Wise man
The MoNA [emoji120][emoji120]
1. yanayofanywa gizani mkuu ni yapi?
2. Wenye kufanya gizani ni akina nani mkuu?
3. Mkuu kwa nini Ds hawajataka kuwa na chama mbadala chenye sera tofauti ambacho kitakuwa kinapokeza madaraka na Green ili kuwe na kuwekana bench japo miaka 10 kinaingia kingine hata miaka 5 iwapo hawajafanya vizuri km ilivyo USA ingawa wao ni miaka 8 au 4, bila shaka ina faida kwa taifa,
Kuliko siku zote wako wao tuuuuu kwa gharama zozote zile, na hii hutengeneza hali ya kiburi, kutokujali wala kuwathamini wana wa kampuni walio wengi.
Ni mengi sana yanayofanyika gizani huko,
Hivi unaamini chama kilichopo hakikutoka 2015 na 2020? Foul zilizochezwa hiyo miaka hapakuwa na refa neutral wa kuamua ni foul au lah.! Kwani wote wana maslahi na foul hiyo. Refa ameweka mkeka, wachezaji wameweka mkeka, unatarajia refa akatae foul yenye kumnufaisha yeye na wachezaji wa timu tawala ? Unalo jibu tayari.
Kuna mengi sana hufanyika huko ila nuruni panaonekana ni yafaayo japo kuna muda nuruni pia hawaoni kama yafaayo. Kidnappings and assassination ni baadhi yanayofanywa gizani, kuhama chama kwenda chama kikuu ni miongoni mwa ya gizani. Matukio yanapangwa kuhamisha mijadala mikubwa ya kampuni kama ya kitabu na DP, ni miongoni mwa yanayofanyika gizani”,.
Prof ASD alitenguliwa na kupewa barua ya kustaafu kwa hiyari, na kulipwa kila kitu akiwa na 58yrs, kinyume na utaratibu wa kitabu kwa cheo chake, alitolewa kwa nguvu kwani kuna mengi alikuwa anaambiwa ayapindishe ila hakutaka hata kidogo, wakamla kichwa. Tengua tengua za wakuu wa mabaraza na kitengo nyeti haya ni ya gizani” sio kwamba wameshindwa kazi kama wanuruni tunavyoaminishwa, ni wengi kutokuunga juhudi kwenye mambo nyeti.
Wenye kufanya ya gizani ni watu wa gizani, wenye maslahi binafsi na keki ya kampuni.
Ds ni ngumu kuuvunja kwa sababu itikadi imesambaa kwa wengi na huwezi ku sacrifice wengi kwa ajili ya wengi, ni lazima iwe mmoja kwa wengi au wachache kwa wengi.
Moja ya kitu kigumu ni kuvunja itikadi iliyokaa miaka mingi sana mioyoni mwa watu, sio rahisi na sio haiwezekani. Huu ni mchakato mrefu utachukua muda mrefu kuvunja mfumo uliopo na kuwekwa mwingine. Na ili kuweka mwingine lazima wanakampuniz wapoteza uhai wa kutosha ndipo mabadiliko yatokee.
Wenye akili wote mfumo huwatema, ukiwa mwenye akili zako timamu ukiingizwa kwenye mfumo sharti ufwate mfumo wao you like it or not. Na vichwa vigumu dawa ni kuwaondoa kwenye miili yao no better option.
Wengi wanaopotezwa ni watu ambao wanajaribu kuuvunja mfumo uliopo na wenye mfumo unaowanufaisha hawapo tayari kwa hilo. Miaka inavyozidi kwenda itikadi inazidi kusambaa ya kutaka kuuvunja mfumo, kwa kuthibitisha hilo, angali idadi ya wanaopotezwa, jaribu kuangalia wanaharakati wanavyozidi kuongezeka wa kuuvunja mfumo angalia chaguzi mbili za mwisho zilivyoenda utagundua
mfumo umeanza kuzidiwa pole pole.
Kuna gharama kubwa kufanya chaguzi za muda mfupi, kwa wenzetu wenye kujiweza ni rahisi kwao, tofauti na kwetu.
Mfumo kukaa muda mrefu au mfupi sio tija, kinachopaswa kuwepo ni mfumo wezeshi kwa wengi na zalishi kwa wengi.