Daudi Ballali's Death

Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.
serikali imeshatangaza rasmi msiba huu, au wanataka kututangazia kuwa alikufa ijumaa ilopita na mwili tayari umeshazikwa?

Serikali itatangazaje msiba while haijui aliko Balali? Hapa hamna Serikali upupu mtupu ndugu yangu. Sielewi hawa jamaa huwa wanafikiri nini!
 
jama hii ni changa la macho, wanatuweka sawa kabla ya tume kutoa taarifa ya uchunguzi wake (kumbukeni ukamilifu wa uchunguzi uko ukingoni) KIKWETE UNAHARIBU NCHI.... BALALI HAJAFA

Mimi binafsi sishangai watu kutoamini hii taarifa. Hii ni kwa sababu tumekuzwa katika mfumo ambao hatukuzoea kumuamini mtu mwingine isipokuwa serikali. Ndio maana MKJJ alituonya kuhusu Amina tukamkatalia na kumkebehi lakini waliposema serikali ndio tukakubali. Vilevile tulijua kwamba mwalimu alifariki siku kadhaa lakini hatukuamini hadi tulipoambiwa na Mkapa! Hapa nako tunasubiri kuambiwa na akina Salva ndipo tukubali kwamba Balali kafa. Ndivyo mifumo ya kifashisti na kidikteta inavyofanya kazi: kuhakikisha kwamba ni serikali tu ndiyo inayokuwa na monopoly ya habari. Tuendelee kuwasubiri akina Salva.
 
Hivi inakuwaje kama balali ni mmoja wa guests 213 kwenye post hii au hata one of the members.

Dunia ni duara huzunguka jua na hujizungusha yenyewe pia. Balali aweza kuzunguka jua na hata kujizungusha mwenyewe.

Kama alivyosema invisible huu unaweza kuwa ni mwanzo wa picha yenyewe. Kifo chake chaweza kuwa ni mwanzo wa mafanikio ya Watanzania. Who knows what Mr President will say on balali after his dealth. Anaweza akajichanganya mpaka akaonekana u-zero wake ktk hili. Kama angeendelea kuishi yawezekana tungeendelea kusubiri aje aseme kiasi kwamba ingechukua muda mrefu sana. lakini sasa hatusubiri bali anything can come out in the recent days.

Kuhusu wosia au kiapo alichoacha kwa mwanasheria itategemea ujasili wa mtu aliyeachiwa kuutoa hazarani. Maana mafisadi wanaweza kumbalali pia na yeye. Sioni namna nyingine ya mwanasheria huyu kuutoa wosia huo hadharani zaidi ya kuupost hapa JF. Kiboko ya mafisadi.
 
Mimi binafsi sishangai watu kutoamini hii taarifa. Hii ni kwa sababu tumekuzwa katika mfumo ambao hatukuzoea kumuamini mtu mwingine isipokuwa serikali. Ndio maana MKJJ alituonya kuhusu Amina tukamkatalia na kumkebehi lakini waliposema serikali ndio tukakubali. Vilevile tulijua kwamba mwalimu alifariki siku kadhaa lakini hatukuamini hadi tulipoambiwa na Mkapa! Hapa nako tunasubiri kuambiwa na akina Salva ndipo tukubali kwamba Balali kafa. Ndivyo mifumo ya kifashisti na kidikteta inavyofanya kazi: kuhakikisha kwamba ni serikali tu ndiyo inayokuwa na monopoly ya habari. Tuendelee kuwasubiri akina Salva.

Mkuu Mkumbo

na hawa hajamaa... hii cinema yote ni kutaka watanzania tuchanganyane weeee na kujichanganya ili wao wajipange vzr

Halali mtu hapa WATZ wa leo si wa jana
 
Ndugu kukaa kimya maana yake ni kuwa
Wanajua kuwa Balali hajafa, ila serikali inatafuta jinsi ya kumkwepesha kwenye hii ishu ambayo inataka kulitibua Taifa

Hakuna kifo hapo jamani, mnadanganywa, hii ndio inapoof kuwa sisi ni wadanganyika kweli

Yaani kirahisi hivi " Balali hatunaye tena" then mnaamini tu, Balali ni mtuhumiwa mkubwa sana nchi mwetu, hivyo habari zake zinatakiwa kuwa wazi wazi naza kuaminika, sio kirahisi namna hiyo

Pili si walisema hawajui halipo? , sasa iweje waseme hamekufa, wamejuaje??

Poor Goverment na wananchi wake kweli ni vichekesho
 
sawasawa Mkuu Mtanzania, iweje wana ndugu wawe kimya hivyo? au wanafumbwa mdomo? kuna kitu, Ndugu na Serikali wanakijua zaidi... what is that?

Haya ndiyo mambo ambayo tunapigania ikiwa ni kuhakikisha kuwa tunatofautisha mambo ya serikali na binafsi. Hawa wanafamilia wamekuwa watu wa ajabu sana tangu Balali augue kwa kukubali habari za ndugu yao zihodhiwi na serikali.
 
