DART yapendekeza nauli kuwa TZS 1,500

DART yapendekeza nauli kuwa TZS 1,500

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umependekeza nauli kwa njia jumuishi kuwa TZS 1,500 kutoka TZS 800 inayotozwa hivi sasa.

DART imetoa mapendekezo hayo katika kipindi hiki ambapo Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) ikitarajia kufanya mabadiliko ya nauli kwa mabasi hayo yaendeyo haraka maarufu mwendokasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya LATRA, wameitisha mkutano wa wadau kutoa maoni ya nauli ya mabasi hayo baada ya kupokea maombi ya kurejea nauli za mabasi hayo kwa mkoa wa Dar es Salaam kutoka DART.

Katika mapendekezo yake DART inataka njia kuu ambazo abiria wanatozwa TZS 650 kwa sasa ipandishwe hadi TZS 1,200 na kwa njia ambazo abiria wanatozwa TZS 400 kwa sasa ipande hadi kufikia TZS 600.

Kwa upande wa njia jumuishi ambazo nauli TZS 800, DART imependekeza abiria watozwe TZS 1,500 na kwa wanafuzi wanaotozwa TZS 200 imependekezwa walipe TZS 300.
 
Dart wamependekeza nauli ya mabasi ya mwendokasi iwe 1500. Kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Mimi ninaona hii nauli ni ndogo, ilipaswa kuwa 3000, kwa kuwa kutoka gerezani hadi kimara ni mbali sana, pia Yale mabasi ni mazuri na yapo faster, pia 1500 chenji zitakua zinasumbua sana.
Screenshot_20220526-161752_1.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_20220526-161233_1.jpg
    Screenshot_20220526-161233_1.jpg
    64.6 KB · Views: 30
Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umependekeza nauli kwa njia jumuishi kuwa TZS 1,500 kutoka TZS 800 inayotozwa hivi sasa.

DART imetoa mapendekezo hayo katika kipindi hiki ambapo Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) ikitarajia kufanya mabadiliko ya nauli kwa mabasi hayo yaendeyo haraka maarufu mwendokasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya LATRA, wameitisha mkutano wa wadau kutoa maoni ya nauli ya mabasi hayo baada ya kupokea maombi ya kurejea nauli za mabasi hayo kwa mkoa wa Dar es Salaam kutoka DART.

Katika mapendekezo yake DART inataka njia kuu ambazo abiria wanatozwa TZS 650 kwa sasa ipandishwe hadi TZS 1,200 na kwa njia ambazo abiria wanatozwa TZS 400 kwa sasa ipande hadi kufikia TZS 600.

Kwa upande wa njia jumuishi ambazo nauli TZS 800, DART imependekeza abiria watozwe TZS 1,500 na kwa wanafuzi wanaotozwa TZS 200 imependekezwa walipe TZS 300.
Wamefanya vizuri sana. Ni lazima kila mwananchi achangie kuijenga nchi yake. Lakini mbona viwango pendekezwa bado ni vidogo? Ni bora wapandishe zaidi ili zitumike kwa muda mrefu!
 
Nauli ya 800 dart ? ukiwa unatoka wapi kwenda wapi?
Ticket ya bei juu combined ni 1050 , (650+400)
 
Hiyo nauli ikipanda kwa kiwango hicho vurugu itarudi kwenye daladala, japo sidhani kama hayo mapendekezo yatafikiwa, itapanda kwa kiasi kidogo kama ilivyokuwa kwa daladala na mapendekezo yao.
 
Back
Top Bottom