Mojawapo ya mtu influential ndani ya TISS au mwenye ushawishi kwenye top state organizations ndio anaweza pata classified info za crandestine operation kama hii. Na lazima kuwe na some information lagging kwenye story nzima, huwezi jua wapinzani waliambiwa nini, ukajua DAB aliambiwa na kufanya nini, ukajua story ilianzaje na kuishaje. Confession hufanyika na mtu mmoja aliyehusika kwenye part yake, secret service hawaambiani role ya kila mmoja. Nenda popote duniani mission yoyote ngumu ikivuja kuna story inakosekana kuunganisha.
Then mission ngumu huwa ni one way, huitaji kutumia Polonium-210 zaidi ya mara moja au kuipa msaidizi wa aina nyingine kama umeshajua ya kwanza ilikuwa successful, na hiyo sio sumu ya kumuondoa head of state unless uwe very careless na matokeo, ikifanyika autopsy kinyume na ulivyotarajia unapata matokeo tofauti. Polonium yenyewe ina dalili ambazo huyo deceased hakuwa nazo, hakunyonyoka nywele wala mwili kuwa fainted.
Presidential security sio wazembe kama ilivyoonyeshwa hapa. Hakuna individual mmoja anayeruhusu mtu kupita au kutokaguliwa, inahitajika wawepo vilaza wa hali ya juu sana kumruhusu mtu bila kukaguliwa. Hata akipangwa mlinzi mmoja, bado sio jukumu la single individual kuamua. Ni jukumu la protocol, unless ungesema aliyeshiriki ni mke au mtoto wa mhusika somehow naweza kubali. Then chakula cha mkuu hakiguswi na mtu, huwezi mimina chai hapo ukasubiri atoke sijui chumbani anywe, mambo sio rahisi kama unavyodhani.
Mtu mwenye nafasi kama yako kuna maandiko anakuwa nao, sio huu wa kutumia emoji nyingi na kutumia lugha ambayo tunajua agent hawezi kuwa kama huyu. Kuna mambo mengi sana yana makosa ila tuishie hapa. Huu ulinzi anaopewa head of state unaoonesha hapa unaweza zidiwa na hata alionao CEO wa CRDB