Nilisikia kwamba aliwaeleza mawakili wake kuhusu sakata zima la BoT pamoja na wahusika wake na yeye alihusika kwa namna gani, ikiwa ni pamoja na kuwapa nyaraka muhimu zinazothibitisha yote hayo. Sasa kama kafa hao mawakili wako wapi walete hizo taarifa humu kwenye jamvi?
 
Kuhusu wosia au kiapo alichoacha kwa mwanasheria itategemea ujasili wa mtu aliyeachiwa kuutoa hazarani.

Hakuna mwanasheria mwenye huo ujasiri TZ. Kama yeye alishindwa kujitutumua tena akiwa nje ya nchi, itawezekanaje mwanasheria wake aweze? Tena mwanasheria, kuna watu waoga kuwashinda wanasheria?
 
Mimi binafsi sishangai watu kutoamini hii taarifa. Hii ni kwa sababu tumekuzwa katika mfumo ambao hatukuzoea kumuamini mtu mwingine isipokuwa serikali. Ndio maana MKJJ alituonya kuhusu Amina tukamkatalia na kumkebehi lakini waliposema serikali ndio tukakubali. Vilevile tulijua kwamba mwalimu alifariki siku kadhaa lakini hatukuamini hadi tulipoambiwa na Mkapa! Hapa nako tunasubiri kuambiwa na akina Salva ndipo tukubali kwamba Balali kafa. Ndivyo mifumo ya kifashisti na kidikteta inavyofanya kazi: kuhakikisha kwamba ni serikali tu ndiyo inayokuwa na monopoly ya habari. Tuendelee kuwasubiri akina Salva.

Kitila mkuu sii kwamba siamini ila tuu hapa kumetokea mchezo naamini kabisa huju jamaa kafa na ninaamuni kabisa serikali ndio imemuua kutokana na hizi episods hapo chini hebi zisome

--------------------------------------------------------------------------------

Jamani someni hapa ili mjue ni kiasi gani serikali ilikuwa inatuandaa na taarifa za ukatili huu au uongo huu kwa wananchi wake

SERIKALI DAMU YA BALALI IMEBAKI MIKONONI MWENU mmezoea sana nyinyi kuua, kolimba, mtoto wa malechela, amina chifupa na wengine weeeeeeeeeeeeeeeeeengi sana kwaharaka siwezi kuwakumbuka sasa this has to be put to an END, hata mtuhumiwa nahaki ya kuishi

KIKWETE nakuona sana jinsi unavyotafuta sifa za kinataifa na kujisafisha kwaajili ya 2010. kwa hili la BALALI UMEJIHARIBIA,KABISA, TRUST ME.............amasivyo ongea

ni kwanini MKULO alisema alienda kumtafuta nani alimtuma, na alienda kumtafuta yeey kama nani

Salva alikuwa anamaana gani kusema serikali hainahaja ya kumtafuta BALALI na kwamba wakimuhitaji watampata

na kama milivotutangazia kwamba hamumtafuti kwanini makachero walienda kumtafuta kimya kimya bila huyo Salva kutangaza

Na mwisho kabisa mara gafla wakati kisunguzungu huchi cha Mkulo na Salva hakijaeleweka BALALI awe amekufa??????????
 
Nilisikia kwamba aliwaeleza mawakili wake kuhusu sakata zima la BoT pamoja na wahusika wake na yeye alihusika kwa namna gani, ikiwa ni pamoja na kuwapa nyaraka muhimu zinazothibitisha yote hayo. Sasa kama kafa hao mawakili wako wapi walete hizo taarifa humu kwenye jamvi?

Nasema hivi tusahau hilo. Yeye kama amekufa amekufa na habari hizo na watu leo huko Dar watakuwa wamechukua likizo wakajipongeze. Hakuna watu waoga wa mapambano kama wanasheria. Tena woga wao ni hatari zaidi maana ni wa kufundishwa!
 
Acheni kudanganyana nyie jamani
Mbona sisi watanzania ni wepesi kuamini namna hii jamani, vielelezo vya kifo viko wafi, wapi mwili wake, maana hiyo ndio proof tu.

Hivi mbona sisi wepesi namna hii jamani, na tutakuwa tunadanganywa kila siku tu, na kuibiwa

Kwa dunia ya leo mkuu hivi vitu unavyodai (vielelezo, mwili) waweza kuvipata hata huyo mtu hajafa nawakazika huo mwili. Inategemea wahusika wa msiba wanamalengo gani. Tuko ktk dunia ya uharibifu.

nani anajua rafiki wa Balali hasa wa marekani? balali ni kiboko yao anamarafiki wenye kuihadaa dunia I know one of them. Walifanya kazi wote WB ni matapeli mwisho. So anything can happen na hata serikali ya JK inaweza kupigwa changa la macho vile vile na kuishia kusema wanajua/hawajui balali aliko ili kuficha aibu ya changa la macho walilopigwa na kijana wa mjini balali. Ni aibu selikari kusema Balali haijui aliko ndo maana inajibaraguza kusema tukimtaka tutampata lakini kiuhakika haijui aliko na wameingzwa mjini na mtoto wa mjini Balali.

