DART yapendekeza nauli kuwa TZS 1,500

DART yapendekeza nauli kuwa TZS 1,500

Kwani tangu balaa lianze, mafuta yamepanda kwa kiasi gani? Mbona kama ongezeko lote anabebeshwa abiria mmoja?

Au kila abiria anatumia lita yake kwa kila kilomita anayosafiri?
Swali zuri sana Ndugu. Maana unamwambia mtu nauli 1500 kweli kwa maisha yapi? Inamaana kila abiria na lita yake? Badala kuboresha huduma zao wao wanazidi kandamiza abiria. Gari zenyewe zimeshajifia ,unangoja gari kituoni mpaka unakoma wanapita tu, sasa ngoja gari lifike mnajazana kama nyanya na hakuna tena spika za matangazo wala screen kuionyesha gari jili linaenda wapi.Yote tisa njoo sasa kwenye tiketi zile mashine zilishakufa na hakuna mpango wa kuzifufua zamani tulitumia hadi kadi maalum unajaza ukifika huna haja ya kukaa foleni kata tiketi unaweka kwenye mashine iasoma mlango unafunguka unapita.Badala ya kuboresha wao wanazidisha nauli yaani imekuwa abiria ndiyo wa kukandamizwa.Basi moja dogo linauwezo wa kuchukua abiria mpaka 60 sasa zidisha kwa safari ngapi kwa siku na hapo ni mwanzo hadi mwisho wa safari sijaongelea wapo wanaoshuka njiani na kuingia utaona ni kiasi gani wanapata.njoo yale marefu unaweza sema yanapakia abiria 100 nayo piga hesabu. Kumbuka haya magari hayakai kwenye foleni hivo kuna unafuu wa matumizi ya mafuta .
 
1,500/- kimara hadi posta ni ndogo? Kuweni na aibu basi hata kama mmetumwa kufanya propaganda mitandaoni.
Nagongea like!
Hana hata nerve 1 ya aibu, kwenda na kurudi mwananchi alipie Lita, Yale mabasi yanabeba abiria mpaka 100 one way, kwenda na kurudi 3,000 so kila abiria achangie Lita safari ya kwenda na kurudi!

Maajabu ya firauni!
 
Usafiri wenyewe wa kujazana na kubanana?
Huo usafiri ubadilishwe jina, uitwe Mwendokaraha au Mwendokero au Mwendokubanana!

Wabongo hakuna sustainable ya project za kiserikali yote nalaumu siasa hasa chama Fulani!
Wanaosemekana kuharibu mfumo ili kupokea mafungu ya mapato!
 
1500 ni ndogo sana, Udart watapata hasara mara zaidi. Mm nashauri nauli iwe 10000.
 
Sasa nyie mnaosema mnachangia lita, kwani gharama za uendeshaji ni lita tuu?

Kuna mishahara ya wafanyakazi, service, vipuli nk. Pia walipe kodi na kuweka akiba ya kuboresha miundombinu na mabasi, hizo hela zitatoka wapi?
 
1500 ni ndogo sana, Udart watapata hasara mara zaidi. Mm nashauri nauli iwe 10000.
Ndugu Mbaga, kuwa na aibu basi kiongozi. Hivi mnadhani maisha ni marahisi kiasi hicho, au wenzetu bado ni tegemezi hamuoni maisha yanavyokwenda eti?
 
Ndugu Mbaga, kuwa na aibu basi kiongozi. Hivi mnadhani maisha ni marahisi kiasi hicho, au wenzetu bado ni tegemezi hamuoni maisha yanavyokwenda eti?
Kwan mm nmependa iwe hvy.? Hawa watu wanatuona sisi ni source of income zao Kwahiyo Acha tuwape tuu
 
1,500/- kimara hadi posta ni ndogo? Kuweni na aibu basi hata kama mmetumwa kufanya propaganda mitandaoni.
Pole pole usipige kelele sana. Angalia mtoto asiamke ndiyo anataka kulala. Nimeongoza kuni kwenye moto ambao hawa watawala wameuwasha wenyewe pengine wananchi wataamka kwenye usingizi wa pono waliolala wakati nchi inaliwa!
 
Serikali imetoa fedha kukabiliana na ongezeko la bei ya mafuta.

Sasa DART nao wazingatie kuwa bei ya mafuta inaenda kupungua,na wao wana wanapita katika barabara maalum,hivyo foleni haiwasumbui.

Ushauri kwa DART,mjikite katika ubunifu wa kuwa na ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa biashara na huduma kwa mteja.

DART mkumbuke mlianza na nauli kubwa,lakini huduma zenu bado hazipo kiushindani, niwashauri muandae mkakati wa kuboresha huduma kwa mteja na wala sio kukimbilia kuongeza nauli.
 
Dart wamependekeza nauli ya mabasi ya mwendokasi iwe 1500. Kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Mimi ninaona hii nauli ni ndogo, ilipaswa kuwa 3000, kwa kuwa kutoka gerezani hadi kimara ni mbali sana, pia Yale mabasi ni mazuri na yapo faster, pia 1500 chenji zitakua zinasumbua sana.
View attachment 2239464
3000 hata AC hakuna na kuna nyakati mnajazana kama ng'ombe
 
Watapanda wenyewe
20220527_180210.jpg
 
Halafu mabasi yenye injini nyuma huwa hayakawii kuchoka

Huduma yenyewe ya hovyo bado wanataka kupandisha
 
Back
Top Bottom