Dark days 17/03/20...

Nyakanazi - Lusahunga - Biharamulo - Bukoba hadi Mutukula

Unapita muda wowote sasa hivi

V T alipaweka shwari kabisa
Hapa ninazungumzia mabasi, ila magari mengine wanapita. Zamani ilipokuwa ukifika muda wa kupita hiyo njia haijalishi ni mchana au usiku kiroho kinadunda, mpaka umalize salama ulishaomba saaana. Hata hili ni la kushukuru sana, wale watu walitamba sana enzi hizo.
 
Jeshi la polisi wanilidharau lakini kuna wengine tunajua mziki wao, kuna kipindi mauji na uharifu wakutumia silaha ulikithiri kigoma kilichotokea ni historia. Walikuja marastaman kujifanya wachoraji, wengine wasanii Dah! warundi walikaangwaa kwelikweli. Kuna sniper aliwatwanga za kichwa majambazi kama saba wote walimwagwa hospital vichwa vimetobolewa. Tuache siasa ukijua kulaumu basi jua na kushukuru, viva maafande wetu mnafanya kazi nzuri
 
James mwakibolwa
 
Wazee wa ngerengere wasikie tu wale jamaa ni hatari wanamafunzo kwelikweli ya kutumia silaha na mapambano
 
Umeongea kitu kikubwa sana.

Na nilisema watu wa Kanda ya ziwa na Kigoma wasimulie matukio ya namna hii maana wao wanajua madhara ya vita, uhalifu wa kivita, ujambazi, wizi,watu wenye roho mbaya wanawajua vizuri sana, ulafi wa madaraka, chuki za kikabila wanazijua kupitia kwa majirani zao.

Jeshi la Polisi linafanya kazi nzuri sana,mimi mwenyewe nimewahi kusaidiwa na polisi kutoka kwenye mikono ya majambazi yenye silaha za kivita, zile silaha nimewahi kuziona kwenye filamu tu,lakini siku hiyo niliona live.

Kwa weledi wa askari wetu ambaye alikuwa escort wetu hawakuweza kulifikia gari japo walitupiga na kusababisha vifo na majeruhi ila mizigo yetu na pesa ilibaki salama, walikuwa mtu kama 10 na silaha nzito, askari wetu alikomaa nao mpaka wakakimbia.

Kwahiyo watu wachache wanaoharibu sifa za jeshi letu waondolewe na kubakisha wale wanaostahili tu.Kongole pia kwao.

Utasikia watu wanasema tutakinukisha iwe isiwe, ngoja lipigwe bomu la machozi tu,watu hoi, machozi,makamasi kama yote, wengine wanasema tulizimia kabisa, sasa shida yote hii ya nini?

Sasa kwenye hizo Kanda kusikia milio ya mabomu, risasi, moshi wa baruti, maganda ya risasi ilikuwa ni kitu cha kawaida, watu wa kule huwa hawashadadii vita wanajua madhara yake.

Kuna kipindi ikifika saa 12 jioni watu mnaingia ndani mji wote kimya maana hamjui watakuja saa ngapi, hivi mnajua walikuwa wana ujasiri wa kuja mpaka karibu na vituo vya Polisi?

Ila sasa operation ilivyoanza mbona waliimba nyimbo zote? Ukiona mtu anataka vita muangalie mara mbili mbili, labda anajua pa kukimbilia ila sisi wengine ambao hatujazoea shuruba za kutumikishwa au utumwa kwenye nchi za watu hatuwezi kuunga mkono.

Watanzania baadhi wanajidangany kwamba likitokea la kutokea tutaomba hifadhi kwa majirani, sahau hiki kitu,hatupendwi, tunaonewa wivu,huko tutanyanyasika sana.

Bora niongozwe na Rais anayeonekana ni dhaifu machoni pa watu anayenijua udhaifu wangu,mila zangu,utamaduni wangu,miiko yangu, kuliko kutawaliwa na mgeni asiyenijua atanirudisha utumwani.
 
Wazee wa ngerengere wasikie tu wale jamaa ni hatari wanamafunzo kwelikweli ya kutumia silaha na mapambano
Ni kweli miili yao tu ni silaha tosha.

Huko kwa majirani kuna komandoo eti ametishiwa na jambazi panga akatoka ndukiii hadi kambini kwao kuomba msaada, walivyokuja hawakukuta mtu, sasa jambazi akusubirie tu.

Yaani panga jamaa kakimbia, angekuwa na bunduki je? Ila wanavyoisifu nchi yao, jeshi Lao utadhani ni level nyingine.

Nilichojifunza ni uzalendo wa nchi yao. Watanzania tuamke hakuna atakatekuja kuisafisha na kuipamba nchi yetu kama siyo sisi wenyewe.

Hakuna nchi hapa duniani isiyokuwa na madhaifu lakini hayasemwi hadharani.

Upinzani na nyinyi mtusaidie kuwaeleza watu wenu kuongea kitu cha kweli,mlipinga sana vitu vya kweli hadharani huku vyumbani mwenu mnaishia kusema ni kweli lakini serikali imefanya.

Hii ni nchi yetu sote, leo upo upinzani lakini kesho upo chama tawala, sasa yale uliyokuwa ukiyapinga utaanzaje tena kuyahubiri?

Utawala uliopo unaweza kuisha, vyama vikaisha na vikaja vipya, wapinzani wakaisha na kuja wengine. Lakini Tanzania itaendelea kuishi vizazi hadi vizazi.

Taifa ili liishi daima ni kujenga uzalendo wa kweli kwa vizazi vichanga ili vikue kati hali ya kuthamini utu na vitu vya nchi yao..."mfundishe mtoto njia impasayo kwa maana akikua hataiacha.."( nukuu kutoka kwenye Biblia).
 
Kulala Kahama

Nilisikia ni mkakati

Wa kibiashara



Kuboost uchumi wa huo mji

Ingawa Lusahunga palifaa zaidi

Bukoba ingebaki Km 230 tu
Ila watu wanateseka mazingira ya pale stend siyo mazuri sana, kama ni kulala pale mabasi mengi tu ya dar na sehemu nyingine ndio mwisho wao?

Kwenda Bukoba ni machache sana haiwezi kuathiri zaidi kama yataruhusiwa kupita.
 
Hizi ngonjera kawape wengine, uongo mtupuuu.
 
Mm nilipata ajira wakati wa mkapa, nikaaacha ili niende kusoma . Nikaja nikapata tena wakati wa JK 2011, nikaendelea nayo nikaacha 2016. 2017 wakati wa Magufuli nikapata tena na ndio nipo nayo hadi sasa japo naweza pia kuja kuiacha.
Kwa tafsiri yako maraisi hao wote watatu ni wazuri kwa kuwa Mimi nilipata ajira miaka yao wakiwa madarakani?
Magufuli alikua na madhaifu mengi sana ya kiuongozi Ila kusema pia JK naye sikuona huo uungwana, nilichoona yeye alikua mfanyabiashara hivyo alikua akienda sawa na partners wenzake kwa kuwa alikua na cha kupoteza.
Mchunga ng'ombe yeye hakuna na cha kupoteza ndio maana alikuwa vile wa kuharibu haribu tu
 
Sasa je,n bora born town aende au pk?me nawaza aende pk kwanza alaf huyu born town ataenda hata kwa kulogwa[emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…