Daudi Ballali's Death

Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.
Hahaha,,, kazi ipo!

Ila kuna siku utaamini tu ndugu yangu. Naona hata Tanzania Daima la leo wameandika kama inavyoonekana hapa chini.

Ni gazeti pekee la Bongo (nadhani) ambalo limeweza kuziandika hizi habari na kwa taarifa nilizopata toka kwa watu wangu wa karibu ni kuwa mtaani almost limeisha.

Mimi Invisible ninahitaji kupewa vigezo vya kuaminika, na sio habari hizo za ajabu ajabu, nakuamini katika kutoa habari, lakini katika hili bado kidogo.

Kama JK aliomba waandishi wa habari waandike mambo ambayo hayako, inashindikana vipi kutengeneza hii habari?

Sio mwepesi wa kuamini habari, kwa sababu habari nyingi kutoka katika serikali ya kisura ni za kupika pika tu na hazina ukweli wowote sometimes
 
baba H, NAONA HAPO TUPO PAMOJA,MIMI NTAAMINI PINDI NIKISIKIA MWILI WAKE UMERUDISHWA BONGO KWA MAZISHI
 
Hahaha,,, kazi ipo!

Ila kuna siku utaamini tu ndugu yangu. Naona hata Tanzania Daima la leo wameandika kama inavyoonekana hapa chini.

Ni gazeti pekee la Bongo (nadhani) ambalo limeweza kuziandika hizi habari na kwa taarifa nilizopata toka kwa watu wangu wa karibu ni kuwa mtaani almost limeisha.


Mkuu nilishakwambia tumezoeshwa kwamba habari lazima zitoke serikali. Hawataamini hadi serikali iseme!!
 
Hapa kilicho kufa ni jina tu.

Hila mwili wake na roho bado vipo. Tuendelee kuomba serikali ilete mwili wa mfanyakazi wake. Unless waseme aliondoka na rafiki na jamaa zake, at hakuwa mtanzania.

Tungeomba kutoa salamu za mwisho kwa mtu aliyetumikia taifa letu kwa muda aliokuwa hai.
 
Ni Kweli Bwana Hizi Habari Wametangaza Hata Bbc, So Subirini Hadi Serikali Itakapowatangazia Ndo Muamini Siye Wakati Huo Tutakuwa Tunaanua Matanga.
 
Hata TBC1 (RTD), RFA na Radio One "wameikwepa" habari hii mchana huu!
 
Mkuu nilishakwambia tumezoeshwa kwamba habari lazima zitoke serikali. Hawataamini hadi serikali iseme!!

Wala mimi sihitaji kuamini kutoka kwa serikali, kwani serikali ndio waongo mpaka basi jamani

Ninachotaka mimi, ni mwili wa Balali uletwe Bongo na watanzania tushuudie kuwa huyu ndiye balali

Sio habari za kuambiwa balali amekufa, wakati serikali juzi tu imesema haijui halipo huyu Mwizi Fisadi, na wanasema mazishi yanafanyika Marekani!!

Changa la mamcho jamani
 
Sasa wakuu hebu tuwe watu wazima, according to the dataz........Mkono ndiye mwanasheria wake mpaka hii leo, yaani oficially!
Sasa hebu waandishi mtafuteni Mkono, ili aseme kama client wake amekufa, maana ninajua kuwa majuzi alionekana mahali akibadilisha vitambulisho, ambavyo ndani yake ameweka jina jipya, tuache uvivu ndugu zetu wa media mtafuteni Mkono....!


ikiwa MKONO ndiye mwanasheria wake!! basi inatupasa kuamini yale yote yaliyozungumzwa na MMkj ya kwamba Balali hatunaye tena
 
Balali ni nani mbona kifo chake kimekuwa siri sana!mbona hayati Rutihinda kifo chake hakikuwa siri na alikuwa Gavana pia?ila serikali ilisema haimtambui balali maana si mfanyakazi wao tena!Balali itakuwa umekufa na siri nzito!
 
Mkuu nilishakwambia tumezoeshwa kwamba habari lazima zitoke serikali. Hawataamini hadi serikali iseme!!

Kitila
unajua bado tuna mawazo ya kijima kwamba hadi itangazwe na Kamishina wa wa pilisi kanda maalum DSM,kwamba vyanzo vingine ni uongo na nasikia hiyo TBC Taifa tunayoiaminia hadi saa 7 mchana hakuna taarifa.
Huyu Balali kwanza alikuwa Ishu,na wananchi walikuwa wakimhitaji arudi,kwa hiyo lazima kuwe na kigugumizi.
 
Dah si wabongo kiboko.......fisadi kafa lakini bado tunashuhudia sifa zake kemkem ooh alikuwa mchapa kazi dah hii kali sasa
 
naona mmafisadi wamefunga bao la mkono hapa!
fisadi moja walalahoi sufuri
 
Rest In Peace Ballali Yanayotokea Yalishatabiriwa Hata Kiabla Hujaondoka Kwenda Us......ukute Wamekupa Ile Poison Kuua Taratibu...ile..ile............
 
Kwa nini tunakataa kwamba balali hajafa?

Ni juzi tu tumesikia anasakwa. Leo amekufa, ina maana wale waliokuwa wanamsaka walikuwa wanasaka nini? Au hii taarifa haikuwa sahihi?

Kwa nini wahusika wanapata kigugumizi ktk kutangaza? Kifo huwa hakijifichi. Hivi serikali walikuwa hawamlipi mshahara? maana ninachojua hakufukuzwa kazi serikalini.
 
Jamani ya kweli haya??
Mbona imekaa kisirisiri sana?? Tuamini kipi?? Serikali inasemaje? mkono mrefu wa kumsaka popote ndio huo? Mh, hata haiclick ubongo wangu.
Let see.
 
Kweli hiki kijiwe ni kiboko! Wakuu humu hamna mchezo. Big up
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom