Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.

Kauli zingine hapa zinaashiria kama JF ina wenyewe kama ilivyo CCM. Tuonyeshwe mapema tu hayo mawe ya pembeni ili tuyakalie!
 
tatizo ni nini hasa? amekufa hajaaga au amekufa?

Given the very serious nature and extent of accusations Balali has been subjected to, its in the public interest to confirm WITHOUT ANY REASONABLE DOUBT that Balali is really dead.

Therefore many people aren't buying, won't buy and should not buy unfounded claims about Balali's purported death till they see his carcass (before they cremate it and bury/throw away the ashes on US soil of all places.)
 
Najiuliza kwa msoma risala awe kiongozi kutoka serikalini atasomaje risala katika mazishi ya balali. kama ni wewe ungefanyaje?
 
Halafu wandugu kuna swali moja la kuhusu dini ya Bw Balali!
Je ni Moslem ama mkristo?
Kwasababu kama ni Msilam then hakuna uwezekano wa kuonyeshwa sura wakati wa heshima za mwisho!
Na pia kama ni Muislam kwanini apelekwe Kanisani?
Daud Timoth Said Ballali,
Ni Mkristo wa dhehebu la Roman Catholic na imeandikwa atazikwa katika makaburi ya Kikatoliki ya Gate of Heaven.
 
TAtizo ni kuwa tunajaribu kumfikiri Ballali kama mhalifu. So far siyo mhalifu, amekufa akiwa mtu huru kabisa. Who is to blame for that..? Kwa hiyo atazikwa kwa heshima atakazopatiwa na hakuna mtu mwenye haki ya kudai kuuona mwili wake kama ndugu zake hawataki, hata serikali haiwezi, believe me... I made my moves the whole of yesterday..

But then.. as I promised.. wait for Friday... it is just tomorrow. Ukweli utajulikana tu na sehemu nyingine ya ukweli wiki ijayo kwenye ardhi ya nyumbani kwao.
 
Kauli zingine hapa zinaashiria kama JF ina wenyewe kama ilivyo CCM. Tuonyeshwe mapema tu hayo mawe ya pembeni ili tuyakalie!

Umemshtukia? Jamaa anatukana ovyo ovyo lakini anapeteshwa. Lakini hatishi, ni mtupu ile mbaya. Kadai moja ya sababu kwanini Billal hajafa ni kwamba hata yule m-bongo mcheza kikapu cha College hajui hicho kitu. Anasema, wazungu wa mji anako kaa jamaa wangekuwa wamemwambia dogo Ballali kafa. Yani sijawahi kusikia kituko kama hicho. Anyway, wazungu wanasema 'tuna samaki wakubwa wa kukaanga.' Tuachane na huyu dagaa, japo hapa JF ni papa.

Kibaya kikubwa ni kwamba Ikulu yetu inaongozwa na watu kama huyu jamaa. Muungwana eti nae akatumia muda wa Rais kumpa audience yule mtoto mcheza kikapu. Mtoto akaja kukutana na Rais kavaa ki hip hop na mkofia wa Baseball. Muungwana nae kakaa anapiga nae stori, mtu kakujia bila hata heshima. LOL. Yani hivi ninavyo andika sina mbavu japo nasikitikia nchi yetu.
 
haki wengine tunafuata maana haya maisha sasa badala ya kuwa mikononi mwa Mungu wapo binadamu wengine wanataka kujichukuilia jukumu la kuwatanguliza wengine mbele ya hukumu.
 
"Mke wa sasa Balali, ni dada wa mume wa dada wa mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima, ambalo ndilo limekuwa la kwanza kusema hizi habari.

....wakuu hiyo nayo inaniacha hoi.
 
"..Hata hivyo haijajulikana kwa uhakika kama mwili wa marehemu utazikwa ardhini kama ilivyo desturi ya kiafrika au utateketezwa kwa moto kwani makaburi hayo yanatoa huduma hiyo pia. Kama ulikuwa ni usia wake kuteketezwa basi kwa kanuni za Kanisa Katoliki basi itafanyika mara tu baada ya ibada.

Kwa kanuni za Kanisa Katoliki mwili uliolazwa kwa njia ya kuteketezwa kwa moto mabaki yake (majivu) hawapewi familia, kusambazwa au kugawanywa katika mafungu madogomadogo na badala yake ni lazima viwekwe ardhini au kwenye sehemu maalumu inayotumika kwa maziko ya namna hiyo."

...Wakuu chekini na hiyo kwamba kuna possibility ya mwili kuchomwa moto sasa if that is the case then hata ushahidi hatutakuwa nao kama kweli balali amekufa au ni changa la macho.
 

Mkuu mi namchukulia Balali hakua na hatia ya ufisadi....hata angeenda mbele ya sheria zetu na kukawa na haki.
Namuombea kwa Muumba wake apate haki yake kama aliikosa hapa duniani.
 
jeuri ya pesa kuzikana ugaibuni, huyi alisaliti mpaka wazazi wake kwa haya yote aliyoifanyia tanzania.
 
 
Mkuu kaandamane kwenye nyumba ya Balali uone kama hukulala lupango, ninasema hivi Balali yupo mzima wa afya hajafa, ndio mchango wangu katika hii topic je wewe hoja yako ni ipi maana so far siioni zaidi tu ya taarabu?

Naona unabadili majina tu kama kawaida yako hoja huna? Tunasema hivi katika kutafuta dataz huwa tunatumia watu wengi sana na huyu Hasim the big star anaweza kuwa mmoja wao kutufikisha sehemu ambazo wewe mlalahoi huwezi kufika kwenye kutafuta dataz za "kifo" cha Balali, ndio maana tunarudia kuwa Balali hajafa,

Naona kama kawaida yako hoja wala dataz, licha ya facts huna on the ishu ila una nyimbo nyingi sana za taarabu na kubadili majina, mkuu hapa hupawezi kabisa, labda tujaribu Darhotwire! Maana kama ujuha sidhani kama kuna unaozidi wa kuimba taarabu kwenye topic nzito kama hii,

Haya tunasubiri maandamano yako kule DC nyumbani kwa Balali, what a clown!
 
Badungu

naomba mniwie radhi lakini sitaki kuwa mnafiki ukweli ni kwamba sijaona huzuni yoyote katika moyo wangu kwa kifo cha huyu bwana (kama kweli amekufa) hasa ukutilia maanani kuna watoto wadogo wengi hapa TZ ambao hawana hata doa la dhambi wanakufa kwa huduma duni za afya na umasikini iliokithiri ambao hatustahili kuwa nao

kinacho nisikitisha ni kwamba ameondoka na ameacha maswali mengi ambayo hayajajibiki na kifo chake kinatufanya tijiulize kulikoni......mwanzo ilikuwa Salome ikisha....Balali na wote hao ni watu muhimu kwa EPA. sijui nani atafuatia.....labda CHENGE.... au EL

nadhani MAFISADI waliobaki na iwe fundisho kwao kama kweli Balali amekufa jee anaondoka na nini vipo wapi vijisenti vyake? yako wapi mahekalu yake... na je yamemsaidia nini katika hali hii ya UMAUTI????
 
Balali is dead , kwa wale ambao hamtaki kuamini hebu tupeni sababu kwa nini mnataka wengine waamini kuwa huyu hajakufa?

Zitawekwa picha humu juu ya atakavyokuwa akionekana kwenye geneza na pia za uchunguzi wa hospitali ...subira huvuta kheri.
 
ivi watu kama hawa si huwa wanzikwa kwa heshima fulani? sasa eti mtu aliyekuwa na nyadhifa kubwa anazikwa kimya kimya!! duh hapa lazima kuna kitu waungwana mtu kama huyu naye tulitegemea angerudi zake unyamwezini na kwenda kwao akisubiriwa kwa shangwe ila yeye imekua tofauti.
Hapa bwana bwana JK lazima ajiangalie sana.
 
Nahisi "marehemu" alikuwa na hoja nyingi za kujibu.

Kwa vyovyote Taifa limepata hasara kubwa akiwa madarakani pale BOT na hasara iliyopatikana inawakilisha athari hisiyohesabika inayowaliza mamilioni ya Watanzania masikini.

Lakini cha kushangaza kauli za viongozi wetu,Serikali yetu hazijawahi kuonyesha hata chembe kama walikuwa interested kujua chchote ambacho marehemu alikijua au alihusikaje na kashfa za pale BOT. Ah inawezekana hasara aliyoliingizia TAIFA inaangaliwa "from VIJISENTI POINT OF VIEW"

Inawezekana marehemu amekufa kwa sababu serikali ilimtelekeza akiwa mgonjwa na kumuongezea mshtuko kwa kumfukuza kazi.

Kwa nini marehemu amezikwa ughaibuni, ni ndugu zake wameamua au ni usia wake?! Well, kama ni usia wake basi labda hakuwa anaipenda nchi yake., by the way angeipenda nchi yake labda asingekuwa maarufu sana wakati huu.. yasingetokea yaliyotokea pale twin towers 2005.

