemu Mchungaji mtikila alivyolitahadharisha taifa juu ya pk kupenyeza watu wake.kp ni hatari katika region yetu.kwahivyo ijapokua simpendi Mr born town kwa anachotufanyia..anakula keki ya taifa yeye na familia yake tuuu.tunamuhitaji born town kumstopisha kp au sio wadau???
Duuh
 
Nadhani kitu kama hicho ila sikumbuki vizuri. Pia inawezekana ndio huyo huyo aliwahi kumpiga mkwara Paka kwamba usipoacha ujinga wako wa kupigana pigana huko ninakufuata nikiwa full.Akatulia.

Sasa huwa ninashangaa eti ana nguvu sana,mara atatupiga, ana jeshi imara sana, hizi propaganda siyo nzuri ifike mahali zife kabisa maana zimeshawaharibu baadhi ya vijana na kumuona shujaa.
Pk alikuwa anatupa miili kule ziwani, Mr mboma akamwambia pk aondoe hizo takata(miili) Mara mmoja lisionekane hata tone la damu. Pk Akafanya hvyo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umenikumbusha kitu.Kuna sehemu tulienda na wife,sasa wanawake wenzake wakawa wanamtenga kwenye story zao nikawauliza vipi mbona mwenzenu mmemuweka pembeni, wakasema unajua mwenzio hajui kilugha sasa umbea kwa kiswahili haunogi, so naunganisha na msemo wako.[emoji846][emoji846]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umbea mtamu kwa lugha ya mazoea.
 
Yawezekana ni kweli uyasemayo ila siasa za hovyo zimeharibu kabisa sifa za majeshi yetu hasa tiss na polis baada ya kujiusisha moja kwa moja katika kupigania maslahi ya wana siasa na wala sio maslahi ya nchi.

Hili kwangu limenifanya nipoteze kabisa imani na hivi vikosi.

#MaendeleoHayanaChama
Sio wewe tu Wafanyakazi wengi wakampuni
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna vichekesho vya mizengwe
Mkwere kaibiwa simu stendi Dar akaamua kujiongeza auze karanga huku akijifanya bubu

Sasa na mimi niliwahi kumuona Mrundi kaja na staili hiyo hiyo ila yeye anatembea na fimbo huku anaomba hela madukani na haongei anatoa macho mpaka unaogopa na usipompa anakutishia kukupiga

Vijana wamachinga alikuwa anawavunjia bidhaa zao mpaka siku moja wakaandaa fimbo wote
Kilichofuata aliongea kikwao kwa sauti
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Changamoto za ndani zimefanya hivi vyombo Raia wa kampuni wapunguze imani. Maana inasikitisha wizi na uharifu ndani ya kampuni unafanyika kila siku vyombo vipo. Vitaaminika vipi sasa? kweli huenda wanafanya kazi nzuri lakini mapungufu yamekuwa very obvious.
Ninakuelewa mkuu. Kuna wakati najiuliza nani amfunge paka kengele?

Imani imeshuka sana kwa raia kwa vyombo vyetu vya dola hasa polisi mpaka inatia hasira kwasababu kuna ujinga ulikuwa unafanyika mpaka mtu wa kawaida unajiuliza ina maana hawayaoni haya kweli?

Viongozi wetu ndio wakulaumiwa, vijana wetu wako vizuri lakini wanaamriwa kufanya utekelezaji tu japo hata wao roho inawauma.

Unajua kuapa kwamba nitatii amri ya mkubwa wangu nayo ni shida ukienda kinyume unaonyesha umekiuka kiapo cha utii inakula kwako. Kiapo cha kimwili na kiroho ni kibaya na wakati mwingine ni kizuri inategemea umeapa kwa ajili gani.

Kwa kweli viongozi wetu wabadilike sana,waache tamaa, wazuie wizi, ufisadi, uzembe na rushwa. Bado ninaamini tuna jeshi zuri na imara kabisa, kama tukirekebisha hizi kasoro ndogo ndogo tutakuwa Taifa lenye kutamaniwa na wengi kuja kuishi ndani yake.

Hata Polisi kuna kazi nzuri sana huwa wanazifanya kwa umakini na zinafanikiwa lakini hazitangazwi, ila likitokea baya linajulikana na kufuta mazuri yote. Me ninadhani hata mazuri yawe yanasemwa ili tujue sisi raia, tusiwe tunajua mabaya yao tu.
 
Pk alikuwa anatupa miili kule ziwani, Mr mboma akamwambia pk aondoe hizo takata(miili) Mara mmoja lisionekane hata tone la damu. Pk Akafanya hvyo
Umeona ehee. Yaani huo ukanda mzee ni noma. Me ningeshauri wazawa wa kule wanagekuwa wengi hapa JF yaani tungepata uhondo sana maana kuna matukio mengi ya kufurahisha na kustaajabisha.

Pia itakuwa ule mto mkubwa unaoanzia kwa jirani yake kusini hadi kwenye bwawa kubwa la akina Viktoria jirani na akina mama Koku.
 
Back
Top Bottom