Taarifa ya kwanza ya serikali juu ya kifo cha Balali isikilize kwa makini you will know what is inside it.
 
Hakuna mwanasheria mwenye huo ujasiri TZ. Kama yeye alishindwa kujitutumua tena akiwa nje ya nchi, itawezekanaje mwanasheria wake aweze? Tena mwanasheria, kuna watu waoga kuwashinda wanasheria?

Ndio maana tunawaomba hao wanasheria waoga waweke hizo data humu ndani halafu waone kama hazitafanyiwa kazi.
 
Kwa dunia ya leo mkuu hivi vitu unavyodai (vielelezo, mwili) waweza kuvipata hata huyo mtu hajafa nawakazika huo mwili. Inategemea wahusika wa msiba wanamalengo gani. Tuko ktk dunia ya uharibifu.

nani anajua rafiki wa Balali hasa wa marekani? balali ni kiboko yao anamarafiki wenye kuihadaa dunia I know one of them. Walifanya kazi wote WB ni matapeli mwisho. So anything can happen na hata serikali ya JK inaweza kupigwa changa la macho vile vile na kuishia kusema wanajua/hawajui balali aliko ili kuficha aibu ya changa la macho walilopigwa na kijana wa mjini balali. Ni aibu selikari kusema Balali haijui aliko ndo maana inajibaraguza kusema tukimtaka tutampata lakini kiuhakika haijui aliko na wameingzwa mjini na mtoto wa mjini Balali.

Taarifa ya kwanza ya serikali juu ya kifo cha Balali isikilize kwa makini you will know what is inside it.
Nakubaliana na wewe kabisa kwa sababu Serikari walivyogusiwa kuhusu huu mchanga wa macho hawakuamini sasa wametuma makachero wao nasasa wanayaona mazingaombwe
 
WanaJF mlioko DC, MD au VA hebu fuatilieni nyumbani kwake huko Bethesda si ajabu mkamkuta mzima wa afya anapeta...
 
Believe me watanzania na serikali yao wameingizwa mjini na mtoto wa mjini balali. Waombe ufanyiwe DNA huo mwili kubaini kama ni Balali kweli na waufanye wao na siyo wamarekani. Balali ni mwisho
 
Ndugu wananchi kwasababu anayedaiwa kuwa marehemu alikuwa ni mtuhumiwa..Then tuna kila haki ya kuuhitaji ushaidi wa mwili wa marehemu kabla hatujaamua kufunga makabrasha yetu!

hata mimi hapo ninakubaliana na wewe mkuu, lazima mwili wake urudi kwa tanzania tena kwa kutumia vile vijecenti vye2 walivyo kwiba
 
Utashangaa ndugu zake watakuwa wanalia ktk msiba ili kuendeleza libeneke la changa la macho kwa watanzania na serikali yao
 
"Habari za hivi karibuni zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili, zinaeleza kuwa, wafanyabiashara, baadhi ya viongozi wa juu serikalini na wale waliostaafu, kwa siku kadhaa sasa wamekuwa wakihaha kuhakikisha kuwa Dk. Ballali harejei nchini."

"Kwamba, mikakati ya viongozi hao ni pamoja na kuhakikisha kuwa hata kama Dk. Ballali akirejea, hafanikiwi kivifikia vyombo vya habari au vile vya sheria kwa sababu, hatua hiyo inaweza kuibua kashfa kubwa kwa serikali"

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=9254

halafu uniambie ni kwanini nisiamini kuwa hao viongozi wa serikali wahajamuua
 
Acheni kudanganyana nyie jamani
Mbona sisi watanzania ni wepesi kuamini namna hii jamani, vielelezo vya kifo viko wafi, wapi mwili wake, maana hiyo ndio proof tu.

Hivi mbona sisi wepesi namna hii jamani, na tutakuwa tunadanganywa kila siku tu, na kuibiwa
Hahaha,,, kazi ipo!

Ila kuna siku utaamini tu ndugu yangu. Naona hata Tanzania Daima la leo wameandika kama inavyoonekana hapa chini.

Ni gazeti pekee la Bongo (nadhani) ambalo limeweza kuziandika hizi habari na kwa taarifa nilizopata toka kwa watu wangu wa karibu ni kuwa mtaani almost limeisha.
 
Attachments

  • Ballali_2.jpg
    Ballali_2.jpg
    139.5 KB · Views: 150
  • Ballali_.jpg
    Ballali_.jpg
    178.4 KB · Views: 142
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom