Nadhani, kama it is a good idea, TISS ivunjwe:
Iundwe:
1) Tanzania Intelligence and Security Agency.
2) Tanzania Secret Service.
Zote mbili zihusike na mambo ya ndani pamoja na mambo ya nje.
Ila TSS inaweza kuwa maalumu zaidi kwenye eneo la ulinzi wa viongozi. Presidential Protection Unit, na VIP Protection Unit, zinakuwa ndani ya TSS.
Nadhani Takukuru ibadilishwe iitwe: Tanzania Bureau of Investigation, kwa kiswahili: Taasisi ya Uchunguzi (au Upelelezi). Kazi yake iwe kuzuia na kupambana na economic crimes (including corruption).
Kwingine kubaki kama kulivyo, Millitary Intelligence, Millitary Police, Police Intelligence, CID, FIU, DCEA, zote zibaki kama zilivyo.
Kuwe na 'polisi wa polisi' ndani ya jeshi la polisi. Ambao kazi yao itakuwa kusimamia nidhamu ya polisi wenzao, kama vile millitary police wanavyosimamia nidhamu ya wanajeshi wenzao.
Halafu kuwe na maximum security prison(s), ambapo watu waliokamatwa kwa mujibu wa sheria na kwa sababu za msingi kabisa (Using an improved Preventive Detention Act etc) na TISA au TSS, watakaa, hadi watakapo achiwa au kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.
Watu hao pia wanaweza kutembelewa na ndugu zao au na wanasheria wao. Pia, haki za binadamu za watu hao ziheshimiwe.
Magereza yaboreshwe ili kupunguza msongamano wa wafungwa, na ili kuboresha haki za binadamu za wafungwa wote.