Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.
Pia tunahitaji tujue rights za ilegal immigrant vs legal!
Serikali yetu haifahamu resolve baadhi yetu tuliyonayo!
Wamarekani Watueleze why didn't them deport an illegal immigrant!
Na kama alikuwa hospital...Then kwanini hawaibani serikali yetu kushirikiana na wananchi?
Kwa niaba ya wananchi wa Tanzania...Tutawauliza wananchi wa marekani!
Hii ni ili kuweza kuudumusha huu tunaouhita mshikamano!
 



Asante sana jmushi.
 
It gets hot up in here when the lawyer meets the space engineer watazamaji.



Kuhani



MWK
 
Mwafrika wa Kike,

Kuna wakati unatetea vitu haviteteeki. Halafu unatetea watu fulani wale wale. Nashindwa kuamini ukweli wako wa kimawazo (intellectual honesty).

Mwanzoni Mkuu alisema hivi:

sisi watu weusi hilo n word linatuathiri vipi? usijifanye una uchungu sana kiasi cha kulazimisha hoja kwa matusi. JF is bigger and stronger na hatuwezi kuvumilia matusi. Jenga hoja isimame au endelea kuuliza maswali.

Halafu, ilipooneka position controversial, akajieleza hivi:

well you are right...kujifafanua zaidi siwezi lakini sikwaziki mtu yeyote akitumia neno hilo dhidi yangu kwani ni mtu mweupe ndiye anafikiri litaniumiza au kwamba ni magic word ambayo inamgeuza mtu mweusi... not I.

Huwezi kutetea hapo kwamba Mkuu kachemsha ku suggest kwamba N word ni poa tu likitumika hapa.

Halafu kuuliza sometimes kunaweza kuwa suggestive. Unakumbuka Mkuu wa Harvard Lary Summers alivyotimuliwa kwa kuuliza swali – kwa kuuliza – kama inawezekana Wanawake hawakuumbwa kumudu Hesabu na Sayansi?
 

Mkuu wangu kuhani,

Nilichoona ni hiki:

sisi watu weusi hilo n word linatuathiri vipi? usijifanye una uchungu sana kiasi cha kulazimisha hoja kwa matusi. JF is bigger and stronger na hatuwezi kuvumilia matusi. Jenga hoja isimame au endelea kuuliza maswali
.

Hili kwenye bold ni swali,

Na kisha nikaona hiki:

well you are right...kujifafanua zaidi siwezi lakini sikwaziki mtu yeyote akitumia neno hilo dhidi yangu kwani ni mtu mweupe ndiye anafikiri litaniumiza au kwamba ni magic word ambayo inamgeuza mtu mweusi... not I.

Maelezo kuwa Mkjj hakwaziki na N word....

je unapinga na hili pia?
 
Mwafrika wa Kike,

Tuiue ishu. Kina Pundit wachonganishi ndio wanafaidika. Waliotoa ma statement na waliokwazwa hawapo.

E bwana Chenge yu hai?
 
Kwa hiyo hilo tusi langu lililowakwaza wewe na mwanakijij ni lipi?
Ili tuweze kujua ni yapi hayo yanayomkwaza nani na kwanini!
 
Mwafrika wa Kike,

Tuiue ishu. Kina Pundit wachonganishi ndio wanafaidika. Waliotoa ma statement na waliokwazwa hawapo.

E bwana Chenge yu hai?

Usijali mkuu.... ten more minutes then I will be off na utakuwa na jamvi lote for yourself.

Chenge "bado yu hai" kulingana na kumbukumbu zangu!
 
Mwili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Daud Timoth Said Ballali (65) aliyefariki Ijumaa uliyopita umehifadhiwa katika Nyumba ya Maziko ya De Vol iliyoko mjini Washington DC, nchini Marekani ambako inasubiri mazishi siku ya Ijumaa.

Taratibu za ibada na mazishi ambazo KLHN imepata nafasi ya kuziona inaonesha kuwa Gavana Balali alifariki tarehe 16 hapo Washington DC na atazikwa hapo hapo siku ya Ijumaa. Misa ya kumwombea Marehemu itafanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Stephen Shahidi mjini Washington DC anuani yake ni ST. STEPHEN MARTYR CHURCH 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington, DC 20037.

