DART yapendekeza nauli kuwa TZS 1,500

DART yapendekeza nauli kuwa TZS 1,500

Mwendokasi zenyewe ziko slow kama daladala. Wapande wafanyakazi wa DART
 
hiyo nauli ya 800 ilikuwa inatozwa mwaka gani mkuu maana najua mwendokasi njia jumuishi ni 1050
 
Kumekucha.

Wale wa kimara kivukoni express kazi tunayo.

Utoke hapo upande ya mbezi.

Mbona tutamkumbuka JPM kwa mazuri.

#MaendeleoHayanaChama

Kipindi chake Sukari ilipanda haikushuka mpaka leo.
Hata hizi nauli zinazopanda kwa sasa tusitegemee kushuka hata hali ya mafuta itakapo kuwa nzuri.
 
Dart wakitaka waweke luxury kwa anaetaka kwa nauli apande,iwe level seat halafu full kipupwe
 
Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umependekeza nauli kwa njia jumuishi kuwa TZS 1,500 kutoka TZS 800 inayotozwa hivi sasa.

DART imetoa mapendekezo hayo katika kipindi hiki ambapo Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) ikitarajia kufanya mabadiliko ya nauli kwa mabasi hayo yaendeyo haraka maarufu mwendokasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya LATRA, wameitisha mkutano wa wadau kutoa maoni ya nauli ya mabasi hayo baada ya kupokea maombi ya kurejea nauli za mabasi hayo kwa mkoa wa Dar es Salaam kutoka DART.

Katika mapendekezo yake DART inataka njia kuu ambazo abiria wanatozwa TZS 650 kwa sasa ipandishwe hadi TZS 1,200 na kwa njia ambazo abiria wanatozwa TZS 400 kwa sasa ipande hadi kufikia TZS 600.

Kwa upande wa njia jumuishi ambazo nauli TZS 800, DART imependekeza abiria watozwe TZS 1,500 na kwa wanafuzi wanaotozwa TZS 200 imependekezwa walipe TZS 300.
Mi-5 tena 🙄 kwa Bi-tozo!
 
Kimsingi DART wanatakiwa kupunguza nauli kutokana na biashara iliyopo...Kwa sasa DART wanakusanya fedha nyingi ambazo zinaibwa kutokana na mpango na usimamizi mbovu...Serikali itafute taasisi nje ya nchi ambayo ina utaalamu katika usqfirishaji wa abiria.
Kama wakiruhusu DART kuongeza nauli basi waruhusu watu binafsi waende mjini na kariakoo kwa bei nafuu.
 
Tupo uchumi wa kati. 1500 ni hela ndogo sana
Kidumu chama cha mapinduzi.
Kimsingi DART wanatakiwa kupunguza nauli kutokana na biashara iliyopo...Kwa sasa DART wanakusanya fedha nyingi ambazo zinaibwa kutokana na mpango na usimamizi mbovu...Serikali itafute taasisi nje ya nchi ambayo ina utaalamu katika usqfirishaji wa abiria.
Kama wakiruhusu DART kuongeza nauli basi waruhusu watu binafsi waende mjini na kariakoo kwa bei nafuu.
 
Hiyo nauli ikipanda kwa kiwango hicho vurugu itarudi kwenye daladala, japo sidhani kama hayo mapendekezo yatafikiwa, itapanda kwa kiasi kidogo kama ilivyokuwa kwa daladala na mapendekezo yao.
Daladala gani inafika KKOO kutokea Kimara?
 
Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umependekeza nauli kwa njia jumuishi kuwa TZS 1,500 kutoka TZS 800 inayotozwa hivi sasa.

DART imetoa mapendekezo hayo katika kipindi hiki ambapo Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) ikitarajia kufanya mabadiliko ya nauli kwa mabasi hayo yaendeyo haraka maarufu mwendokasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya LATRA, wameitisha mkutano wa wadau kutoa maoni ya nauli ya mabasi hayo baada ya kupokea maombi ya kurejea nauli za mabasi hayo kwa mkoa wa Dar es Salaam kutoka DART.

Katika mapendekezo yake DART inataka njia kuu ambazo abiria wanatozwa TZS 650 kwa sasa ipandishwe hadi TZS 1,200 na kwa njia ambazo abiria wanatozwa TZS 400 kwa sasa ipande hadi kufikia TZS 600.

Kwa upande wa njia jumuishi ambazo nauli VTZS 800, DART imependekeza abiria watozwe TZS 1,500 na kwa wanafuzi wanaotozwa TZS 200 imependekezwa walipe TZS 300.
HIVI HAWA WANAKUNYWAGA KWANZA POMBE HALAFU NDIO WANAKAA VIKAO AU HUWA AKILI WANAPELEKA WAPI?
 
Wamefanya vizuri sana. Ni lazima kila mwananchi achangie kuijenga nchi yake. Lakini mbona viwango pendekezwa bado ni vidogo? Ni bora wapandishe zaidi ili zitumike kwa muda mrefu!
Uko sahihi. Hata Marekani kituo hadi kituo ni dola 5 zaidi ya elfu 10 za kitanzania. Tulipokuwa ziarani Marekani hatukuwahi kuona wananchi wakilalamikia nauli; walikuwa wanalipa kwa bashasha kwanini hapa iwe tofauti? Hapana, watu walipe!

Hili ni soko huria kila mwananchi alipie huduma hakuna vya bure. Wasioweza wahamie Urundi.
 
Yale yale unafanaisha mimba na kitambi. Kama ndio hivyo sasa kwanini wanashindwa kulipa mishahara na posho sawa sawa kama Marekani anavyo walipa watu wake.

Yaani unafananisha kipato cha mtu wa dunia ya kwanza na ya tatu,ila si shangai aliyesema akili ni nywele ila hakutaja ni za eneo lipi.
 
Back
Top Bottom