Dark days 17/03/20...

Dark days 17/03/20...

hapana, 4 5% sio ya pato la ndani, ni shares ya Zanzibar katika pato la nje la mikopo na misaada yoyote ya JMT kutoka nje ila hazihusishi FDI. Tanzania ikikopa dola bilioni 100, dola Bilioni 4.5 zinapelekwa Zanzibar!.
P
Je wanashiriki kulipa marejesho?? Hiyo mikopo 4.5% nani anairejesha pamoja na riba zake?

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Kiukweli ni ngumu sana, hebu chukulia polisi tuu au jeshi, angalia wanatumia kiasi gani Zanzibar, halafu ukokotoe wanatumia kiasi gani bara, then kile kiasi cha bara ni kiasi gani jeshi linatumia kwa ulinzi wa mipaka ya Tanzania bara tuu, hizo ni gharama za bara, uje kwenye kiasi gani kinatumika kulinda mipaka iliyoongezeka ya Zanzibar, inashindikana kwasababu hata bila muungano jeshi lingelinda mipaka ya Tanzania bara yote, hakuna namna ya kukokotoa gharama za ziada za ulinzi wa mipaka ya Zanzibar pekee!. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Wizara zote za muungano pia ni Wizara za bara, hakuna demarcation ya gharama za bara pekee na gharama za muungano!. Dawa ya hili ni serikali 3.
P
Serikali tatu tena brother?
Pona yetu ni kuvunja huu muungano ,au iwe serikali moja Zanzibar iwe mikoa ya Tanganyika.
 
Je wanashiriki kulipa marejesho?? Hiyo mikopo 4.5% nani anairejesha pamoja na riba zake?

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
Kanuni ya mkopo ni anayelipa ni aliyekopa, hivyo mikopo ya JMT Zanzibar anapatiwa 4.5% na halipi, analipa aliyekopa!.

Ila kuna mikopo Zanzibar anakopa kwa udhamini wa JMT, hii ni Zanzibar wenyewe wanalipa, ila ikitokea Zanzibar akashindwa kulipa, atakayedaiwa ni mdhamini!.

Kuna madeni kibao tunawalipia na hatuna tatizo!. Vipi wenzangu unaona shida yoyote kumlipia deni mkeo?.

P
 
Kanuni ya mkopo ni anayelipa ni aliyekopa, hivyo mikopo ya JMT Zanzibar anapatiwa 4.5% na halipi, analipa aliyekopa!.

Ila kuna mikopo Zanzibar anakopa kwa udhamini wa JMT, hii ni Zanzibar wenyewe wanalipa, ila ikitokea Zanzibar akashindwa kulipa, atakayedaiwa ni mdhamini!.

Kuna madeni kibao tunawalipia na hatuna tatizo!. Vipi wenzangu unaona shida yoyote kumlipia deni mkeo?.

P
Hahaha eti mkeo.

Inavyoonekana Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kindugu zaidi kuliko kisheria. Sa zingine sheria inaweza kukutenga na ndugu zako lkn upendo hauwezi.

Hii ndo sababu wakasema tudumishe Muungano wetu kwa ghalama yoyote ile. Sasa linapokuja swala la ghalama wengine bado wanahoji inakuaje.
 
Haya sasa ni mambo ya numbers, sio mambo ya Ikungulyabashashi wala wapi!, kiwango halisi kiko kwenye bajeti, naweza kukupa estimates za 42 trillion nimeiround 40 trillion na hivyo 4.5% nimeround 5%
hivyo 40 x5 ÷100= 2 hivyo Zanzibar ni trillion 2!.
P
Pato la taifa ni sawa na bajeti ya nchi? Umezidi kumchanganya huyo nghosha. Pato la taifa huwa zaidi ya Trillion 100!!
 
Mkuu mwambie aende Zanzibar akafanye research ya mamiradi mikubwa mikubwa inayojengwa huko, halafu aoanishe, mapato ya Zanzibar, mgao wa mapato ya muungano, mikopo ya wahisani, sijui na hela za kubinafsisha visiwa vyao kama hela hizo zinaweza kujenga miradi mikubwa mikubwa kwa muda mfupi aliokaa madarakani.
Ok, nilitaka nichangie ila ngoja kwanza
 
Yoga nina ombi kwako kwamba kabla ya December weka hii Dark days katika mfumo wa PDF, yaani kuanzia season 1 hadi ulipoishia.

Bado tunasumbuka kufatilia hii story kwa sababu comments za wadau ni nyingi na zinatupoteza wafatiliaji wa dark days story.

Binafsi sijui hata story ilipoishia ni post namba ngapi.

Ni ombi nawasilisha.
 
Ni ombi nawasilisha.
Njia Rahisi, ni kutafuta post alizoweka hapa yoga Toka March 20, 2022 mpaka sasa kupitia heading ya uzi huu kule kule kwenye profile yake. Hapo utakuwa umepunguza wingi wa posts, na itakuwa Rahisi kuzibaini post husika.

Ukifuata maelezo haya utakuwa umesaidia sana sisi kupata haraka uzi mpya tarajiwa kutoka kwa yoga; maana yoga atakuwa na muda wa kutosha kufanya maandalizi ya uzi mpya.
 
Njia Rahisi, ni kutafuta post alizoweka hapa @yogq Toka March 20, 2022 mpaka sasa kupitia heading ya uzi huu kule kule kwenye profile yake. Hapo utakuwa umepunguza wingi wa posts, na itakuwa Rahisi kuzibaini post husika.
Ninajua hilo, ila ninamuomba kama ataweza kuiweka ktk mfumo wa pdf afanye hivyo, au kama kuna mdau anaweza kufanya hivyo basi yoga atangaze tenda kisha mdau aliyewin apewe kazi
 
....kufanya hivyo basi yoga atangaze tenda kisha mdau aliyewin apewe kazi
Vurugu (kama unaziona ni vurugu lakini) zote hizo ninazofanya, lengo kufanya yoga ashughulike tu na kazi ya kuandaa Episode mpya tu.

Kwa kuwa unashauri tenda itangazwe ya kutengeneza pdf ( yoga asihusishwe kwa namna yoyote Ile kwenye kutangaza tenda hii maana kazi yake ameishamaliza) nashauri ulisimamie hili wewe Mkuu.

Ikiwezekana, unaweza kufanya bidding mwenyewe ukajipa tenda.
====
Kwa maelezo haya, unaweza kufikirika ni kwa namna gani ninaisubiri kwa hamu hiyo episode ya December kutoka kwa yoga. Ha ha haaaa!

Mchana Mwema, Mkuu.
 
Why serikali tatu? How do we benefit with Zanzibar at all?

Binafsi ninafikiri ni bora tudai Tanganyika yetu.

Tishio la usalama lililokuwepo wakati wa ule halipo tena.

Tuwaache hao mbwa wajitegemee.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Mpaka watoto WA Cain waamue ndio mtatengana bila hivyo tukae kwa kutulia tuote jua.
 
Nguruvi3 anauliza wao wanachangia kiasi gani kwenye akaunti ya pamoja?
Mkuu P

Uongo wa akaunti ya pamoja umeenezwa sana na Makamu wa Rais wa Zanzibar Masoud Othman (OMO) kwa muda mrefu kwa makusudi kabisa akijua ni uongo ni uzushi lakini moja ya utamaduni wa ndugu zetu visiwnai ni Unafiki

Rais Hussen Mwinyi akaamua kuumaliza uzushi na uzandiki huo

Gazeti la Mwananchi Desemba 11 2021 limeeleza kuhusu akaunti ya pamoja


Rais Mwinyi anasema wanaokataa kuanzishwa kwa akaunti ya pamoja ni Zanzibar kwasababu itakapokuwepo lazima washirika wachangie. Hilo akasema lina tatizo kwa Zanzibar kwasababu itabaidi ichangie gharama za mambo kama Ulinzi, mambo ya ndani n.k. ambazo ni kubwa sana akimaanisha Zanzibar haiwezi.

Huu uongo na Pascal unajua ni uongo umefikia kikomo.

TUJITEGEMEE
 
It's not fair ila wao hawana kosa, waliomba wapewe gharama za kuendesha muungano, imeshindikana kwasababu Wizara zote za muungano, pia ni Wizara za Bara, hivyo hakuna demarcation ni gharama zipi za muungano na zile za bara!.
P
Hapana si kweli

Ikiwa hakuna demarcation ya gharama za Muungano na za Tanganyika mbona Wazanzibar wamepewa 21% ya ajira?
Iko wapi demarcation katika ajira?

Ikiwa hakuna demarcation mbona wanapewa 4.5% ya pato la Tanganyika ikiwemo kodi za watu , madini, Utalii, mifugo, kilimo n.k. ambazo si za Muungano? Iko wapi demarcation?

Ikiwa wanataka demarcation Mbarawa anatia saini mikataba ya bandari kwa lipi?
Katibu mkuu wa Mbarawa ni Mzanzibar, mbona hatuoni demarcation?

Ikiwa wanataka demarcation Shaka Hamdu anafanya nini Kilosa?

Ikiwa wanataka demarcarion mbona wanapewa ardhi bara ambalo si jambo la Muungano?

Ikiwa kuna demarcation wale Wabunge wa Zanzibar kwanin wanajadili mambo ya Tanganyika pale Dodoma ?

Ni hivi linapokuja suala la gharama za kuendesha Muungano Wazanziba ni wepesi wa kutafuta sababu za kipuuzi.
Kukiwa na mgao wapo ''front seat' namimi , nataka, nipewe n.k

Mkoa wa Simiyu, ambao ni mchanga sana una mchango mkubwa kuliko Zanzibar lakini tunatumia mapesa mengi sana Zanzibar kuliko Simiyu.

Kura ya maoni ni jibu, waulizwe kama wanataka Muungano, kama hawataki safari njema! hatuna cha kupoteza
 
Mkuu una hoja ya kufikirisha,juzi wakati Jamaa anasheherekea kutimiza miaka mitatu madarakani;kuna Mwandishi sijui ni wa Mwananchi aliuliza kuwa jamaa anatoa wapi pesa za kuendesha miradi;jamaa akajibu kuwa eti kaimarisha mifumo ya makusanyo kwa kuhakikisha mapatao yalikuwa yamavuja zamani yanadhibitiwa na pia mikopo ya wahisani.Dah,bado haingii akilini arguments zake!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Ni kwamba pesa zinatoka Bara. Kadri mapato yanavyokusanywa Bara wao wana 4.5%.
Pili, Zanzibar hawakopi ila kupitia JMT na deni hawalipi inalipa JMT ambayo ni Tanganyika
Tatu, Zanzibar haina Bajeti ya Ulinzi , mambo ya ndani, nje, hata Elimu ya Juu wanapata Bara
Nne, Bajeti ya Zanzibar inapewa ruzuku kutoka hazina Dar es Salaam
Tano, gharama za Taasisi za Muungano haziwahusu.
Sita, mapato ya Zanzibar hayavuki bahari lakini ya Tanganyika yanavuka

Kwa usawa huo wanashindwaje kufanya mambo makubwa? Jiulize kwanini inatokea sasa na si huko nyuma?
Marais waliopita hawakukubali uporaji wa rasilimali, tuna ushahidi lakini sasa shamba la bibi.
 
Back
Top Bottom