Daudi Ballali's Death

Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.
wahenga walisema "mficha ugonjwa mauti itamwumbua" sasa sijui mficha mauti ataumbuliwa na nini...Kaazi kweli kweli...

Dude u cracked me up!
 
Sipendi unafiki na sina haja ya kuambiwa taratibu!
Nani anafanya mapenzi hapa!
Ebu takini taimu zenu bana!
Kwanza mi nshachoshwa so i dont give a efyu si kei![/QUOTE]


this one....

Kwa kutumia fasihi ipi hiyo kumepelekea wewe kusema hayo maneno uliyo ya highlight ni matusi!?
Hivi hayo maneno hapo juu ni matusi kwa lugha ipi hiyo?
Maana si ulisema kuna lugha hazikukwazi?
Sasa hiyo hapo juu hainikwazi mimi!
 
Ama kama mtu akaja na jina lake hapa jf akasema yeye ni efyu na baba yake ni sikei we utasema ni matusi?
Ama kuna mengine yakukwazayo?
 
Mi nakwambia nitawabana mpaka wajue kweli Tanzania mpya si ya zamani!
Tatizo hapa ni kwamba...Kama serikali yetu haitupi ushirikiano..Then wanafanya nini madarakani?
Mi naona hakuna tena muda wa business as usuall!
Kama hao washauri wa JK ni wazembe kiasi hicho..Then itamkosti Muungawana kwa namna isiyoweza kuelezewa!

Mkubwa kweli issue yako ipo Makini na ina leta maana ila sasa ndio atarudi? Hapa ndipo ujue kwamba hata Serikali ya Marekani wameshiriki katika huu ujinga .
 
Mkubwa kweli issue yako ipo Makini na ina leta maana ila sasa ndio atarudi? Hapa ndipo ujue kwamba hata Serikali ya Marekani wameshiriki katika huu ujinga .

Tutawabana Mkuu hawana pa kwenda!
Kesi sasa haitakuwa baina ya serikali yetu na serikali ya marekani!
Kesi sasa inaamishiwa kwa wananchi wa pande zote!
Kazi yangu mimi ni huku!
Na wengine waendelee na kazi huko bongo!
UNTIL JUSTICE IS SERVED!
 
Tutawabana Mkuu hawana pa kwenda!
Kesi sasa haitakuwa baina ya serikali yetu na serikali ya marekani!
Kesi sasa inaamishiwa kwa wananchi wa pande zote!
Kazi yangu mimi ni huku!
Na wengine waendelee na kazi huko bongo!
UNTIL JUSTICE IS SERVED!
excellent approach.
 
Na kama kuna watu wana siri ni bora wazitoe sasa hivi la sivyo mambo yakija kuwekwa wazi tutawajumuisha na wezao!
 
for public interent,
serikali ya kikwete na familia ya balali wanahitaji kutoa maelezo ya wazi (to make the oicture clear) kama jamaa amefariki.
mnavyokaa kimya mnazidi kuongeza mafuta kwenye mota huu wa hii kasumba.
umnavyoacha picha blank, yaani mnatuambia sisi tu fill inthe blank kutokana na information tulizokuwa nazo.
mimi binafsi naona kama hii imetengenezwa, ili tukubali halafu tuendelee tu na maisha.
Wanafamilia you need to appoint independent person to attend the funeral. Ili Balali kama kafa kweli watu wairuhusu roho yake ipumzike kwa amani. ama sivyo hakieleweki kitu hapa...... This is very disturbing
 
Mhmmmm!!! mpaka sasa hivi siamini, ila ni mimi tuu na mawazo yangu. Anazikiwa USA? ndivyo alivyoomba? na tutaambiwa kachomwa moto. Well!! Watu hawaruhusiwi kumuona! na huo usia alioandika haujataja na majina ya watu waliochukua hela BoT? At least angeacha hayo majina. Anyways! RIP, ila tuwe tunamuogopa Mungu kwa matendo yetu duniani.
 
Mwili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Gavana Ballali ameacha mke na familia.

Raha ya milele umpe ee bwana
Na mwanga wa milele umuangazie
Apumzike kwa amani.

Amina.
Hakuna cha kupumzika kwa amani wala amina hapa tunataka pesa zetu, wewe usitake kutuletea mambo ya kidini hapa... hata kama amekufa ipo siku tutamfukua tuu na mwishowe pesa zetu zirudi kwani hajazikwa nazo...
yani hapo juu umeandika kana kwamba huyu mtu aliyekufa alikuwa mtakatifu kumbe... ni MHARAMIA MKUU, ipo siku tugtawachoma moto barabarani wao pamoja na familia zao kama wazulu walivyofanya kwani hiyo ndio dawa...........
 
Kafia hospitali gani? Kwa ugonjwa gani?

Mtu ambaye aliwahi mpaka kuwa gavana wa nchi, wananchi wa kawaida hawawezi kwenda kumwaga?

Jamani jifunzeni, ufisadi kitu balaa kabisa. Hili linanikumbusha mazishi ya Maboutu.
 
safari yake imeisha!acha wafu wawazike wafu wenzao! sasa tugange yajayo
 
m/kijiji mmmmh
huyu bwana ni mhalifu, ametutendea madhila mengi. Ameuwa wengi kwa maamuzi, matendo, na wizi wake na mafadhihina wenzeke.

Mungu ametusaidia sisi watanzania wanyonge na anamuonyesha kikwete hata kama hataki kuwafikisha mahakamani na hatimaye jela mafedhuli wenzeka Kazi ya Mungu hawezi kuizuia.

Dito kauwa wakambeba. Balali kawa enginia wa wizi wakamficha sasa waende nao kaburini kuwalinda.

Mungu wa kweli atatoa adhabu ya kweli kutokana na matendo yetu.

Jasusi ni jasusi haitaji huruma ya jamii wacha liende.

Ili kusamehewa Yesu alimwambia Zakayo aende akagawe mali alizoiba kwa masikini, sasa balali hajarudisha alizoiba. Tuandamane kwa mabango siku ya mazishi yake kanisani kwani hakuna anayeweza kuzuia mtu asiingie kanisani.

Mabango juu asizikwe balali mpaka mali zetu zirudishwe.
 
•Kitendawili !

Joseph Lugendo na Reuben Kagaruki

HATIMAYE baada ya kimya kirefu juu ya alikokuwa akiishi aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dkt. Daudi Ballali, Serikali imethibitisha kwamba, alikutwa na mauti Ijumaa ya wiki iliyopita, Mei 16 mwaka huu mjini Boston Marekani na yenyewe ilichelewa kupata habari huku kifo chake kikiacha maswali mengi kuliko majibu.

Taarifa fupi ya uthibitisho wa kifo hicho ilitolewa jana jioni jijini Dar es salaam na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa BoT, Bw. Emmanuel Mwero, baada ya kutokea mazingira ya kutupiana mpira wa kuthibitisha kifo hicho, miongoni mwa maofisa mbalimbali za Serikali.

"Sisi hapa benki, tunaungana na familia ya marehemu Ballali kuomboleza msiba huu na kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Dkt. Ballali alijiunga na BoT kama Gavana Julai 14, 1998 hadi Januari 8, 2008 cheo chake kilipotenguliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Bw. Mwero alipoulizwa iwapo wanafahamu siku mwili wa Dkt. Ballali utakapoletwa nchini kwa ajili ya mazishi, alisema taarifa iliyotolewa inajitosheleza na kama kutakuwa na habari nyingine, wataitoa baadae.

Awali taarifa za kifo cha Dkt. Ballali zilionekana kuwa za usiri mkubwa kutokana na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo maofisa habari kurushiana mpira pale walipotakiwa kuzitolea ufafanuzi.

Gazeti hili lilipofika Wizara ya Mambo ya Nje ili kupata uthibitisho wa kifo chake, maofisa wake hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo. Katibu Mkuu,Bw. Patrick Mombo, alipoulizwa na waandishi wa habari kwa njia ya simu kama ana taarifa za kifo hicho, alisema juzi alizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Marekani lakini hakumpa taarifa hizo.

Aliwataka waandishi wa habari kuwasiliana naye jana saa 11 jioni kwa kuwa asubuhi majira ya saa 5 kwa madai kuwa muda huo Marekani ni usiku na watu wamelala.

Kutokana na utata huo, waandishi wa habari wa gazeti walibisha hodi kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu, hata hivyo taarifa zilizopatikana zilieleza kuwa alikuwa na mkutano.

Gazeti hili lilikwenda moja kwa moja nyumbani kwake alipokuwa akiishi Kitalu namba 387 Kata ya Msasani, Masaki nyumba namba msn/msk56 ambapo hakukuwa na dalili zozote za msiba.

Baadaye gazeti lilipata taarifa kutoka kwa chanzo cha habari kilicho karibu na familia hiyo, ambacho kilithibitisha kutokea kifo hicho.

"Ukiona mtu mwenye umri mkubwa anazungumza huku anatoa machozi ujue kuna jambo kubwa limemtokea," alisema mtoa habari huyo huku akibubujikwa machozi.

Kuhusu chanzo cha kifo chake, mtoa habari huyo alikataa kuzungumzia suala hilo kwa undani huku akitoa kauli iliyobeba ujumbe nzito ndani yake kuwa; "Serikali ina mambo mengi."

"Hapa nimepigwa pini (kuzuiwa) nisiondoke, nimeambiwa kuwa watakuja watu wengi wakiwemo wakubwa, kama unataka kuonana na ndugu au jamaa wa karibu, nenda Boko kwenye shamba lake, unaweza kupata taarifa zaidi," alisema huku akisisitiza kuwa kifo cha Dkt. Ballali kina mambo mengi.

Kuhusu siku ya mazishi na nchi atakayozikwa, mtu huyo alikataa kuzungumzia suala hilo. "Siwezi kusema zaidi, ni kweli habari mnazoulizia zimetokea ndio maana nimeamua kuwasaidia," alisema na kuwataka waandishi kuwasiliana naye baadaye.

"Siwezi kusema zaidi, ni kweli habari mnayoulizia imetokea, ni kweli kabisa, mimi nilitaka kukusaidia kama mwandishi, najua mpo kazini nadhani umethibitisha, labda uende ofisini kwake unaweza kupata taarifa zaidi," kilieleza.

Baada ya hapo, gazeti hili lilipiga hodi kwa mara ya pili ofisini kwa Bw. Rweyemamu na alipoulizwa kama taarifa za kifo cha Dkt. Ballali ni za kweli aliwataka waandishi wa habari kuvuta subira kwa maelezo kuwa kuna taarifa inatolewa na BoT au Wizara ya Fedha.

Alipoulizwa ni wapi alikuwa anaishi alisema ni Oysterbay karibu na Ubalozi wa Afrika Kusini, lakini alipodokezwa na waandishi kuwa wamefika nyumbani kwake na hakuna dalili za msiba alijibu; "Sasa hilo siwezi kujua kawaulize watu wa BoT hili sio suala la Ikulu bali ni la Serikali ngoja nikawaitie Mpenda (Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw Kassim Mpenda).

Akizungumza na waandishi wa habari, Bw. Mpenda ambaye alikuwa kwenye mkutano na Bw. Rweyemamu na maofisa wengine, alikiri kuwa Serikali inajua hilo, lakini wamekubaliana kuwa atakayetoa taarifa hiyo ni Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndullu.

"Na mimi nimeyapata gazetini kama ninyi subiri mtapata taarifa," alisema Bw. Mpenda. Waandishi wa habari walipofika BoT kwa lengo la kuonana na Gavana walielezwa na mmoja wa walinzi kuwa warudi tena BoT saa 8.30 ili kuonana na Mkurugenzi wa Itifaki.

Pamoja na waandishi kufika muda huo ilibidi wasubiri zaidi ya saa mbili ndipo baadaye, alitokea Bw. Mwero akiwa na taarifa yenye picha ya Dkt. Ballali ya kuthibitisha kifo hicho. Katika hali ya kushangaza hakutaka kuwapa nafasi waandishi wa habari ya kuuliza maswali ili kupata ufafanuzi mbalimbali.
 
•...Watanzania washtushwa usiri wa kifo chake


*Wapinzani watakaka, arejeshwe waone mwili


Na Reuben Kagaruki

WAKIZUNGUMZIA kifo cha Dkt. Ballali wananchi mbalimbali walielezea kusikitishwa na hatua ya serikali ya kuchukulia kifo chake kwa usiri mkubwa hali inayoibua maswali mengi ndani ya jamii.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania Labour Party (TLP) Bi. Nuru Kimwaga,alisema Watanzania wataamini kuwa amefariki ikiwa mwili wake utarejeshwa nchini na wakaushuhudia kwa macho yao.