Ibada hiyo ya mazishi itaenda sambamba na kuuona mwili wa Marehemu kuanzia saa nne asubuhi. Hata hivyo shughuli hiyo nzima ni kwa ndugu, jamaa, na marafiki wa karibu na si kwa hadhara ya kila mtu atakaye kushiriki.

Marehemu atalazwa katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, MD. Hata hivyo haijajulikana kwa uhakika kama mwili wa marehemu utazikwa ardhini kama ilivyo desturi ya kiafrika au utateketezwa kwa moto kwani makaburi hayo yanatoa huduma hiyo pia. Kama ulikuwa ni usia wake kuteketezwa basi kwa kanuni za Kanisa Katoliki basi itafanyika mara tu baada ya ibada.

Kwa kanuni za Kanisa Katoliki mwili uliolazwa kwa njia ya kuteketezwa kwa moto mabaki yake (majivu) hawapewi familia, kusambazwa au kugawanywa katika mafungu madogomadogo na badala yake ni lazima viwekwe ardhini au kwenye sehemu maalumu inayotumika kwa maziko ya namna hiyo.

Dr. Ballali ambaye amefariki akiwa amezungukwa na wingu kubwa la kashfa dhidi yake na dhidi ya taasisi aliyoingoza inasemakana aliacha usia uliotaka atakapofariki basi azikwe Marekani. Hata hivyo pamoja na kashfa nyingi zilizoandikwa na vyombo mbalimbali vya magazeti na kutangazwa majukwaani Bw. Ballali hakuwa mtuhumiwa yeyote na hakukuwa na kesi yoyote ile ya kihalifu dhidi yake na hivyo amekufa kama raia na mtu huru.

Hata hivyo Dr. Balali ilidaiwa kuwa aliandika barua ya kutaka kujiuzulu kutokana na hali mbaya ya kiafya uamuzi ambao haukujibiwa hadi pale taarifa ya uchunguzi wa EPA ilipotoka na Rais Kikwete kutengua uteuzi wake kama Gavana wa Benki Kuu. Hata hivyo, taarifa ya Rais iliyosomwa na Katibu Mkuu kiongozi haikusema kama Gov. Ballali ni mhalifu, anatafutwa, au kwa namna yoyote ile amefanya makosa ya kisheria.

Hilo lilithibitishwa siku chache zilizopita ambapo Ikulu walitangaza kuwa walikuwa hawamtafuti Ballali na ya kuwa kokote alikokuweko alikuwa ni “mtu huru”.

Ni kwa sababu hiyo basi ibada ya mazishi inatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiongozwa na Balozi wa Tanzani nchini Marekani Bw. Ombeni Sefue, watumishi wa idara mbalimbali alizowahi kuzitumikia ikiwemo IMF, ndugu zake ambao wamewasili siku chache zilizopita, na baadhi ya Watanzania kadhaa waishio maeneo ya Washington DC.

Gavana Ballali ameacha mke na familia.

Raha ya milele umpe ee bwana
Na mwanga wa milele umuangazie
Apumzike kwa amani.

Amina.


WEKA SAHIHI KITABU CHA RAMBIRAMBI

NB: Taarifa hizi si rasmi na si za familia au mwanafamilia wa Ballali na hivyo zaweza kubadilishwa wakati wowote ule bila ya maelezo. Ni matokeo ya uchunguzi wa KLHN International.
 
Ok baada ya hiyo commercial break....Maswali, Je Ballali tunaye au hatunaye, I mean kikwelikweli? Kafia wapi MA au MD? Aliwekewa mashine (sijui ni ya life support au?...iliyozimwa baadaye) wapi nyumbani kwake au hospitali? Inakuwaje dada Premi Kibanga, kwa mujibu wa habari za magazetini anadai Ikulu inaandaa rambirambi na itazituma baadaye, whatever that means? Mbona ugonjwa na umahututi haukuwa siri ila mauti ndio imekuwa siri, wahenga walisema "mficha ugonjwa mauti itamwumbua" sasa sijui mficha mauti ataumbuliwa na nini...Kaazi kweli kweli...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…