S
Naomba kuuliza kuhusu Kule kisiwani,
1. Hivi bajeti yao kwa mwaka ni kiasi gani?
2. Makusanyo yao kwa mwaka ni kiasi gani?
3. Mgao wao wa muungano kwa mwaka ni kiasi gani?
Maana yanayofanyika hivi sasa kisiwani unajiuliza hizi ni hela za makusanyo yao ya kodi, mgao wa muungano na mikopo kutoka kwa wahisani pekee au kuna hela nyingine wabara tunapigwa na Mkojani fc?
1. Barabara za ndani ndani mitaani asilimia kubwa za Unguja zimewekewa lami,
2. Barabara ya Mnazi mmoja hadi Airport imefumuliwa na kujengwa upya,
3. Barabara ya Mtoni - Darajabovu hadi airport nayo hivyo hivyo imefumuliwa na inajengwa upya.
4. Fryover Kwerekwe na Amaan,
5. Uwanja wa mpira wa Abeid Karume umepanuliwa ili uwe mkubwa na wa kufunika.
6. Soko la kwerekwe limepigwa chini linasimamishwa jingine,
7. Soko la Mombasa nalo hivyo hivyo jipya linajengwa.
8. Soko la chuini la kimataifa lenye supermarket na yard za magari linajengwa.
9. Soko la Jumbi la kimataifa litakalokuwa na kumbi za mikutano nalo hivyo hivyo linajengwa.
10 Mkwajuni nako soko jipya.
11. Bandari mpya ya boat za abiria kujengwa Kizimkazi.
12. Bandari mpya ya meli za mizigo inajengwa Mangapwani.
13. Chuo cha kimataifa maeneo ya Fuoni kunajengwa.
Bado huko Pemba na miradi mingine chungu zima inayoendelea kufanyika.
[emoji1621] Ni muda mfupi sana yaani huu ni mwaka tatu tangu jamaa akae madarakani haya yote yote anayoyafanya, wakati mambo haya yakikamilika hata Amaan Karume na Shein waliokaa miaka 10 madarakani hamfikii huyu kwa wingi wa miundombinu anayoifanya.
[emoji1621] Mkojani Fc aliwahi kujidai kusema kwa wateule wake pasipo kuwakemea wala kuchukua hatua za " kila mtu hula kwa urefu wa kamba yake, mna kula sana na kuvimbewa"
Je amewaacha wateule wake wa bara wale wawezavyo ili yeye awe anachepusha hela zetu za bara kwenda kisiwani pasipo kuhojiwa na wateule kwa sababu na wao si wasafi?
[emoji1621] Kama si hivyo mdogo wake kisiwani anatoa wapi hela zote hizo za miradi mikubwa mikubwa hivyo?
Bara utasikia miradi inaenda slow slow lkn Kisiwani miradi inaenda kwa kasi ya 5G
Pascal Mayalla,
TumainiEl