"Tutaaminije kama amefariki au ni janja ya kutuuzia mbuzi kwenye kiroba?"alihoji, Bibi Kimwaga

Alisema serikali imekaa kimya muda mrefu bila kumchukulia hatua gavana huyo aliyehusishwa na kashfa ya EPA wala kubainisha alipo, wakati wakiendelea kutafakari, wanaambiwa amekufa.

"Inashangaza serikali imekaa kimya muda wote mbali ya wananchi kuhiji kila siku aliko Ballali na kutaka arudishwe nchini, leo ghafla tunaambiwa amekufa na anazikwa huko huko tutaaminije kama amekufa ? ,"alihoji Bi.Kimwaga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TPP-Maendeleo, Bw. Peter Mziray, alipinga vikali kauli iliyotolewa na Ikulu hivi karibuni kuwa serikali ilikuwa haijamhitaji Dkt. Ballali hivyo alikuwa na uhuru wa kuishi popote.

"Dkt. Ballali alikuwa akihitajika kwa sababu tangu Rais Jakaya Kikwete, alipomfukuza kazi alikuwa hajawahi kurejea nchini kukabidhi ofisi...alitakiwa arejeshwe nchini akabidhi ofisi kwani alikuwa akifanyakazi kwa mkataba," alisema Bw. Mziray.

Alisema Dkt. Ballali amefariki akiwa shahidi mkubwa kwenye sakata la ufisadi katika akaunti ya EPA hivyo kitendo cha Rais kumtimua bila kukabidhi ofisi kinaibua maswali mengi.

Mwenyekiti wa Democratic Party (UDP), Bw. John Cheyo, alisema kwa nafasi aliyokuwa nayo Dkt. Ballali wananchi walipaswa kujulishwa mapema kuhusiana na taarifa za kifo chake.

"Alikuwa na nafasi kubwa, watu walitakiwa kupewa taarifa mapema," alisema Bw. Cheyo.

Naye Mhadhiri katika Kitivo cha Sayansi za Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, alisema ilikuwa ni jambo la busara kwa serikali kutoa taarifa mapema hasa kwa kuzingatia taratibu zinazoendelea za kuchunguza yaliyojiri katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPE).

"Angalau serikali itoe tamko ili kuondoa athari zinazoweza kujitokeza na kuondoa watu wasiwasi ili wasitunge hadithi zinazohusiana na kifo chake," alisema Profesa Baregu.

Mkazi wa Kata ya Msasani, Oysterbay alipokuwa akiishi, Dkt. Ballali, Bw. Samwel John, alisema ni jambo la kusikitisha kwa mtu mkubwa kama Gavana taarifa za kifo chake kugeuzwa siri.

"Sisi tulikuwa tukiishi vizuri naye lakini hatuna taarifa sahihi kuhusiana na kifo chake ukimya huu unatufanya tujiulize maswali mengi," alisema Bw. John. Alisema kwa kipindi ambacho ameishi naye jirani alikuwa akishirikiana vizuri na watu ukiondoa kashfa iliyomkumba.

Hata hivyo alisema Dkt. Ballali amekufa na siri nzito hivyo serikali bado ina nafasi ya kueleza kilichojiri kwenye akaunti ya EPA. "Nina uhakika ushahidi wake ungeibua mambo mengi hasa ufisadi ndani ya BoT," alisema na kuitaka serikali kutoa taarifa kuhusiana na sababu za kifo chake.

"Sawa kifo chake kimetokea kimya kimya lakini wananchi tuelezwe nimesababisha kifo chake ili kuondoa hadithi za kufikirika ambazo wananchi wameanza kuzitunga," alisema Bw. John.

Mkazi mwingine, Bw. Haruna Moshi, alisema kifo cha Dkt. Ballali kisiwe mwisho wa kuficha yaliyojiri ndani ya EPA. Alisema watu wengi wanataka kujua mambo mengi hivyo uchunguzi inabidi uendelee ili wananchi waweze kujulishwa yanayojiri.

Mkazi wa Tegeta. Bi Yasinta alisema kwamba usiri mkubwa ulioko ndani ya kifo cha Dkt. Ballali na akahoji kwamba ni kwanini Serikali haikutoa taarifa juu ya kifo hicho wakati Dkt. Ballali alikuwa mtumishi wao wa muda mrefu mpaka hapo alipoachishwa na Rais Kikwete.

