Kuna wakati shetani mwenyewe anaweza kuongea kupitia kinywa Cha mwanadamu.Ukifuatilia Bungeni wana utaratibu wa kuanza session na ratiba ya bunge kwa dua na sala kila siku.
Pia tuna katiba inatambua na kuruhusu uhuru wa kuabudu kwa watu wote kila mmoja kwa imani yake.
Sasa kama huko bungeni wanaanza siku kwa kumuomba Mungu kwa dua na sala kwanini iwe ni tatizo mkuu wa nchi kutangaza maombi kwa taifa?
Bungeni wanaomba Mungu kwanini mkuu wa nchi kutangaza maombi iwe tatizo?
Mfano mtu aliyepagawa na mapepo, aweza ongea mambo ambayo akiulizwa BAADAYE haezi kumbuka,
Daudi aliingiwa na mawazo asijue yametoka wapi, ghafula akaamua kuwahesabu wananchi anaowaongoza, Nchi ilipata ADHABU Kutoka Kwa Mungu sababu mawazo Yale aliyaweka SHETANI ndani ya Daudi Mfalme.
Petro aliposikia YESU akisema atakufa baada ya siku kadhaa, aliropoka na kusema, Hutakufa, MIMI Petro nitakufa Badala Yako, Yesu alijua aliyeongea Si Petro Bali ni SHETANI kupitia kinywa Cha Petro akamwambia Rudi nyuma SHETANI maana u kikwazo kwangu.
So usishangae kauli kama hizo za kupinga mambo yenye TIJA Kwa Taifa.