My brother in Christ,unaongea na Mungu Mkuu kwa sauti na wazi wazi? Real?!
Ndio,
Mungu anaongea na WANADAMU wema Kwa waovu kupitia NDOTO, NENO,maono mchana,na ktk Ulimwengu wa Roho tukilala au macho wazi.
Asiye na VAZI, Mungu akisema naye mchana Kwa maono na asisikie, humjia usiku alalapo ktk ndoto mwili ukitulia , alalapo. Makinika na ndoto uotazo na ukaamka unazikumbuka.
Aliye na VAZI, anaye Roho wa YESU aitwaye ROHO MTAKATIFU, huyo amesaidia kurudisha mahusiano na mawasiliano kama aliyokuwa nayo adamu Bustani ya EDEN.
Mungu anaongea nasi wazi wazi na tunaisikia sauti yake clear. Unaweza panga safari siku Fulani, bt Mungu akabadili ratiba ya safari Kwa maelekezo kabisa.
Unaweza andaa somo la kuhubiri usiku, akabadili somo au kuongeza ayatakayo useme na watu wake.
Tusomapo NENO lake husema nasi wazi wazi na sauti utasikia kupitia sikio la ndani la mtu wa ndani, ROHO.
KUPITIA KINYWA CHA NABII.
Mungu anaweza kuongea kupitia kinywa Cha Nabii akitoa maelekezo, akifundisha au kuonya watu wa Mungu.
Pitia channel ya UKWELI MINISTRY Nabii MESHACK ana karama hiyo, ya Mungu kuongea wazi kupitia kinywa Cha Nabii.
Mungu anaweza ongea na watu kupitia kinywa Cha muhubiri Ibadani, anaweka neno lake na unatamka mambo yenye kugusa maisha ya watu ambayo hata akili na mawazo Yako hayakupanga kuyasema na mengine hutoyakumbuka Hadi ukumbushwe na waliosikia ujumbe.
Ukitaka kulisikia sauti ya Mungu wazi wazi, acha dhambi, ishi maisha ya Utakatifu, hata ukiwekewa SUMU ktk chakula na maadui atakukataza kula.
Mungu Yu juu ya yote.
Amen