Hata hivyo Bi Yasinta aliishauri Serikali kutositisha uchunguzi kwenye akaunti ya EPA kwani unawahusu na mafisadi wengine waliokula fedha hizo.
 
Je, mafisadi wa CCM wameamua kutucheza kama John Darwin?

The TimesDecember 4, 2007

The 'dead' canoeist John Darwin, his wife and the Panama connection
Five years after the ‘drowning tragedy', missing man wanders into a London police station
Image :1 of 2

Andrew Norfolk, Rajeev Syal and Murad Ahmed
The wife of a man who disappeared in an apparent canoeing tragedy five years ago had moved to Panama and opened a new bank account only weeks before he walked into a police station to declare that he was still alive, it emerged last night.

Anne Darwin, 55, is understood to have emigrated to Panama City soon after the sale of two properties that she once jointly owned with her husband, John Darwin, who had formally been declared dead by a coroner.

Yesterday Mr Darwin, 57, a former teacher and prison officer, was preparing to be interviewed by detectives who want to know how he has survived in anonymity before he strolled into West End Central police station in Savile Row, Central London, last weekend. Police officers said he had no memory of what had happened.

The mystery of his wherabouts has baffled friends of the couple, who had belived that he had drowned off the Cleveland coast half a mile from his home in March 2002.

Bill Rodriguez, a former neighbour, said that when he last saw Mrs Darwin in August, she told him that she had just returned from a six-week holiday in Panama. "She said she loved it out there and was going to move out full-time," he said.

A former neighbour said that Mrs Darwin's departure six to eight weeks ago, had been extremely sudden.

"She left the house full of furniture. She left everything. It took them 15 skips to get the rubbish out," she said.

The Times understands that Mrs Darwin has "hundreds of thousands of pounds" in a Panamanian bank account, and had sent some of her furniture to the Central American state.

The bizarre story began on March 21 five years ago when Mr Darwin took his red canoe out to sea.

The couple had moved to a seafront house two years earlier with their dogs. Their sons, Mark and Anthony, had moved away and the couple told neighbours that they hoped to retire there.

The North Sea was said to be unusually calm that spring day. Mr Darwin was reported missing when he did not return home. Hours later his damaged boat was washed up on the sandy beach. A member of the emergency services who launched a fruitless 14-hour seach for Mr Darwin after his disappearance said last night that sea conditions had been as "smooth as a millpond". Tom Waller, 60, a member of Hartlepool Coastwatch, said that rescuers had been puzzled that the prison officer could have got into trouble in such conditions.

An extensive search operation was mounted along the coastline from Hartlepool to Staithes, North Yorkshire. No sign of Mr Darwin was ever found.

Six months after his disappearance, Mrs Darwin, a doctor's receptionist, told a local newspaper that she could not move on without seeing her husband's body. She said: "People die, have a funeral, they have a headstone, there is something to mark the fact they existed on this Earth. But without a body, I don't know how we can mark John's life.

"All I want is to bury his body. It would enable me to move on. It's difficult to grieve without bringing things to a close, but as it is I'm in limbo and there's nothing I can do."

An inquest was eventually held in April 2003, 13 months after his disappearance, and the Hartlepool Coroner recorded an open verdict.

The couple paid £170,000 in December 2000 for two adjoining properties on Seaton Carew seafront. Robert Meggs, the former owner, said the Darwins planned to live in one house while earning a £2,000 monthly rental income from the second, which was divided into 15 bedsits.

"They had been living near Durham but they used to come to Seaton regularly to walk their two rottweilers on the beach," he said. "Mr Darwin also told me that he was a keen canoeist. When they saw these adjoining homes for sale they thought it was their dream house."

Mr Meggs said that the couple owned a black Range Rover with a personalised number plate. Mrs Darwin had been "very striking" and appeared to be the dominant partner in the relationship, he said. Her husband had told him that he had a heart condition.

On the day that they moved in, Mr Meggs said he had been puzzled when Mrs Darwin confided in him: "If this doesn't work out, we'll lose everything."

Documents from the Land Registry show that Mrs Darwin transferred both of their properties to her son, Mark, in June 2006.

She continued to live in one of the houses, but one was sold in October 2007 for £295,000 while the other fetched £160,000 in March.