Ah kwa upande mwingine naona yote sawa tu maisha yenyewe ni mafupi...!

Oh nafikiri sio vizuri sana kumsema vibaya mtu aliemaliza safari hapa duniani. Basi Kama kawa ngoja tuhitimishe kwa kusema marehemu alikuwa mtu mzuri, mpenda watu na anaeipenda nchi yake. Marehemu alijituma sana kuhakikisha nchi inakuwa kiuchumi na kiwango cha maisha ya mtanzania kinapanda. Alisifika sana kwa uwazi na ukwei na jinzi alivyokuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi, nepotism, na uhujumu uchumi. Msimamo wake wa kuhakikisha mali za TAifa zinatumika kwa maendeleo ya Taifa na wananchi ndio umesaidia kuliokoa taifa dhidi ya viongozi wenye tamaa ya fedha na rasilimali za nchi.

Mungu mwenye haki na amlaze marehemu mahali anapostahili kulazwa.

AMINA
 
Swala linalonisumbua akili ni kwamba....Ballali kama "respected public fugure" wa Tanzania....
aje Marekani kwa matibabu....
tusitangaziwe sisi waTanzania tuishio kwenye mji wa hiyo hospitali....
halafu afariki dunia....
pia ubalozi usitoe matangazo yoyote kwa muda wa zaiai ya wiki moja....
habari za mazishi pia ziwe na utata....mpaka watu wanakaribia kushikana mashati ndio zitolewe....
Halafu....maandalizi ya mazishi yake yanakwenda kwa kasi sana.
Sisi waTanzania mara nyingi mtu kama Ballali tungependa kumsindikiza kwa heshima zote....na kuusafirisha mwili wake uende nyumbani kwani yeye hajaishi Marekani miaka mingi na pia amelitumikia taifa kwa muda mrefu na kwahivyo anastahili kupewa heshima hasa wakati wa mauti yake.
Hakuna tangazo lolote "credible" kutoka kwenye balozi zetu hapa Marekani linalotoa maelezo ya kuuaga mwili wa marehemu Mr. Ballali...bali tu kwamba...."atazikwa Ijumaa"................
Kwa hiyo....lazima niweke Alama ya Kuuliza".....kwanini kuna usiri kwenye mauti yake?
 

Mkuu FME,
Nakubaliana nawewe asilimia miamoja, sina data zaidi ya kutumia tu hekima ya kuona zengwe lililo gubika taarifa za kifo hiki kwamba ni usanii wa hali yajuu kutaka kufunika soo la EPA,

Myezi sita ya uchunguzi inafikia ukingoni, watueleze nini basi? njia iliyo onekana bora ni kumwambia Ballali kwamba tuna tangaza umekufa mchezo uishe, na ndo maana kigugumizi kikubwa namna hii,

Lakini wacha watuchezee kuna siku yao yaja upuuuzi wote huu utajulikana na ndo hapo watatamani milima iwaangukie!

Wito,

La msingi kwa sasa tuelekeze nguvu zetu kwa wahusika wengine wakuu kama akina Gray Mgonja ikibidi nao wafe kikweli kweli ama kisanii sanii kama Ballali ama la waelekee makazi mapya ya segerea.
 
Balali is dead , kwa wale ambao hamtaki kuamini hebu tupeni sababu kwa nini mnataka wengine waamini kuwa huyu hajakufa?

Zitawekwa picha humu juu ya atakavyokuwa akionekana kwenye geneza na pia za uchunguzi wa hospitali ...subira huvuta kheri.

Mpaka Kieleweke,

Hizo picha si mungeanza kuziweka tokea alipolazwa hospitalini? Si mungeruhusu Watanzania wote wanaojiweza waende kuuaga mwili wake? Si mungesaidia kurudisha mwili wake TZ, kwenye nchi yake, kwa ndugu zake ili wote wamuage kwa mbwembwe zote?

Tumeona cinema na real life stories jinsi watu walivyokufa, kuzikwa na ndugu na baadaye wanaonekana wazima. Unafikiri picha pekee zitatusaidia nini kwenye hili?

Wasipoweza kujibu maswali ambayo wananchi tunauliza, naamini wananchi hatuwezi kuamini kabisa.

Watoe hospitali alipokuwa amelazwa na mengine waachieni waandishi wa habari, watafuatilia inavyotakiwa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…