Yesterday afternoon two police officers called at one of the couple's properties to take away mail. The male and female uniformed officers spoke to John Duffield, 36, for about ten minutes. When he and his partner moved in, furniture had been left including wardrobes and settees. There were few personal items, he said, though "we did find Teach Yourself Spanish books in her study", he said.

Mr Darwin studied at the St Francis Xavier College in Liverpool. He wrote on the Friends Reunited website in January 2002, just weeks before his disappearance: "After leaving St Francis went to De La Salle College, Manchester, where I did biology and chemistry. Taught in Derwentside for 18 years before leaving teaching to join Barclays Bank. At present work for Prison Service and have portfolio of properties.

"Married to a convent girl Anne Stephenson, we have two grown-up sons and two dogs. Recently moved to Seaton Carew where I hope to retire soon."

This weekend, Mr Darwin reappeared at the Central London police station, looking tanned, refreshed and healthy. Inspector Helen Eustace, of Cleveland Police, said yesterday: "The guy can't remember anything about what's happened or why he's come forward. He has no memory at all. He has obviously been somewhere for the last five years and a lot of questions need answering."

He is believed to be staying with relatives in the South of England.

This weekend some of his relatives expressed relief that he had reappeared. His brother, David, speaking from his home in Barnet, North London, said: "All the family is so relieved that John is alive."

Mr Darwin's 90-year-old father, Ronald, of Blackhall Colliery, Co Durham, told a newspaper: "I always said to the police that there might be more to this than it appeared at first. When his canoe was found but he wasn't, it didn't seem right."

Mr Darwin said that when his son was 4 or 5 he was knocked down by a car and suffered a head injury, which could have caused amnesia later in his life.

"Now he's got his memory back," Mr Darwin said. "When I speak to him, I will ask him where he has been these last few years and I'll ask, ‘Why didn't you make arrangements to see me before now?'."

One relative was less supportive. Mr Darwin's aunt, Margaret Burns, said that her nephew had only once made contact with his father in the past 36 years, and that was on the day of his mother's funeral 16 years ago. She said that at the funeral he had boasted of owning 17 properties and predicted that he would be a millionaire by the age of 50.

Officers from Cleveland Police will meet Mr Darwin before Friday.

Detective Chief Inspector Paul Beddow said: "This has been a long-running inquiry by Cleveland Police and officers from the inquiry team hope to speak to Mr Darwin to establish his whereabouts."

Vanishing acts

John Stonehouse The former Labour Cabinet minister was presumed to have drowned after his clothes were found in a pile on a beach in Miami on November 20, 1974. He was, in fact, en route to Australia, where he hoped to swap his family and mounting debts for a new life with his mistress and secretary, Sheila Buckley. Having adopted the new identity of John Markham, he was discovered on Christmas Eve by Australian police, who thought initially that he might be the missing British aristocrat Lord Lucan. Stonehouse was eventually deported to Britain and imprisoned for his crime.

Karl Hackett Reported missing, presumed dead, by Lee Simm after the Paddington train crash in October 1999. Mr Simm maintained his story for a month and Mr Hackett's relatives attended a memorial service before it was discovered that the two men were the same person. It emerged later that Mr Hackett had been sentenced to 12 months' imprisonment for indecent assault in 1987, and had lived as Lee Simm since his release. He saw the Paddington crash, in which 31 people died and dozens were seriously injured, as an opportunity to kill off his former identity. In 2000 he received a suspended sentence for wasting police time.

Graham Cardwell A Lincolnshire dockmaster, Mr Cardwell was thought to have died in September 1998 after his belongings were found on mud flats on the docks where he worked. His grieving family members were somewhat surprised when he was discovered about eight months later very much alive and well, and living as a bachelor 200 miles away in the West Midlands. He claimed that he had decided to stage his disappearance after coming to believe that he was suffering from cancer.

Thomas Osmond Attempted to avoid standing trial for sex offences by faking his own suicide. The civil servant was thought to have killed himself by jumping off the Severn Bridge in March 1995, the day before his trial was due to start, and left a suicide note to support that version of events. One suspicious detective did not believe the father of three was dead, however, and kept on searching. He eventually discovered Osmond in Bristol three years later, where he had been living under the false identity of Stephen Williams. Osmond was sentenced to seven years in prison.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom